Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,848
- 730,370
Kwanza niseme wazi kabisa kwamba hili nimeshindwa kulipatia majibu ya kutosha hata baada ya kujipa muda wa kutosha kulitafit.
Binafsi nilishawahi kumuona walau ndondocha mmoja mwenye asili ya kiasia pale buguruni kwa tajiri mmoja wa magari ya kusafirisha mizigo..huyo ndondocha alikuwa mama mzazi wa huyo tajiri na alikuwa kawekewa wafanyakazi wawili wa kumwangalia kwa kila kitu...alikuwa anafungiwa chumbani muda wote na alikuja kufariki mwaka 2004 na jamaa kufilisika kabisa mwaka 2005.
Hizi habari za ndondocha zinahusishwa pia na wakinga na watani zangu wachaga japo kwa kiasi kidogo na wabondei na makabila mengine kwa uchache.
Nimeshindwa kupata jibu la hakika inakuwaje kumfanya mtu ndondocha kisha wewe upate utajiri...!!!yani mwingine ateseke aishi kifungoni huku wewe kupitia yeye uishi maisha ya ufahari sifa mafanikio heshima na umaarufu???
Utajiri wa ndondocha hauna tofauti na utajiri wa kuua lazima uishi kwenye maagano na viapo na masharti mengi..! Unapenda utajiri sawa unapenda mafanikio sahihi kabisa..! Lakini angalia unapata utajiri wa aina gani ili mwisho wa siku tusikuone unafilisika ghafla na kuwa na mikosi kibao.
Utajiri wa ndondocha unatesa wengi sana kwakuwa huyu akifa inabidi fasta uandae mwingine wa ku take cover na kumbuka wote lazima wawe ndugu wa karibu