Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Pasco umetisha baba...!!!tunahitaji majibu ya hayo maswali...lakini tunamtaka pia Daudi Bashite Halisi ajitokeze,na kama amekufa tupate cheti chake cha kifo.
 
Hapa hatuna haja ya kumuuliza Makonda maswali yasiyo na msingi. Muhimu ni kuunga mkono kupinga madawa.

Makonda hapa pa madawa ya kulevya amefanya kazi nzuri sana hata kupita Watanzania wooooote.

Kuhusu jina lake???? HAITUHUSU WALA SI MASILAHI YETU.

Letu tunapenda tufukue mambo ya kishetani yote na kuyamaliza kwa nguvu zote.
Wewe sio bure lazima kama sio DAUDI BASHITE MWENYEWE basi una maslahi nae..kwnn tusimuulize elimu YAKE.. kama kiongozi mkubwa aliyepewa dhamana ya kuongoza mkoa anakuwa MUONGO. tutamuamini kwa lipi?VYETI fake...maadili hana ya uongozi ..wanawake wa mjini WOTE wake...na kila analolianzisha anashindwa...alianzisha operation MASHOGA wakati hao ndy rafiki zake.. operation ya MADAWA ya KULEVYA rafiki zake hakuwataja na hata akienda huko south anakuwa nao...operation VYETI fake yeye ndy mtuhumiwa namba moja..kujilimbikizia Mali yeye YUPO.....mambo ya shisha kumbe alikuwa anapewa posho..aliponyimwa mgao akaanza KUPAYUKA ..hii issue ya MADAWA ni marufuku Dunia nzima hakuna anayepinga OPERATION....YEYE..ANGEWAACHIA POLICE NA KITENGO CHA MADAWA...ndio wenye weledi wa kufanya kazi hizo..na sio YEYE....mambo ya maendeleo ya mkoa yanamshinda anaparamia mambo yasiyomuhusu...sisi tunataka watuletee MAENDELEO.. shule hazina walimu...maisha yanapanda ...bidhaa zinapanda BEI hovyo..majambazi yanatisha amani....mambo mengi tu ya kuendeleza inchi hii...au yeye kwa vile VYETI VYA KUUNGA anategemea na watoto wetu pia tuwanunulie VYETI? inashangaza sana..mtuana VYETI fake halafu anaongoza watu wenye wenye VYETI halisi....tena anakomalia kabisa wenzie wapekuliwe VYETI.. Wakati yeye mwenyewe VYETI sio vyake....
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Pascal Mayalla
Paskali we ni Mwandishi wa kujitegemea tena wa habri za kiuchunguzi. Kweli suala kama hili linkosa majibu kana kwamba makonda kaziliwa na kusimea sayar nyingine. NawazA tu hapa nilipo mm kweli naweza ficha details zangu mtu asizijue. Nina majirani,ndugu jamaa na marafiki. Kwann wasiojiwe hao kwa sharti la kutotaja majina yao na kupa info zangu..
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Ndugu yangu Pascal, umesahau kutuambia sisi ndugu na jamaa tumtetee Makonda yupi kati ya hawa watatu, yaani Makonda mwandishi wa habari, Makonda Mkuu wa mkoa au makonda Bushet Christian
 
Utetezi umeanza

PAUL MAKONDA:

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community & Economic Development (CED).

18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community & Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
 
Salaam wakuu,

Nimeona bora niulize hili jambo hapa ili wenye majibu waweze kunijuza. Kama Daudi Bashite alizaliwa na taarifa za kuzaliwa kwake zipo, kama alisoma shule ya msingi then sekondari na taarifa zipo na kisha kupotea katika mazingira ya kutatanisha baada tu ya matokeo ya form four kuonyesha kuwa amefeli, je ni jitihada gani zilifanyika kumtafuta huyu kijana wetu? Ni miaka zaidi ya 15 sasa haijulikani kijana wetu yupo wapi, haijulikani kama ni mzima au la! Na tumekaa kimya tu bila kufikiria kuwa yule ni mtanzania mwenzetu.

Leo hii ni siku ya 105 tangu kuripotiwa kupotea kwa Ndugu Ben Saanane ambaye analiliwa kila kona ya nchi, lakini kwa Daudi ni miaka mingi imepita bado tupo kimya. Hatujui kama aliliwa na wanyama wakali, hatujui kama alijitumbukiza kwenye acid (tindikali), hatujui chochote.

Bring back our Daudi!
 
Daudi Bashite hajapotea, yupo katulia tuli kama mkuu wa mkoa wa wajanja, mkoa wa Dar. Ni jina tu la Daudi Bashite limepotea ingawa jina la Daudi linatumika kama kawaida. Hoja yako inaongeza wigo kwa wale wanaotafuta ukweli wa jambo hili kufuatilia zaidi. Lakini pia tusubiri wale wageni toka Kolomije wataongea nini kanisani kwa Gwajima na familia ya ufufuo na uzima jumapili hii? The drama continues
 
Tumechoka na humu wimbo wa Bashite,,
Asubuh, mchana,, Alasili na Usiku kila ukiingia humu Jf unakutana na wimbo huu huu wa Bashite.
 
Hapa alikua anajiiata a.k.a Shite boy
ea63f4b47eaa3ea550f01543b9c2a568.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom