Spika Ndugai alilewa Ugimbi wa Madaraka kabla ya Ujio Magufuli; Abebeshwe zigo lake...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
1066521
Na. M. M. Mwanakijiji

Wapo baadhi ya watu ambao wanaona kana kwamba Spika Job Ndugai ameanza leo kutumia madaraka yake vibaya na wakati mwingine vibaya zaidi kila akikalia kiti cha Spika. Wengi wanaliona hili hasa kwenye hili sakata la CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali). Ndugai anaonekana kama ni mbabe fulani hivi. Na kwenye sakata la Lissu na hata mambo mengine anavyozungumza wakati mwingine unaamini kabisa kuwa anapokaa kwenye kile kiti cha enzi na joho lake la korosho, zabibu, na mabibo huwa anajisikia nguvu fulani hivi.

Matokeo yake kila anachofanya au asichofanya kinahusishwa na Rais Magufuli. Wapo ambao wanaamini kuwa anapokea na anatendea kazi maagizo toka Ikulu. Inawezekana kuna ukweli lakini Spika wa Tanzania hayuko chini ya Rais na hapaswi kujitendea kama yuko chini (subjected) kwa Rais.

Yeye ni mkuu wa Mhimili unaojitegemea wa serikali. Kama anashindwa kutetea nafasi yake na kufanya anachoambiwa na Rais hili si tatizo la Rais ni tatizo la Spika mwenyewe. Kama angekuwa ni Spika kutoka upinzani sidhani kama angekubali au angefuata maelekezo ya Rais. Lakini katika demokrasia inapotokea Spika na Rais wote ni wa chama kimoja ni wazi watafanya kazi kwa kuratibu mambo mbalimbali pamoja. Hili hata hivyo si lazima limfanye Spika aonekane mjakazi wa Rais.

Ni vizuri hata hivyo kukumbushana na kuyaweka mambo katika muktadha wake sahihi; Job Ndugai hajaanza leo wala hajaanza baada ya Magufuli kutumia kiti cha Spika ama kuwabania wapinzani, kutishia watu wengine au kukandamiza mijadala. Mifano ipo tu; nitataja michache kukumbushana.

1. Mwaka 2014 Mei 19 akiwa Naibu Spika kwenye mahojiano na Radio One kwenye kipindi cha "Tuongee Asubuhi" Job Ndugai alionesha mgogoro wake na CAG (wakati huo Utoh). Alinukuliwa katika kipindi kile akipinga vikali ushauri wa CAG na kudai kuwa wakati mwingine CAG anachunguza mambo yasiyomhusu na kuwa anatoa ushauri mbovu. Kwa mnaokumbuka CAG alikuwa anashauri mara kwa mara wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za mashirika ya umma. Jambo hili Ndugai alikuwa hapendi (inadaiwa alikuwa ni mjumbe wa bodi kadhaa). Jambo hili hadi leo inaonekana Ndugai halijamtoka. Mgogoro wake na CAG haujaanza na ripoti hii au CAG wa sasa! Ikumbukwe hadi katikati ya mwaka 2015 kulikuwa na Wabunge karibu 45 waliokuwa wajumbe wa bodi mbalimbali za mashirika ya umma.

2. Kuhusu tishio lake la kutuma askari kwenda kumkamata CAG kwa wanaokumbuka hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Ndugai kutumia au kutishia kutumia madaraka hayo. Nadhani mtakumbuka tishio lake juu ya Halima Mdee na Esther Bulaya Juni 7, 2017. Alitishia kuwa kama angetaka angetuma polisi wawakamate wabunge hao wa upinzani na kuletwa Bungeni wakiwa na pingu tena kwa "usafiri wowote". Mwezi mmoja baadaye akiwa msibani mahali fulani Ndugai alinukuliwa kutishia kuwa kama isingekuwa kanuni za Bunge angeweza hata kuruhusu wabunge wakorofi wale wa upande wa pili "kuchapwa viboko hadharani"!

3. Mwaka huo huo 2017 watu inawezekana wamesahau tena ni kuwa Ndugai aliandaa futari na wabunge wa upinzani walisusia futari ile. Ni wakati ule Lissu alimuita Ndugai "Mnafiki" kwa kuwabagua wapinzani. Kwa wanaokumbuka ni kuwa vitendo vya kukandamiza wabunge wa upinzani havikuanza wakati wa Magufuli; hata wakati akiwa Naibu Spika mgogoro mkubwa sana ilikuwa ni jinsi anawatendea upinzani kila akikalia kiti cha Spika kiasi kwamba watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona "Bunge live" ili kuona mgogoro gani Ndugai atakuja nao!

4. Mwaka huo huo - kwa wanaokumbuka - Ndugai alimpiga mkwara wa nguvu Zitto na kumtishia kuwa ana uwezo wa kumfungia kuzungumza Bungeni kwa miaka yote mitano! Ilikuwa ni Septemba 2017 alipotoa kauli hii maarufu "nimwambie Zitto, una uwezo wa kupambana na Spika kweli? Nina uwezo kukupiga marufuku kuongea humo mpaka miaka yako ikaisha, hakuna pakwenda, hakuna cha swali, hakuna cha nyongeza, hakuna cha kuongea chochote humo ndani ya Bunge utanifanya nini. Pambana na kitu kingine na siyo Ndugai". Fikra zake hizo zinaendana na alichokisema miezi mitatu nyuma alipowaambia wale wabunge waliosimamishwa na wakataka kwenda mahakamani na kuwaambia kuwa hakuna cha kesi wala nini yeye ndio Mr. Speaker!

Ningeweza kuendelea kutoa mifano mingine mingi. Kwa ufupi itoshe tu kuonesha tu kuwa tatizo la Ndugai ni la Ndugai. Na watu waendelee kumbebesha lawama yeye kama Mkuu wa Bunge. Kujaribu kumfanya kuwa ni kikaragosi (puppet) wa Rais ni kumfanya awe duni; abebe korokocho lake mwenyewe. Magufuli naye atabeba ya kwake kama Rais.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Wapo baadhi ya watu ambao wanaona kana kwamba Spika Job Ndugai ameanza leo kutumia madaraka yake vibaya na wakati mwingine vibaya zaidi kila akikalia kiti cha Spika. Wengi wanaliona hili hasa kwenye hili sakata la CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali). Ndugai anaonekana kama ni mbabe fulani hivi. Na kwenye sakata la Lissu na hata mambo mengine anavyozungumza wakati mwingine unaamini kabisa kuwa anapokaa kwenye kile kiti cha enzi na joho lake la korosho, zabibu, na mabibo huwa anajisikia nguvu fulani hivi.

Matokeo yake kila anachofanya au asichofanya kinahusishwa na Rais Magufuli. Wapo ambao wanaamini kuwa anapokea na anatendea kazi maagizo toka Ikulu. Inawezekana kuna ukweli lakini Spika wa Tanzania hayuko chini ya Rais na hapaswi kujitendea kama yuko chini (subjected) kwa Rais. Yeye ni mkuu wa Mhimili unaojitegemea wa serikali. Kama anashindwa kutetea nafasi yake na kufanya anachoambiwa na Rais hili si tatizo la Rais ni tatizo la Spika mwenyewe. Kama angekuwa ni Spika kutoka upinzani sidhani kama angekubali au angefuata maelekezo ya Rais. Lakini katika demokrasia inapotokea Spika na Rais wote ni wa chama kimoja ni wazi watafanya kazi kwa kuratibu mambo mbalimbali pamoja. Hili hata hivyo si lazima limfanye Spika aonekane mjakazi wa Rais.

Unahangaika sana kumtetea ngosha mwenzio ila tambua tu! Mmeikosea sana Nchi hii kutuleteq huu mkosi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai ana matatizo. Na Magufuli ana matatizo, tena pengine zaidi ya Ndugai.

Mbona katika uchambuzi wako "umesahau" kuwa Ndugai aliwahi kukiri kuwa humpigia simu Magufuli kuomba ushauri wakati wa teuzi mbalimbali huko bungeni?

Hivi Magufuli angekuwa msafi kama unavyojaribu kutuaminisha angeidhinisha mabilioni yaliyotumika kwa ajili ya matibabu ya Ndugai kwa miezi kadhaa huko India?

Ndugai ana matatizo yake lakini Magufuli ana matatizo makubwa zaidi na hawa wawili wana symbiotic relationship: Magufuli analiendesha bunge kwa rimoti kupitia Ndugai, na Ndugai analipwa fadhila kwa Magufuli kulipa gharama za matibabu yake.

It is high time Mkuu uvue hiyo miwani ya mbao re Magufuli, na ikikupendeza uondoke kwenye campaign mode.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi ni uleule unabadili heading tu. Lengo ni kusafisha jiwe dhidi ya CAG

Unajitahidi sana kumkwepeshwa jiwe katika sakata. Mnajipendekeza mnapata nini au ni mahaba tu baasi. Kujipendekeza kwa kina Makonda ni bora kuliko kwako,maana wale wanapiga hela na fursa
 
Lakini katika demokrasia inapotokea Spika na Rais wote ni wa chama kimoja ni wazi watafanya kazi kwa kuratibu mambo mbalimbali pamoja. Hili hata hivyo si lazima limfanye Spika aonekane mjakazi wa Rais.
Hapa ndipo shida ilipo, Iliwahi kumtokea Marehemu Sitta alipojaribu kusimama kama Spika,Matokeo yake akapigwa chini.Tatizo ni mfumo wa CCM.
 
Mimi niko nje ya Mada kidogo,
Hivi kuna anaefahamu kwanini Hospital Kuu ya Wagonjwa wa Akili ya Mirembe ilijengwa Dodoma?? Alieamua hivyo alizingatia nini hasa??
 
Pamoja na maelekezo ya JPM kwa JOB ila suala la ugonjwa pia ni changamoto kubwa kwa JOB

Na hili la yeye kuitwa mgonjwa huku mitandaoni ndio linamfanya atoe maamuzi ya jazba kama sehemu ya kupunguza machungu yake.
 
Mzee Mwanakijiji Duh! Kwani wewe brother unatumia ugimbi wa aina gani siku hizi?

Mbona haya mambo yako wazi kabisa: Ndugai asingekua anaendelea kuyafanya anayoyafanya kama kweli Rais angekua hakubaliani nayo kwa vitendo. Kumbuka, Magufuli ni Mwenyekiti wa chama pia.

Magufuli ana njia nyingi sana za kisheria za nchi na chama za kumzuia Ndugai asifanye uhalifu; kama ambavyo amewazuia kwa mafanikio makubwa baadhi ya wahalifu nchini kutokutimiza malengo yao ya kihalifu. Sasa, nini kinamshinda Magufuli kufanya hivyo kwa Ndugai? Mbona kama jibu lipo wazi lakini hutaki kulisema?

Hahahahaaaaaaa! Punguza aina ya ugimbi unaotumia Mzee Mwanakijiji. Watanzania wanaofuatilia mambo wanalo jibu siku nyingi sana.
 
Back
Top Bottom