Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,689
119,326
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuhamasisha a mass mobilization ya kupata kundi kubwa la watu, kuunga mkono kwa dhati, juhudi kubwa zinazofanywa na Mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Christian Makonda, katika vita mbalimbali, ikiwemo vita hii v kubwa ya dhidi ya madawa ya kulevya yanayowaharibu vijana wetu na kupoteza nguvu kazi muhimu ya taifa.

Makonda ameamua kulivalia njuga tatizo hili kwa kujitoa mhanga kuwaumbua kwa kuwataja wazi wazi na hadharani wabwia unga, wauza unga na mapapa wa mihadarati, jambo lililowaogopesha wauza unga, hivyo kuamua kumchafua Makonda kwa kila aina ya uongo.

Hivyo hili ni bandiko la wito kwa kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki wa dhati, wanaomjua Makonda kwa karibu na kwa ukweli, njooni tujitokeze kwa wingi, kumtetea Makonda tunayemfahamu dhidi ya uongo na uzushi unaozushwa na kusambazwa na mapapa wauza unga kupitia kwao na vibaraka wao na wapambe wao kumsingizia uongo. Paul Makonda kuwa ameghushi majina, amegushi vyeti, amejiunga na kusoma chuo kikuu kwa cheti cha kughushi na mpaka sasa anatumia majina ya kughushi!.

Tangu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina hadharani, live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, vibaraka wao, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasiolitakia mema taifa hili, wameanza kampeni chafu ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema na taifa hili, wanaweza kutusaidia kumjibia.

Maswali ni haya.
  1. Paul Christian Makonda alizaliwa lini, wapi, na alipozaliwa alipewa jina gani?.
  2. Kwenye chetu chake cha kuzaliwa majina matatu ya wazazi wake wote wawili ni nani?.
  3. Pauli Christian Makonda alianza shule Kolomije, Jee aliandikishwa shule ya msingi, lini, wapi na kwa majina matatu ya yapi?.
  4. Alipohama shule ya msingi Kolomije akiwa darasa la 4 na kuhamia Mwanza, alihama kwa majina matatu yapi? .
  5. Alimaliza darasa la 7 mwaka gani kwa majina matatu yapo na matokeo yake ya shule ni msingi ni yapi?,
  6. Baada ya kumaliza darasa la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani na kwa majina matatu gani?.
  7. Alimaliza sekondari wapi, lini kwa majina matatu yapi na matokeo yake ni yapi, hivyo sasa ana cheti cha kuhitimu cha NECTA kina majina gani?.
  8. Alipomaliza alijiunga na Chuo cha uvuvi Nyegezi, jee alijiunga lini kwa kozi gani na kwa majina gani?.
  9. Baada ya Nyegezi alijiunga chuo cha uvuvi cha Mbegani mwaka gani, kozi gani na kwa majina gani? .
  10. Baada ya Mbegani alijiunga chuo kikuu cha ushirika, Moshi mwaka gani, kozi gani kwa majina gani?.
Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wale wote wanaotaka kumzushia kuwa Paul Christian Makonda, hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Update 30/08/2018
Hata hili sakata la Makontena, kuyatoza kodi ni juhudi za kutaka tuu kumkwamisha juhudi zake kuwapatia waalimu wa Dar es Salaam vifaa vya ofisi, na wakati huo huo, kuwakatisha tamaa Watanzania walioko nje ya nje kuisaidia Tanzania.

Natoa wito kwa Watanzania marafiki wa Makonda, tujitolee kumchangia hizo bilioni 1.2 za kodi, makontena hayo yalipiwe kodi, waalimu wetu wapatiwe samani zao, na sakata hili lipite.
Hivyo huu nao pia ni upepo tuu na utapita!.
P
Update 3 -20/02/2020
Leo February 20/02/2020 ni miaka 3 tangu bandiko hili lipande, nikisisitiza tumtete Makonda. Hata hili sakata la kunyima viza kuingia Marekani kwa kumsingizia mambo ya uongo, ni muendelezo tuu, hivyo wote wenye mapenzi mema na taifa letu, tusikubali, tujitokeze kumtetea kwa kupangua hoja kwa hoja, tuhuma zote zilizoelekezwa kwake na mabeberu hawa wa Marekani, kwa kuanza na kuipa hongera serikali yetu kuwapuuza na kutowajibu chochote huku Makonda akiendelea kupiga kazi.

P
 
Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
Christian hili jina alipewa na mwalimu wake wa darasa wakati yupo form two maana darasa zima yeye peke yake ndo alikuwa Mkristo
Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
 
Ng'wanangwa bwana!Hiyo ni kwa wenye akili tu!Mkuu Paskali,nimekuelewa.

Hoja au ombi lako kwa wale wote wamtambuao mpigana vita uloitaja ni jambo jema sana.Hao ndiyo watasema na kutueleza ama ni kweli au si kweli ktk yote anenewayo huyo ulomtaja.

Shime,njooni nyote mumfahamuyo kiranja tajwa.
 
Haki itamtetea. Makonda hahitaji utetezi wetu. Hata ukiwepo huo ni mdogo sana. Haki na kweli itamtetea.Historia itamtetea. Hata sasa unaona kila kiongozi wa nchi yetu wa ngazi yoyote akisimama anaunga mkono vita hii. Zile kelele zilizokuwepo za kumkatisha tamaa Makonda zimeendelea kupungua. Hata hiyo iliyojitokeza itapungua. Si unaona hata Marekani. Walimbeza sana Obama. Leo amemaliza kazi kweli inamtetea. Uchumi mzuri, ajira imepanda, hata hawataki Trump ajichotee sifa kwa uchumi ulioinuka wanasema "ameukuta Obama kautengeneza."Hivyo ndivyo historia inavyofanya na siyo ile ya muda mrefu tu, hapana ya muda mfupi tu. Ya zama hizi hizi tu. Sizuii mtu kumtetea Makonda. La hasha. Atetewe tu.Ila utetezi wa kudumu wa Makonda ni matokeo ya kuthubutu kwake yanayoonekana hata sasa. Dawa za Kulevya zimepungua mtaani, watumiaji wanajisalimisha kwenye vyombo husika ili kupata msaada, vijana wetu wanaona "mubashara" jinsi madawa ya kulevya yanavyoweza kuua mara moja. Wanajifunza. Punde tutaona watu wengi wakijitolea kuwasaidia watu hawa wapate "rehab'. Serikali nayo itaendelea kuweka mikakati mizito ya kuwasaidia ndugu zetu hawa. Kamishna alidokeza kidogo nia hiyo katika hotuba yake. Mashirika ya dini nayo sasa yataongeza nguvu kuwapokea waathirika hawa na kuwasaidia kimwili na kiroho. Natamani siku ile tutakapoona wale magwiji wa madawa wenyewe wakijisalimisha Polisi kama alivyofanya Pablo japo alijaribu sana kupambana na sheria na haki alijisalimisha tu ili mambo yaishe.
 
Naunga mkono hoja asilimia 100%. Tena ikiwezekana, Alibatizwa kanisa katoliki wapi, na kupewa sacrament ya kwanza wapi. Aliandikwa darasa gani na kama kuna mtoto mwingine anaye mkumbuka pale waliposoma pamoja?? Mbona nawakumbuka wote nilosoma nao Std.1 mwaka ule 1960?? Tena wapo ka 4 ninaowajua wako hai?? Tumatetee Makonda tafadhali, tukiliweza hili tu, tutamaliza mzuka wote.
 
Kwenye hizi tuhuma za Makonda kuna uongo mwingi kama sio zote. Mfano, tuhuma za kukarabati ofisi yake wakati harakati za kukarabati ofisi zilianza kabla hata Makonda hajashika iko cheo cha mkuu wa mkoa!
 
Back
Top Bottom