Wadau,
Leo katika kipindi cha tuongee asubuhi cha radio one, Naibu Spika Ndugai amepinga vikali wazo la CAG kwamba wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za masharika ya umma. Ndugai akiongea kwa jazba amesema CAG anaingilia mambo ambayo hayamuhusu na amekuwa akitoa ushauri mbovu ambao hautekelezeki na usio na mashiko, ameendelea kusema kwamba CAG anaingilia kazi zisizomuhusu.
Najiuliza nini kimemfanya Mh Ndugai apandwe na jazba kiasi kile?
Hawa watu ukigusa masilahi yao utaona chamoto!