Ndondocha na utajiri

Ndondocha na utajiri

Me nazijua, ni pm, Nina kitabu flani kinaitwa Myths and Legends of the Bantu, ni cha urithi toka kwa padre wa kwanza wa kiafrika jimbo la Mtwara, ila kiliandikwa na wamisionari wa kizungu kwa tafiti zao. Kipo wazi kwa mambo mengi hasa hili la ndondocha. Huwezi kupata kokote kitabu hicho kwani hata teknolojia yao ya maandishi yanaonesha hawakuwa na soft copy.
***
Ramea/
ningependa sana kukisoma kwa kujifunza tu.na kuelewa!
 
Kuna jamaa mmoja anafahamika kwa jina la BAYA almaarufu BATCO ni Mkurya wa Tarime lakini ameishi mjini Magu kwa miaka mingi sana, mwanzoni maisha yake yalikuwa si mazuri hata kidogo.

Miaka imeenda mara huyu jamaa akawa anamiliki mabasi na mpaka sasa mabasi yake yanipiga route kati ya Mwanza na Tarime, lakini mwaka juzi (2014) tulimzika mkewe baada ya kuugua ukichaa kwa mda mrefu jamaa akaoa mke mwingine na akahamia Mwanza mjini. Kwa taarifa nilizonazo hata kijana wake mkubwa ni kichaa na amepata ukichaa baada ya mama yake kufariki, njoo stendi ya Magu utamwona.

Hadi sasa juzi jamaa ameongeza tena mabasi mengine matatu, ila inaonekana jamaa anawafanya watoto wake wawe madondocha ili azidi kupata mali nyingi.
 
Hapa umenijibu Mshana Jr swali ambalo nililokuwa najiuliza, tofauti ya ndondocha na msukule. Ila mkuu Kama unaweza fafanua zaidi tafadhari, Mshana Jr.
Ndondocha huwekwa tu ndani na kutunzwa na mmiliki wake hupata utajiri(hapa kuna mengi yanahusika) wakati msukule kwanza hawekwi ndani bali ni kama mtumwa na hutumikishwa kishirikina kama mpagazi na maksai mashambani na kazi nyinginezo ngumu
Ndondocha hakatwi ulimi na hupewa chakula kizuri wakati msukule hupewa vyakula vya hovyo kabisa hasa unga wa mahindi na maji tuu
Ndondocha hupumbazwa tu na madawa huku msukule inabidi kuuliwa kishirikina kwanza ndio aweze kuchukuliwa usukule
Ndondocha huvishwa nguo na anaweza kuonekana na watu wakati msukule huishi mbali na watu na havalishwi nguo na ni nadra na vigumu mno kumuona kutokana na madawa aliyopakwa
 
Adui wa mtu ni wa karibu sana; ingawa watu wengi huwa wana usema huu msemo ila hawachukulii maanani. Mtu wa karibu anaweza kukufanyia chochote ili yeye afaidike; na anaweza akawa mwema kwako na hata ucweze mfikiria kama anaweza kukutendea kitendo kibaya. Mungu atupatie macho ya rohoni; na Mungu hawez kukupa macho ya rohoni kama ukiwa na chuki au kutomsamehe huyo mtu na kumuacha Mungu alipize kisas kwa ajili yako. Hata hao wanao watoa wenzao ni watu wa karibu kabisaa
 
Kuna jamaa mmoja anafahamika kwa jina la BAY almaarufu BATCO ni Mkurya wa Tarime lakini ameishi mjini Magu kwa miaka mingi sana, mwanzoni maisha yake yalikuwa si mazuri hata kidogo.

Miaka imeenda mara huyu jamaa akawa anamiliki mabasi na mpaka sasa mabasi yake yanipiga route kati ya Mwanza na Tarime, lakini mwaka juzi (2014) tulimzika mkewe baada ya kuugua ukichaa kwa mda mrefu jamaa akaoa mke mwingine na akahamia Mwanza mjini. Kwa taarifa nilizonazo hata kijana wake mkubwa ni kichaa na amepata ukichaa baada ya mama yake kufariki, njoo stendi ya Magu utamwona.

Hadi sasa juzi jamaa ameongeza tena mabasi mengine matatu, ila inaonekana jamaa anawafanya watoto wake wawe madondocha ili azidi kupata mali nyingi.
Amebahatika kipindi hiki kafanya timing nzuri, ila akifa huyo mtoto jamaa ajiandae kufilisika au yeye kuwa ndondocha halafu utajiri wafaidi ndugu
 
Adui wa mtu ni wa karibu sana; ingawa watu wengi huwa wana usema huu msemo ila hawachukulii maanani. Mtu wa karibu anaweza kukufanyia chochote ili yeye afaidike; na anaweza akawa mwema kwako na hata ucweze mfikiria kama anaweza kukutendea kitendo kibaya. Mungu atupatie macho ya rohoni; na Mungu hawez kukupa macho ya rohoni kama ukiwa na chuki au kutomsamehe huyo mtu na kumuacha Mungu alipize kisas kwa ajili yako. Hata hao wanao watoa wenzao ni watu wa karibu kabisaa
DIVINE kumbuka usemi maarufu wa Kikulacho....!!!
 
Ndondocha huwekwa tu ndani na kutunzwa na mmiliki wake hupata utajiri(hapa kuna mengi yanahusika) wakati msukule kwanza hawekwi ndani bali ni kama mtumwa na hutumikishwa kishirikina kama mpagazi na maksai mashambani na kazi nyinginezo ngumu
Ndondocha hakatwi ulimi na hupewa chakula kizuri wakati msukule hupewa vyakula vya hovyo kabisa hasa unga wa mahindi na maji tuu
Ndondocha hupumbazwa tu na madawa huku msukule inabidi kuuliwa kishirikina kwanza ndio aweze kuchukuliwa usukule
Ndondocha huvishwa nguo na anaweza kuonekana na watu wakati msukule huishi mbali na watu na havalishwi nguo na ni nadra na vigumu mno kumuona kutokana na madawa aliyopakwa
Mkuu nini faida zao kwa kwa kuzingatia tofauti zao hizo, kumbe ndondocha tunaonana nao kila siku ila nilikuwa siwajui ingawa sio kila chizi Ni ndondocha. Mmoja aliniomba sh. Mia mbili pale mlimani city kituo cha basi za kwenda mwenge nikamnyima, au sijui Ni tena yule ila yule Ni zoba Fulani hivi.
 
Ndondocha halisi hatembei barabarani bali hutunzwa nyumbani au dukani wale ambao unawaona barabarani wengine wamechizishwa kwa makusudi hayo hayo ya mtu kupata utajiri
 
Dah Kuna Mzee wangu mmoja wa kipare, alikua anatuambia unamuona huyu tajili magari yake, na yameandikwa maneno ya Mungu, mwanawe kamtoa msukule anatoka maudenda tu. Juzi juzi tena nimeonywesha mama mmoja pale mbezi Luis, eneo wanaliita kitopeni mama Hana uwezo mzuri wa akili, kwakua simju nilimwamkia hakuitikia. Mwenyeji wangu baada akaniambia huyo mama ni msukule(ndondocha kwa majibu wa Mshana Jr) na kafanywa hivo na mumewe nilionyesha pia walikua duka moja pale mume anapata bia.
 
Kuna mengine ni kupakaziana tuu lakini unajiuliza inakuwaje mtu anakaa na mgonjwa wa akili ndani ya nyumba na hata siku moja hajaribu kumpeleka kwenye tiba wakati uwezo anao?
 
Ndondocha halisi hatembei barabarani bali hutunzwa nyumbani au dukani wale ambao unawaona barabarani wengine wamechizishwa kwa makusudi hayo hayo ya mtu kupata utajiri
Hata hivo nilikataa kumpa hela si kwa kujua au kuhisi undondocha wake, bali somo lako ka uchawi wa kulogoshea pesa, Mimi limeniingia Sana. Maana unaweza ona mtu Ana mzuri apita njiani au barabarani na vijiweni akiomba asaidiwe Mia mbili. Ukijiuliza Mia mbili inamsaidiaje kwanini asiseme hitaji lake, alafu Mimi nione uwezo wangu wa kumsaidia.
 
9227030c8fa6ec578697b23b723374a2.jpg

Kwanza niseme wazi kabisa kwamba hili nimeshindwa kulipatia majibu ya kutosha hata baada ya kujipa muda wa kutosha kulitafit.

Binafsi nilishawahi kumuona walau ndondocha mmoja mwenye asili ya kiasia pale buguruni kwa tajiri mmoja wa magari ya kusafirisha mizigo..huyo ndondocha alikuwa mama mzazi wa huyo tajiri na alikuwa kawekewa wafanyakazi wawili wa kumwangalia kwa kila kitu...alikuwa anafungiwa chumbani muda wote na alikuja kufariki mwaka 2004 na jamaa kufilisika kabisa mwaka 2005.

Hizi habari za ndondocha zinahusishwa pia na wakinga na watani zangu wachaga japo kwa kiasi kidogo na wabondei na makabila mengine kwa uchache.
Nimeshindwa kupata jibu la hakika inakuwaje kumfanya mtu ndondocha kisha wewe upate utajiri...!!!yani mwingine ateseke aishi kifungoni huku wewe kupitia yeye uishi maisha ya ufahari sifa mafanikio heshima na umaarufu???

Utajiri wa ndondocha hauna tofauti na utajiri wa kuua lazima uishi kwenye maagano na viapo na masharti mengi..! Unapenda utajiri sawa unapenda mafanikio sahihi kabisa..! Lakini angalia unapata utajiri wa aina gani ili mwisho wa siku tusikuone unafilisika ghafla na kuwa na mikosi kibao.

Utajiri wa ndondocha unatesa wengi sana kwakuwa huyu akifa inabidi fasta uandae mwingine wa ku take cover na kumbuka wote lazima wawe ndugu wa karibu
Mkuu umenigusa sana katika huu uzi. Hili jambo lina ukweli kabisa na takupa mfano hai hata kama kuna watu watafahamu hii sehemu. Katika kijiji cha Kagunga kabla ya kufika Ngoma Sengerema ukivuka Busolwa katika wilaya ya Sengerema ilikuwepo familia maarufu sana ya Hindia Nyanda ambayo walikuwa na ngo'mbe wengi wengi balaa. Kabla ya hapo huyu mzee Hindia Nyanda alikuwa malenga wa ngoma za jadi baadae akaokoka lkn tayari akiwa ashamfanya ndondocha binti yake ambaye alikuwa akishinda nyuma ya nyumba. Nilifika hapo kama mara tatu,siku ya kwanza nikiwa na rafiki yangu (mtoto wa huyo mzee Hindia) nilimuona huyo binti lakini akiwa amevaa nguo mpya na bei mbaya kwa kipindi hicho hata mama yangu sijawahi kuona ametupia japokuwa baba alikuwa mwalimu enzi hizo. Nilipomsalimia nikiamini yuko kamili mwenyeji wangu alinishika mkono kuashiria twende zetu kwa vile hakunijibu. Safari ya pili nyingine nilimkuta akiwa katupia pamba zingine balaa na sikumpa hi kama mwanzo. Baadae nilipata nafasi ya kukuuliza mwenyeji na akanipa stori kamili akiniiambia kuwa: huyo binti ndiye kila kitu kuhusu hao ng'ombe na hutolewa asubuhi kila siku akiwa kapiga hizo pamba kabla ng'ombe hawajaenda malishoni na ni lazima ashuhudie hao ng'ombe wakienda malishoni. Tangia siku hiyo mimi ndo ikawa basi tena kufika hapo. NB: kama kuna mtu wa Sengerema katika kijiji hiki aje akanushe. Mimi nilifika hapo miaka ya 199.......
 
Hata hivo nilikataa kumpa hela si kwa kujua au kuhisi undondocha wake, bali somo lako ka uchawi wa kulogoshea pesa, Mimi limeniingia Sana. Maana unaweza ona mtu Ana mzuri apita njiani au barabarani na vijiweni akiomba asaidiwe Mia mbili. Ukijiuliza Mia mbili inamsaidiaje kwanini asiseme hitaji lake, alafu Mimi nione uwezo wangu wa kumsaidia.
Zamani nilikua nawaonea huruma na kuwapa hela ila kuna siku mchawi mkubwa aliokoka na kutoa ushuhuda jinsi watu wanavoingizwa kwenye maagano na kuzimu mikosi kisa kujifanya una huruma. Wengi waweza waona walemavu kumbe ni wazima wameenda kuvaa mavazi ya ukichaa na ulemavu. Kumpa hela omba omba ni hatari sana
 
Kumbe!!!!! Mbona kama hivyo watakuwa washaondoka na nyota yangu jamani!!!
 
Back
Top Bottom