Good Guy
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 3,822
- 1,434
Me niliota naolewa na JK , katika kutoa kiapo nikaganda kdgo ndoto ikaisha.
dah una bahati xana mi nikiota ndoto na hawa jamaa wamo hawa kina Rostam mizizi nawaalibia humo humo,hamna kuremba.
Me niliota naolewa na JK , katika kutoa kiapo nikaganda kdgo ndoto ikaisha.
Mimi niliota nakimbizwa na shangazi na yeye alikuwa na uwezo wa kunikamata tu endapo nitapita kwenye kivuli iwe ni chini ya mti au kivuli chochote, basi nilikuwa nakwepa vivuli kama nini, nikiona kivuli tu nakula kona na kurudi juani.
Hapa unatoa upenyo watu watudandanye na ndoto zao, binafsi bwana yaani naota ndoto vizuri ila nikifumbua macho tu najikuta nishasahau...
Ila kunakitu kinaniboa sana kwenye ndoto zingine nakumbuka ndoto moja niliota nataka kugongwa na gari barabarani sasa kila nikijaribu kukimbia yaani siwezi nabaki tu kwa barabara... yaani siku ile nilikasirika sana, nikamuuliza jamaa angu akaniambia eti ili uweze kukimbia kwenye ndoto ni lazima uwe umelala kiubavu ili uweze kui-roll miguu.
Ndoto zangu tamu nyingi huwa haziishi basi inabidi niwe nazimalizia mwenyewe ile asubuhi wakati usingizi ushakata ila inakuwa ishakata utamu.
Hivi kuna mahusiano ya ndoto na matukio halisi, sometime kama nimelala unakuta matukio yanayotokea wakati huo kwa watu ambao hawajalala unayaota kwenye ndoto, labda upo rum we umelala na washkaji hawajalala basi unawasikia kwenye ndoto kama kuna stori wanapiga.
Lol.... ndotoooo
Nakumbuka siku moja niliota kwamba kwasababu Waislam wanalalamikia sana kwamba nchi inaendeshwa na mfumo kristu na wanabanwa sana katika nafasi za uongozi na matokeo ya mitihani, serikali imepitisha rasmi sheria ambayo inafuta viti maalumu kwa walemavu ila imeanzisha viti maalumu kwa ajili ya waislam na imezindua silabasi Rais sana kwa ajiri yao kwa ajili ya ku-boost matokeo, niliposhtuka nilijisikia vibaya sana, maana hii ndoto sikuipenda kabisa
Sitasahau siku naota niko mbinguni na kupaona plivyo pazuri, nikawa nachekelea kimoyomoyo cha ajabu ndoto ilipokata nikajikuta nipo kitandani nilichukia sana. Lakini nakazana kumpokea Yesu ndani yangu kila siku ili hatimae siku moja nifike huko mbinguni pasipo ndoto.
me niliwah kuota nimekutana na wale watoto wa mitaan bas wakanivamia kutaka kunipiga. nikaanza kupambana nao, nliwakatakata kwa mapanga wote mpk wakafa. nilipoamka nlichukia sana hyo ndoto.
wajameni ndoto niliyoota miaka 15 iliyopita siwezi kuisahau tena,niliota napaa angani halafu natua chini kama helicopter halafu watu wengi sana wanakuja kuangalia tukio,halafu nikapaa tena na kuondoka kuacha watu midomo wazi wakishangaa,kama kuna mtu anaweza kunisaidia maana ya hii ndoto
Naomba msinicheke wadau, ndoto nisiyoisahau ni kama mwaka unusu nyuma, that day bwana niliota naliwa kisamvu cha kopo, kila nikikukuruka niamke wapii, mwisho nikashtuka, kilichoninyima raha kwa siku kadhaa mbele ni kuamka ilhali jicho la tatu linauma, jumlisha na ndoto yenyewe basi nilikosa amani mpaka basi. Mweh!
dah, nahisi ulifauduCode: