Ndugai: CAG anaingilia mambo yasiyomhusu

Ndugai: CAG anaingilia mambo yasiyomhusu

Simchezo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
463
Reaction score
374
Wadau,

Leo katika kipindi cha tuongee asubuhi cha radio one, Naibu Spika Ndugai amepinga vikali wazo la CAG kwamba wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za masharika ya umma. Ndugai akiongea kwa jazba amesema CAG anaingilia mambo ambayo hayamuhusu na amekuwa akitoa ushauri mbovu ambao hautekelezeki na usio na mashiko, ameendelea kusema kwamba CAG anaingilia kazi zisizomuhusu.

Najiuliza nini kimemfanya Mh Ndugai apandwe na jazba kiasi kile?
 
Wadau,
Leo katika kipindi cha tuongee asubuhi cha radio one, Naibu Spika Ndugai amepinga vikali wazo la GAG kwamba wabunge wasiwe wajumbe wa bodi ya masharika ya umma. Ndugai akiongea kwa jazba amesema CAG anaingilia mambo ambayo hayamuhusu na amekuwa akitoa ushauri mbovu ambao hautekelezeki na usio na mashiko, ameendelea kusema kwamba CAG anaingilia kazi zisizomuhusu.
Najiuliza nini kimemfanya Mh Ndugai apandwe na jazba kiasi kile?
Ukiona hivyo ujue yupo kwenye mashamba ya NARCO-KONGWA
 
Tuseme kama ni kweli CAG anaingilia yasiyomhusu,kweli kwenye radio ndio mahali pa kulalamikia?

Hawana vikao vya kujadili hayo?

Au ndio Liwalo na Liwe?

Kwa mwenendo huu, tutasikia mengi sana kabla ya uchaguzi ujao. ....
 
Ndio maana Rasimu ya Mzee Warioba hawaitaki kwani kwao CCM ni sawa na kumeza Klorokwini

Umeona eh!Na walivoenda kwa Mama Maria Nyerere wakapigwa za uso,wakarudi oh unajua yule Mama amechanganyikiwa.Wale wote watakaosema kweli ni lazima wawe wamechanganyikiwa.
 
Wadau,

Leo katika kipindi cha tuongee asubuhi cha radio one, Naibu Spika Ndugai amepinga vikali wazo la CAG kwamba wabunge wasiwe wajumbe wa bodi ya masharika ya umma. Ndugai akiongea kwa jazba amesema CAG anaingilia mambo ambayo hayamuhusu na amekuwa akitoa ushauri mbovu ambao hautekelezeki na usio na mashiko, ameendelea kusema kwamba CAG anaingilia kazi zisizomuhusu.

Najiuliza nini kimemfanya Mh Ndugai apandwe na jazba kiasi kile?
Sasa kati ya Utoh na Ndugai nani mwenye ushauri wa hovyo? iko wazi kuwa CAG anajaribu kuimplement uwajibikaji na uwazi zaidi kwa kuondoa conflict of interest ... Ndugai anajulikana kuwa ni mchumia tumbo kama wachumia tumbo wengine wengi walioko ndani ya CCM! Utoh alicheza sana walipompatia nguvu za kisheria ambazo zinamkinga hadi leo! otherwise ungekuta wameshamtimu long time ...
 
Ndugai Tatizo lake hajui kitu kinachoitwa mgongano wa kimaslahi. katika mihimili ya kikatiba Mbunge ni mhimili na pia Serikali Mhimili hiyo mbunge kuwa mjumbe wa mashirika haya kunakuwa na mgongano wa kimaslahi pale inapotekea shirika kufanya vibaya na mbunge kama mjumbe wa bodi ya shirika husika ni sehemu ya tatitzo kwani atashindwa kuisimamia serikali ipasavyo
 
CAG anachoongea ndio usahihi wenyewe ... hivi wabunge watajikaguaje wakiwa wakuu wa board? jamani ubinafis utatumaliza.Ndugai acha ubinafsi.
 
Ndugai Tatizo lake hajui kitu kinachoitwa mgongano wa kimaslahi. katika mihimili ya kikatiba Mbunge ni mhimili na pia Serikali Mhimili hiyo mbunge kuwa mjumbe wa mashirika haya kunakuwa na mgongano wa kimaslahi pale inapotekea shirika kufanya vibaya na mbunge kama mjumbe wa bodi ya shirika husika ni sehemu ya tatitzo kwani atashindwa kuisimamia serikali ipasavyo

Hakika tumeamini, tumbo likiwa ndio kichwa chako au chanzo chako cha mawazo, hata uwe unaona vyema, macho huwa kipofu...huyu Ndugai, sababu tu ya tumbo anajisahaulisha kabisa ethics, code of conducts na conflicts of interest! amekuwa akishiba sana kupitia ujumbe ktk mashirika haya ya umma bila kujua amekuwa anaathiri vipi maamuzi yanayomhitaji yeye na wabunge wengine walio ktk deal kama hizo...yeye anajitetea kuwa kutokuwaweka ktk boards ni 'kuwafanyia ubaguzi'...kasoma utawala?...useless man!
 
Ndugai yuko kule NGORONGORO authority....

Utupu wa Ndugai kichwani unadhidi kujulikana.hivi hajui kabisa kwa nini sisi tumeshauri hivyo hajui.tuseme kwamba sisi tumewataka tu bila kuweka sababu?haoni kabisa kwa mbunge member wa bodi kuja kuhoji maamuzi ya bodi hiyo hiyo kwa mgongo wa kamati ya bunge.
 
Back
Top Bottom