Kabidhi Imani yako kwa Marafiki ila siyo Ndugu wenye Chuki, Dharau na Unafiki

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akakuombea mabaya ila Ndugu kuombeana mabaya hata Kufa Kwako ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa Mnafiki dhidi yako ila kwa Ndugu Kukusanifu huku akikuchekea ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaona kuna Fursa ya Ajira na asikuunganishe ila ni Nadra mno kwa Ndugu kutaarifiana kuhusu upatikanaji wa Fursa za Kimafanikio.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha kuwa upande wako pale ukiwa na Changamoto za Kimaisha ila Ndugu watakuwa nawe huku wakiwa Wanakusimanga na hata kukuona Kero.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa anakuteta na hata Kukuharibia ila Ndugu wengi wana huu Utamaduni wa Kuharibiana na Kuteta tena wengine unakuta Mafanikio yao Kimaisha yametokana na huyo Wanayemteta.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana ukiwa na shida na kumuomba Msaada akaanza Kukutangazia kwa Watu ila Ndugu wengi ukiwa na Uhitaji wako tegemea Kusaidiwa nae ila Kutangazwa kwa Ndugu wote wa Ukoo.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha hata Siku Mbili au Tatu asiwasiliane nawe ila kwa Ndugu mnaweza kupitisha hata miaka miwili bila Kuwasiliana na Kuwasiliana kwenu kutakuwa ni kupeana tu taarifa za Msiba au kuletewa Kadi ya Harusi ya Ndugu ya Ukoo.

Jitahidi sana utunze Marafiki ulionao, usiwakosee kwani hao ndiyo Kiuhalisia wenye Uchungu na Upendo nawe kuliko Ndugu ambao ukiwa nacho Wanakuthamini ila Ukianguka kimaisha Wanakukwepa, Wanakudharau, Wanakucheka na hata kuzidi tu Kukuombea mabaya.

Mwenyezi Mungu awabariki Marafiki.
 
Ndo unajuwa leo ila kuna marafiki nao vichomi utajuta kuwajuwa, rafiki asie imara ni yule ambae mshagombana na mnaelewana lazima mpitie iyo test , ktk ndugu inategemea kama mmeishi pamoja tangia utoto wenu
 
Mfano unakubaliana nami kuwa 75% ya Watanzania walioko Ulaya, Marekani na hata Afrika Kusini walipata Connections za Marafiki zao kwenda huko na hata kusaidiwa Nauli, ila siyo Ndugu zao walioko huko au walioko Tanzania ila wenye Uwezo na Nafasi?
 
Tafadhali rejea kufanya upya Utafiti wako.
Mkuu mimi binafsi baada ya kutoka chuo na mambo kuchacha nilifulia sana kiasi cha kuuza simu, lakini ndugu walinibeba wakanifungulia biashara, ikafa wakanifungulia nyingine.

Mda huo marafiki wako mbali, mpaka leo nikipata shida yoyote nahesabu ndugu tu ndo watanisaidia.

Ndo maana nikasema kama mlilelewa pamoja toka mnakua, mkalelewa kwa upendo lazima mtashikana.

Mla nawe hafi nawe bali mzaliwa nawe
 
Yes apo ktk kukuwa wote na kulelewa pamoja ina kuwa njema sana
 
Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akakuombea mabaya ila Ndugu kuombeana mabaya hata Kufa Kwako ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa Mnafiki dhidi yako ila kwa Ndugu Kukusanifu huku akikuchekea ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaona kuna Fursa ya Ajira na asikuunganishe ila ni Nadra mno kwa Ndugu kutaarifiana kuhusu upatikanaji wa Fursa za Kimafanikio.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha kuwa upande wako pale ukiwa na Changamoto za Kimaisha ila Ndugu watakuwa nawe huku wakiwa Wanakusimanga na hata kukuona Kero.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa anakuteta na hata Kukuharibia ila Ndugu wengi wana huu Utamaduni wa Kuharibiana na Kuteta tena wengine unakuta Mafanikio yao Kimaisha yametokana na huyo Wanayemteta.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana ukiwa na shida na kumuomba Msaada akaanza Kukutangazia kwa Watu ila Ndugu wengi ukiwa na Uhitaji wako tegemea Kusaidiwa nae ila Kutangazwa kwa Ndugu wote wa Ukoo.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha hata Siku Mbili au Tatu asiwasiliane nawe ila kwa Ndugu mnaweza kupitisha hata miaka miwili bila Kuwasiliana na Kuwasiliana kwenu kutakuwa ni kupeana tu taarifa za Msiba au kuletewa Kadi ya Harusi ya Ndugu ya Ukoo.

Jitahidi sana utunze Marafiki ulionao, usiwakosee kwani hao ndiyo Kiuhalisia wenye Uchungu na Upendo nawe kuliko Ndugu ambao ukiwa nacho Wanakuthamini ila Ukianguka kimaisha Wanakukwepa, Wanakudharau, Wanakucheka na hata kuzidi tu Kukuombea mabaya.

Mwenyezi Mungu awabariki Marafiki.
Mimi hata maendeleo yangu niliyonayo ni mchango wa marafiki.

Asilimia 90 ya ndugu upande wa baba huwa ni washenzi
 
Inategemea Mi ndugu zangu wako poa kinoma kuna brother wangu tunapatana nae kinoma kipindi niko bize alikua ananitunzia hela zangu nampa anaweka kwenye biashara zake paka ikafika 20M na nilipoanza kuzitaka alirudisha zote ndan ya mwaka mmoja tu tena sio ndugu wa tumbo moja n binamu tu, ndio mana anazidi kufanikiwa Mungu azidi kumbariki My Brother azidi kutajirika zaidi na zaidi
 
Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akakuombea mabaya ila Ndugu kuombeana mabaya hata Kufa Kwako ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa Mnafiki dhidi yako ila kwa Ndugu Kukusanifu huku akikuchekea ni Jambo la kawaida.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaona kuna Fursa ya Ajira na asikuunganishe ila ni Nadra mno kwa Ndugu kutaarifiana kuhusu upatikanaji wa Fursa za Kimafanikio.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha kuwa upande wako pale ukiwa na Changamoto za Kimaisha ila Ndugu watakuwa nawe huku wakiwa Wanakusimanga na hata kukuona Kero.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akawa anakuteta na hata Kukuharibia ila Ndugu wengi wana huu Utamaduni wa Kuharibiana na Kuteta tena wengine unakuta Mafanikio yao Kimaisha yametokana na huyo Wanayemteta.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana ukiwa na shida na kumuomba Msaada akaanza Kukutangazia kwa Watu ila Ndugu wengi ukiwa na Uhitaji wako tegemea Kusaidiwa nae ila Kutangazwa kwa Ndugu wote wa Ukoo.

Sijawahi kuona Rafiki mnayeshibana akaacha hata Siku Mbili au Tatu asiwasiliane nawe ila kwa Ndugu mnaweza kupitisha hata miaka miwili bila Kuwasiliana na Kuwasiliana kwenu kutakuwa ni kupeana tu taarifa za Msiba au kuletewa Kadi ya Harusi ya Ndugu ya Ukoo.

Jitahidi sana utunze Marafiki ulionao, usiwakosee kwani hao ndiyo Kiuhalisia wenye Uchungu na Upendo nawe kuliko Ndugu ambao ukiwa nacho Wanakuthamini ila Ukianguka kimaisha Wanakukwepa, Wanakudharau, Wanakucheka na hata kuzidi tu Kukuombea mabaya.

Mwenyezi Mungu awabariki Marafiki.
Umeongea kweli mkuu

Uishi Maisha marefu mkuu
 
Back
Top Bottom