Ndugu, jamaa na marafiki njooni tumtetee Makonda dhidi ya mapapa wauza unga wanaomzushia

Haki itamtetea. Makonda hahitaji utetezi wetu. Hata ukiwepo huo ni mdogo sana. Haki na kweli itamtetea.Historia itamtetea. Hata sasa unaona kila kiongozi wa nchi yetu wa ngazi yoyote akisimama anaunga mkono vita hii. Zile kelele zilizokuwepo za kumkatisha tamaa Makonda zimeendelea kupungua. Hata hiyo iliyojitokeza itapungua. Si unaona hata Marekani. Walimbeza sana Obama. Leo amemaliza kazi kweli inamtetea. Uchumi mzuri, ajira imepanda, hata hawataki Trump ajichotee sifa kwa uchumi ulioinuka wanasema "ameukuta Obama kautengeneza."Hivyo ndivyo historia inavyofanya na siyo ile ya muda mrefu tu, hapana ya muda mfupi tu. Ya zama hizi hizi tu. Sizuii mtu kumtetea Makonda. La hasha. Atetewe tu.Ila utetezi wa kudumu wa Makonda ni matokeo ya kuthubutu kwake yanayoonekana hata sasa. Dawa za Kulevya zimepungua mtaani, watumiaji wanajisalimisha kwenye vyombo husika ili kupata msaada, vijana wetu wanaona "mubashara" jinsi madawa ya kulevya yanavyoweza kuua mara moja. Wanajifunza. Punde tutaona watu wengi wakijitolea kuwasaidia watu hawa wapate "rehab'. Serikali nayo itaendelea kuweka mikakati mizito ya kuwasaidia ndugu zetu hawa. Kamishna alidokeza kidogo nia hiyo katika hotuba yake. Mashirika ya dini nayo sasa yataongeza nguvu kuwapokea waathirika hawa na kuwasaidia kimwili na kiroho. Natamani siku ile tutakapoona wale magwiji wa madawa wenyewe wakijisalimisha Polisi kama alivyofanya Pablo japo alijaribu sana kupambana na sheria na haki alijisalimisha tu ili mambo yaishe.
Maneno mengi,mara haki itamtetea, mara matokeo yatamtetea,, mbwe mbwe zote za nini? Ugumu uko wapi kuthibitisha kuwa mimi ndio mwenye jina? It take only second kuondoa haya maneno.. Uongo ukiachwa huwa ukweli.. Akanushe kama sio kweli.. Mbona vingine wanakanusha kwa haraka na nguvu zote.. Until then..ila for now tutabaki na hili
 
Kweli hata hukuomba mtu akishauri kabla ya kupost hapa!!!
Mi nilidhani utakuja na data za uhakika zinazoeleza dukuduku la wengi ,badala yake unataka sie tutafute majibu! Ama kweli inaitwa kukurupuka!!!
 
hivi mnaombeza Makonda ni kipi mmecholifanyia taifa lenu? Makonda ni mkuu wa mkoa bora kabisa tangu tuwe na jamhuri hii tukufu, hajawahi kutokea mkuu wa mkoa akawa mbunifu na muwajibikaji kama Makonda. kama mnaukweli wwte kumuhusu si muuweke hapa na ushahidi wake kama ilivyo ada ya GT mubashara tuone huko alikoazima cheti!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Katika vile ulivyovibuni kipi ambacho amefanikiwa japo kwa 50% ?
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.
Who is Idd Azani?
 
Hapa inaongelewa juu ya vyeti, na tunataka kumsafisha kwa maneno yanayozagaa mitaani. Hiyo unayosema wewe ni kitu ambayo haiko kwenye discussion hapa....
Hiyo nimetolea mfano kuonyesha kwamba tuhuma dhidi yake zinaweza kuwa ni za kupikwa.
 
Maneno mengi,mara haki itamtetea, mara matokeo yatamtetea,, mbwe mbwe zote za nini? Ugumu uko wapi kuthibitisha kuwa mimi ndio mwenye jina? It take only second kuondoa haya maneno.. Uongo ukiachwa huwa ukweli.. Akanushe kama sio kweli.. Mbona vingine wanakanusha kwa haraka na nguvu zote.. Until then..ila for now tutabaki na hili

Mwenye hoja alinipa like; wewe usipokubailiana na yale niliyooandika kulingana na maudhui na kichwa cha hoja hiyo ni shida yako si yangu. Msomi wa maelezo yangu ataelewa vya kutosha mtiririko wa fikra zangu kulingana na hoja iliyotolewa. Nilijikita kujadili dhana ya kumtetea mtajwa nikichangia hoja kwamba si watu tu waliohamasishwa pekee ndio wanaoweza kutoa utetezi unaofaa kwa mtajwa bali hata mambo mengine zingativu yanaweza pia. Nikayataja kama vile nilivyoyaorodhesha. Hakuna mbwembwe hapo.Nampongeza mleta hoja wa kwanza ( pascali) kwa kuukubali mtazamo wangu ingawa yeye huenda alikuja na mtazamo tofauti. Mleta hoja huyo aliyenipa like simfahamu kwa karibu lakini nimegundua kuwa ni msomi na mwelewa kwa kuukubali upande wangu wa fikra baada ya kuuona una mantiki (reason) ingawa huenda yeye alilenga kitu kingine kabisa. Mleta hoja wa mwanzo kwa hakika anafaa Katika ulimwengu wa wasomi na waandishi. Hongera Pascali.
 
Ngoja nimtetee kidogo
Daudi Albert Bashite hajaghushi vyeti bali majina haya{Paul Christian Makonda) ni yake halali aliyapata kihalali kabisa km ifuatavyo

Paul hili jina alipewa Primary kutokana na kipaji chake cha soka wakati akichezea timu ya shule akifananishwa na Paul Scholes
Christian hili jina alipewa na mwalimu wake wa darasa wakati yupo form two maana darasa zima yeye peke yake ndo alikuwa Mkristo
Makonda hili jina alilipata akiwa form 4 alikuwa na rafiki yake ambaye walikuwa wanarudi pamoja Mwanza likizo na kufanya kazi kwenye daladala hivyo shuleni wakawa wanawaita Makonda

Hilo ndo chimbuko la majina yake wala hajaghushi jamani
Uko sirious!! Yakaingiaje sasa kwenye vyeti hayo majina?!!!
 
Nasikia shule alikua bwege sana kila siku alipata fimbo zamgongini hasa alipo ulizwa orodha ya 9 na 8
 
Mwenye hoja alinipa like; wewe usipokubailiana na yale niliyooandika kulingana na maudhui na kichwa cha hoja hiyo ni shida yako si yangu. Msomi wa maelezo yangu ataelewa vya kutosha mtiririko wa fikra zangu kulingana na hoja iliyotolewa. Nilijikita kujadili dhana ya kumtetea mtajwa nikichangia hoja kwamba si watu tu waliohamasishwa pekee ndio wanaoweza kutoa utetezi unaofaa kwa mtajwa bali hata mambo mengine zingativu yanaweza pia. Nikayataja kama vile nilivyoyaorodhesha. Hakuna mbwembwe hapo.Nampongeza mleta hoja wa kwanza ( pascali) kwa kuukubali mtazamo wangu ingawa yeye huenda alikuja na mtazamo tofauti. Mleta hoja huyo aliyenipa like simfahamu kwa karibu lakini nimegundua kuwa ni msomi na mwelewa kwa kuukubali upande wangu wa fikra baada ya kuuona una mantiki (reason) ingawa huenda yeye alilenga kitu kingine kabisa. Mleta hoja wa mwanzo kwa hakika anafaa Katika ulimwengu wa wasomi na waandishi. Hongera Pascali.
Kumbe wewe u mgeni hapa jamvini. Humjui Paskali Mayala wewe ndio maana hujui "like" yake ina maana gani.
Pole
 
ndg.yangu Cephalocaudo, unashindwa kuona hata hili la bwimbwi leo hii nionyeshe vurugu za mazungu kuanzia magomeni, kinondoni, ilala, sinza, mikocheni na temeke?
 
Mwenye hoja alinipa like; wewe usipokubailiana na yale niliyooandika kulingana na maudhui na kichwa cha hoja hiyo ni shida yako si yangu. Msomi wa maelezo yangu ataelewa vya kutosha mtiririko wa fikra zangu kulingana na hoja iliyotolewa. Nilijikita kujadili dhana ya kumtetea mtajwa nikichangia hoja kwamba si watu tu waliohamasishwa pekee ndio wanaoweza kutoa utetezi unaofaa kwa mtajwa bali hata mambo mengine zingativu yanaweza pia. Nikayataja kama vile nilivyoyaorodhesha. Hakuna mbwembwe hapo.Nampongeza mleta hoja wa kwanza ( pascali) kwa kuukubali mtazamo wangu ingawa yeye huenda alikuja na mtazamo tofauti. Mleta hoja huyo aliyenipa like simfahamu kwa karibu lakini nimegundua kuwa ni msomi na mwelewa kwa kuukubali upande wangu wa fikra baada ya kuuona una mantiki (reason) ingawa huenda yeye alilenga kitu kingine kabisa. Mleta hoja wa mwanzo kwa hakika anafaa Katika ulimwengu wa wasomi na waandishi. Hongera Pascali.
Pascal Mayalla hata ukimtukana kwenye thread yake anakupa like, yuko tofauti na wengine hadi uwasifie ndo wanakupa like. kama ulidhani kukupa like ndo kukubali hoja yako basi unatakiwa ufikiri upya maana hata alichoandika ni fumbo.
 
mbona povu dogo,kama yule mihemko wenu..

wacha wenye hoja wakajenge hoja mahakamani..
endelea kumwaga povu..
 
Hiyo nimetolea mfano kuonyesha kwamba tuhuma dhidi yake zinaweza kuwa ni za kupikwa.

Anaweza kuthibitisha mwenyewe kuwa hicho kinachosemwa ni cha uongo. Kwenye masuala ya elimu hakutakiwi kuwa na politics. Mtu akikwambia huna mtoto wakati una watoto watano, unaweza kukaa kimya ukaacha kujibu chochote kwa sababu that is personal. Lakini mtu akisema ulitumia cheti cha ku-forge na wakati huo wewe ni Mbunge wa jimbo fulani, that is not personal. You have to speak....
 
Nini kimewashinda hao wanaoandika hizi tuhuma kutafuta ushahidi. Wangeweza kwenda baraza la mitihani na kutafuta ushahidi!

Watueleze utaratibu wa kukarabati ofisi ya mkuu wa mkoa ilianza mwaka gani na Makonda aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa lini?

Kila linaloandikwa bila hata chembe ya ushahidi wakati ushahidi unaweza kupatikana kirahisi ukihamua kujibu utajikuta hata unashindwa kutekeza majukumu muhimu!

That being said, Makonda atajibu hizo tuhuma kesho kupia redio.
 
shida nini mpaka leo ? maana mimi ukidoubt cheki changu hata sasa hivi nascreenshot tu au hana ?
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la Mass Mobilization Kuunga Mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Katika Vita Hii ya Madawa ya Kulevya Kwa Kuwaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki, Wanaomjua Makonda Kwa Karibu, Njooni Tujitokeze Kwa Wingi ,Kumtetea Makonda Tunayemfahamu Dhidi ya Uongo na Uzushi Anaozushiwa na Mapapa Wauza Unga Kupitia Kwa Vibaraka Wao Kumsingizia Ameghushi Majina, Amegushi Vyeti, Amesoma Chuo Kikuu Kwa Chati Cha Kughushi na Mpaka Sasa Anatumia Majina ya Kughushi!.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaumbue wauza unga wakuu kwa kuwataja majina live, tena bila kupepesa macho wala kumungunya maneno, mafisadi hawa, wapambe wao, makuwadi wa ufisadi na wale wote wasilitakia mema taifa hili, wameanza kampeni ya kumvunja moyo na kumkatisha tamaa Makonda kwa kumzushia kila aina ya uongo.

Sisi tunaounga mkono vita hii, tunamsisitiza akaze uzi na asitetereke, wala asipoteze muda wake wa thamani kujibu uongo wowote wa kwenye mitandao, yeye achape tuu kazi, na majibu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake, hazina haja kabisa ya kujibiwa na Makonda mwenyewe bali ndugu zake na marafiki zake wenye nia njema, wanaweza kutusaidia.

Maswali ni haya.
1. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
2. Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale
3. Alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani? .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5.Alitumia majina gani matatu sekondari, tukiisha pata tuu majina, tutayaona matokeo yake ya Necta hivyo kuwakata vilimilimi wazushi wote.
6. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa majina gani? .

Majibu ya maswali hayo, yatawakata kabisa vilimilimi wote wanaotaka kumzushia kuwa hakusoma sekondari, alipata Div. 0 na kwamba aliiba cheti cha mtu!.

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda Kwenye Vita ya hii ya madawa ya kulevya dhidi ya mapapa wa madawa wanaotaka kumchafua Makonda wetu.

Paskali.

Yeye ashirikiane nao sie tumtetee,atueleze kwanza utajiri wake wa gafla kaupataje,kama hakupewa na manyangumi wa unga,kiongozi ataeshiriki na ikbar vyovyote iwavyo ni mtu wa kupigwa vita kila kona maana huyu ndo li anaconda lenyewe duniani linajulikana
 
Back
Top Bottom