Ndoto za kuuawa!

me huwa najua kuwa kuna ndoto ambazo mtu huota mara baada ya kuwaza kitu flani kwa muda mrefu, hushuhudia matukio flan kama movies. ndoto zingine huwa kinyume. mf. mwingine huota msiba kumbe kutatokea sherehe. ama mwingine huota sherehe na kukatokea msiba. kuna mdau hapo kasema kuwa mtoa mada ataole ama kupandishwa cheo hayo pia yanawezekana. . .
 
Inategemea, kwa mfano mimi, kila ndoto ninayoota ni lazima itimie. Hebu jaribu kukumbuka kama ndoto unazoota zimeshawahi kutimia. Otherwise utakuwa uliangalia movie ya kikatili ndipo ndoto za namna hiyo zikakuingia.

mkuu mi na movie ni kama mafuta na maji. ngoja nitajitahidi kukumbuka kama huwa ndoto zinatimia
 
yup sometime huwa tunaota kulingana na tuliyoyashuhudia au kuyawaza kabla ya kulala....human brain ni complex machine...

ni kweli kuna ndoto zinazohusiana na tunachokiwaza. lakin katika hali ya kawaida sidhani kama mtu unaweza kumuwazia mama yako/kaka yako kuwa anaweza kukuua. thou nina conflict na boss wangu sijawahi kufikiria kuwa ataniua.
 
tafadhali rejea kitabu cha MHUBIRI 5:3. Inasema "Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi, na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno" sasa yawezeka na ulifanya shughuli nyingi ndo maana ukaota ndoto kama hizo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom