Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Katika jambo ambalo mimi binafsi linanishangaza ni namna ambavyo unaweza kuta mtu kama ndugu yako, rafiki yako, jirani yako, classmate wako, na mtu yeyote ambaye kidogo mnaukaribu anachukia wewe ukifanikiwa, au anakubania connection, au anakuchongea ufukuzwe kazi, au hataki upige hatua kimaendeleo, au anataka uzidi kuyumba kimaisha.
Lakini mtu au watu wa aina hii wanakufanyia yote haya bila kusahau kuwa wewe upo kwenye circle au mzunguko wake wa maisha, kwamba akipata shida yoyote ile yenye kuhitaji msaada wa watu wengi basi na wewe utakuwemo miongoni mwa watu watakaotakiwa kutoa msaada. Mfano unataka uchangiwe harusi, uchangiwe msiba, uchangiwe matibabu au msaada wowote wa kibinadamu, unakuwa umemuweka mtu uliyembania kwenye wakati mgumu, kwa sababu unaweza kuta bado anateseka mtaani hana namna ya kuweza kukusaidia hata kihisia (emotionally), au kifedha (Financially).
Labda husingembania, au kuchukia kupiga hatua kwake... Uenda angekuwa kwenye nafasi nzuri ya kiuchumi, au kimaisha kiasi kwamba ungekwama kwa namna moja au nyingine basi huyo mtu angekupa backup kubwa kimaisha, mfano kusaidia familia yako, kukusadia wewe kwenye nyakati ambazo umekwama na kadharika.
Hivyo basi tuache kuchukia watu kimaendeleo au kuwabania, maana hao hao muda mwingine hapo badae ndio tutahitaji support yao kimaisha. Saidia watu wanaokuzunguka au waliopo kwenye circle yako ya maisha kadri mkono wako utakapofika bila kujali outcome yake.
Na hivyo ndivyo watu wanavyofanikiwa, maana wanakuwa na backup ya watu wengi, ambapo inakuwa ni rahisi wao kukusaidia pale unapotaka kusonga mbele. Husuda, chuki, na fitina hazitakupeleka popote zaidi ya motoni au kupata karma mbaya, tupendaneni au tusaidianeni mpaka pale mkono wetu utakapofika, hivyo ni rahisi hata kwa uliyemtendea mema kukulipa fadhila nzuri hapo badae.