Ndoto ni matokeo ya ubongo kupumzika, hazina maana yeyote zipuuzeni

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,654
9,260
Habari wakuu,

Kama unaota unakimbizwa na majini, unaota mtoto wako wa kumzaa sio wako, unaota upo darasani mnafundishwa na lecturer ilihali ulishamaliza chuo kitambo na upo kazini tayari, unaota ndugu yako kafariki, unaota umekuwa Raisi wa JMT ili hali hujawahi kuwa hata barozi wa nyumba kumi n.k
sleeping-man-dreaming-vector-illustration-57013500.jpg

Puuza hizo ni ndoto tu hazina maana yeyote, usihangaike kutafuta mtu akutafsirie atakujaza ujinga na imani mbovu mbovu,

Mtu anayeamini ktk ndoto hana utofauti na yule anayeamini kuwa dunia ni bapa, hana utofauti na mtu anayeamini kuwa ukiwa vitani ukitamka neno maji risasi zinazopigwa kuelekea kwako zitageuka kuwa maji.

Hii thread itaendeshwa kwa njia/mtindo wa maswali, maana nikisema nianze kueleza kila kitu ni ngumu sana kumaliza kueleza mambo yote maelezo ni mengi sana, ila maswali yataniguide na nitafafanunua kiundani zaidi (deep) kila mtu ataelewa vizuri kabisa.

Nakaribisha maswali.​
 
Ulimwengu unabadirika kila siku, sayansi na teknolojia inakuwa kwa kasi, inatakiwa tuishi ktk usasa sio kuishi ktk maandiko na story za kale za miaka 200 BC, mfalme anamtafuta mtu amtafsirie ndoto, sasa hivi tupo kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

Nashauri kwa wanaotaka kuingia deep waanze na huu uzi kwanza Akili ya binadamu
 
Wakati tunakua kuna kanisa moja la kilokole kulitokea kuwepo na mchungaji mmoja anbaye alisifika sana kwa uponyaji

Sasa ilikua kila jumapili akija kanisani anasema "jana nimeota flani "muumini tajiri" kaninunulia hiki na kweli jamaa ananunua.

Badala ya watu kusanuka mchezo wa pastor wao wakawa wameenda mbali kabisa kumuita nabii mwenye maono kila anachoota kinatokea kweli.
 
Ulishawahi kujiuliza kwanini ukiota unaota matukio mengi mengi yaliyo ktk vipande vipande ambavyo havina uhusiano?

Mfano uote unakula walinyama na rafiki zako hapo hapo unaota unaendesha gali then baadae kidogo unaota umemaliza form six upo JKT mnapigishwa kwata, yaani matukio hayaleti maana.
 
Kuna zile ndoto unaota mko wengi mnakimbizwa, wenzako wote wanakimbia ila wewe tu miguu inakua na ganzi unashindwa kukimbia unaishia kulia huku yule mkimbizaji aki focus kukukimbiza wewe baada ya kuona huwezi kukimbia

Hizi ndoto tulidanganywa sana utotoni kua hapo ni mchawi anakua anakuzuia usikimbie, wengine walijaribu kuiwekea code ndoto kua shetani anazuia maendeleo yako

Kumbe ishu ilikua ni kulala huku umekunja miguu, tangu nijue hivyo sijawahi kupata ndoto ya namna ile.

Kwa hiyo hata hizi ndoto ambazo wengi wanadai kua sijui wametokewa na watu waliokufa ni watu tu hawajazipatia ufumbuzi wa kisababishi chake. Ila hakuna ndoto ya uhalisia
 
Nimefurahi kuona nawewe unauelewa kama wangu mkuu,
Je unajua ni kwanini unapolimbizwa ndotoni huwezi kukimbia wala kukunjua miguu?
Na ukifanikiwa utajikuta unatembea huku ukiwa ndotoni
 
Ndoto Zina maana acha kupotosha watu kabisa..Kuna baadhi ya ndoto zinatokana na harakati za maisha hazina maana yeyote lakini Kuna ndoto mtu unaota vitu vitakavyotokea either reality au kwa mafumbo ..unasema ivo coz hauna Elimu ya ndoto kabisa....vitabu vya dini vyote vinaeleza Mungu anazungumza na watu kupitia ndoto...Mfano halisi ni MIMI MWENYEWE huwa naota vitu vinavyotokea kwa uhalisia au mafumbo na nikitafuta maana inakuwa kweli..Leo uje useme nizakupuuza ..Mambo mengi yanayowapata binadamu mlango mmoja wapo wa taarifa Ni ndoto ...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sijajua nini kinapelekea kushindwa kufanya maamuzi hayo, sometimes unaweza sema akili na mwili vyote vinakua stuck kwenye ndoto na ndio maana inakua ngumu kuchukua action.

Lakini napo nashindwa kuikubali hoja hii kama facts kwasababu kuna muda unaweza ukawa unaota ndoto mbaya halafu kwenye ndoto hiyo ukawa unajibishia mwenyewe kua "hapana hii ni ndoto tu wala sio kweli", sasa kama akili ingekua stucked basi isingewezekana kuwa na awareness inayokujulisha kua upo ndotoni
 
Unajua ni kwanini biblia haijaandikwa ktk mtililiko, pia ukisoma kifungu au mstari mmoja au miwili ile inayofuata haihusiani na mingine inabidi uunganishe na mstari wa kwenye kurasa zingine ili upate maana??? Tueleze sababu??

Je unajua kwanini ukiota unaota kwa vipande vipande ambavyo ukiviunganisha havihusiani wala kuleta maana, tunaomba ujibu?

Je unaelewa nini kuhusu ndoto?

Je unaelewa nini kuhusu probability? Mfano mimi nikiota nimekutana na mzungu halafu kesho yake nikaenda mjini ktk mizunguko nkakutana na mzungu je hapo malaika waliniotesha??? Kwanini mambo yote unayo yaota hayatokei?
 
Habari wakuu,

Kama unaota unakimbizwa na majini, unaota mtoto wako wa kumzaa sio wako, unaota upo darasani mnafundishwa na lecturer ilihali ulishamaliza chuo kitambo na upo kazini tayari, unaota ndugu yako kafariki, unaota umekuwa Raisi wa JMT ili hali hujawahi kuwa hata barozi wa nyumba kumi n.k
View attachment 1912293

Puuza hizo ni ndoto tu hazina maana yeyote, usihangaike kutafuta mtu akutafsirie atakujaza ujinga na imani mbovu mbovu,

Mtu anayeamini ktk ndoto hana utofauti na yule anayeamini kuwa dunia ni bapa, hana utofauti na mtu anayeamini kuwa ukiwa vitani ukitamka neno maji risasi zinazopigwa kuelekea kwako zitageuka kuwa maji.

Hii thread itaendeshwa kwa njia/mtindo wa maswali, maana nikisema nianze kueleza kila kitu ni ngumu sana kumaliza kueleza mambo yote maelezo ni mengi sana, ila maswali yataniguide na nitafafanunua kiundani zaidi (deep) kila mtu ataelewa vizuri kabisa.

Nakaribisha maswali.​
Ndoto ina maana mkuu
 
Ndoto Zina maana acha kupotosha watu kabisa..Kuna baadhi ya ndoto zinatokana na harakati za maisha hazina maana yeyote lakini Kuna ndoto mtu unaota vitu vitakavyotokea either reality au kwa mafumbo ..unasema ivo coz hauna Elimu ya ndoto kabisa....vitabu vya dini vyote vinaeleza Mungu anazungumza na watu kupitia ndoto...Mfano halisi ni MIMI MWENYEWE huwa naota vitu vinavyotokea kwa uhalisia au mafumbo na nikitafuta maana inakuwa kweli..Leo uje useme nizakupuuza ..Mambo mengi yanayowapata binadamu mlango mmoja wapo wa taarifa Ni ndoto ...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ushawahi ota umeokota hela ukiwa ndotoni huko huko ukazishikilia ili ukiamka uamke nazo?

Mkuu ndoto za kweli zipo ila hazijawa based on prediction, au visions kama wengi wanavyo tudanganya, mathalani kama unaota unakojoa basi hiyo ni live streaming ukiamka unaikuta ishakua offline

Kuna siku geto niliishiwa maji ya kunywa, nikalala usiku nikiwa na kiu kikali sana. Nikiwa nimelala nikaota niko porini jua kali kiu kimenibana nikabahatika kuona makazi ya watu ila huwezi amini kila naye muomba maji anani nyima na maji nayaona yalee
 
Sijajua nini kinapelekea kushindwa kufanya maamuzi hayo, sometimes unaweza sema akili na mwili vyote vinakua stuck kwenye ndoto na ndio maana inakua ngumu kuchukua action.

Lakini napo nashindwa kuikubali hoja hii kama facts kwasababu kuna muda unaweza ukawa unaota ndoto mbaya halafu kwenye ndoto hiyo ukawa unajibishia mwenyewe kua "hapana hii ni ndoto tu wala sio kweli", sasa kama akili ingekua stucked basi isingewezekana kuwa na awareness inayokujulisha kua upo ndotoni
Mkuu unafikiria vizuri,

Ipo hivi,
Ubongo unahifadhi kumbu kumbu ktk vipande vipande, hivi vipande vipo kwenye maeneo mbali mbali ya ubongo, na huwa vipo active masaa ishirini na nne, unapopata usingizi ili ubongo upumzike sehemu za ubongo huanza kujizima na kujiwasha kwa zamu, ktk mpangilio usio kuwa maalumu (ndio kuota huko),

Mfano ukiota unalog in JF baadae ukaota unapanda dala dala, baadae ukaota unaangalia mpira maana yake ni kwamba hizo sehemu zenye hizo kumbu kumbu ambazo zipo mbali mbali zilijiwasha wakati ukiwa umelala,

Kisayansi unapokuwa umelala physical activities zote kama vile kutembea, kukimbia huwa zinakuwa switched low(off).

Umenipata mkuu??
 
wale wanaoota huku wanatembea wanaingia kundi gani

Kuna dogo mmoja kijijini tulimuacha ndani amelala si tuko nje tunaota moto tunapiga stori ye akaja akakaa pembeni mguu akauweka kwenye moto halafu anajiongelesha maneno ambayo hayaeleweki. Kesho yake anajikuta ameamka na kidonda mguuni ukimuuliza hana kumbukumbu yeyote kua jana alikua anaota huku anatembea (sleepwalking)
 
Ushawahi ota umeokota hela ukiwa ndotoni huko huko ukazishikilia ili ukiamka uamke nazo?

Mkuu ndoto za kweli zipo ila hazijawa based on prediction, au visions kama wengi wanavyo tudanganya, mathalani kama unaota unakojoa basi hiyo ni live streaming ukiamka unaikuta ishakua offline

Kuna siku geto niliishiwa maji ya kunywa, nikalala usiku nikiwa na kiu kikali sana. Nikiwa nimelala nikaota niko porini jua kali kiu kimenibana nikabahatika kuona makazi ya watu ila huwezi amini kila naye muomba maji anani nyima na maji nayaona yalee
Ukielewa utofauti kati ya kuzimia na kusinzia utapata jibu la kilichotokea,

Kwa lugha nyepesi Ndoto ni thinking in a state of sleeping, na kikawaida thinking is a recall of memmory.

Lakini kuzimia ni ubongo unakuwa umejizima wote kwa muda na ukiamka hutakumbuka chochote
 
mimi nimechallenge pale uliposema mtu akilala physical activities kama kutembea zinakua off
 
Ukipozingua ni hiyo story ya majimaji acha ujinga huo unaamini story za wazungu kuwa wazee wetu walisema maji
 
wale wanaoota huku wanatembea wanaingia kundi gani

Kuna dogo mmoja kijijini tulimuacha ndani amelala si tuko nje tunaota moto tunapiga stori ye akaja akakaa pembeni mguu akauweka kwenye moto halafu anajiongelesha maneno ambayo hayaeleweki. Kesho yake anajikuta ameamka na kidonda mguuni ukimuuliza hana kumbukumbu yeyote kua jana alikua anaota huku anatembea (sleepwalking)
Mkuu hii hutokea mara chache sana kuna sakati upande wa ubongo unaohusika na kutembea ukijiwasha ukiwa usingizini wkati huo huo sehemu zingine zikijiwasha na kuzima utajikuta unatembea kama huyo dogo,

Kuna wengine huwa wanaota wanafanya malenzi (means kumbu kumbu ya ufanyaji mapenzi imejiwasha) na kufika kileleni kabisa yaani wanapiga bao.
 
Back
Top Bottom