Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 31,010
- 60,472
Happy FURAHI DAY people.
Leo naungama kwamba mimi ni cheater, tena mzoefu.
Hehehe joking bana, kama nawaona vile wana infi wakikaa sawa kuunga hoja na wale wengine wakitayarisha mawe. . Lolz
Joking aside, kuna watu ambao ni cheaters wa kudumu. Kama sio wewe pengine mwenzi wako, ndugu yako, rafiki yako, work/class mate, jirani n.k Kwa ufupi ni kwamba kila anamjua mtu ambae amebobea kwenye hiyo sekta na wengi wao hawana hata mpango wa kuacha.
Ukiachilia mbali swala la kudanganya na kuumiza hisia za mke/mume/mpenzi ambalo limeshazoeleka na kukubalika hata na "victims" wenyewe, watu huwa wanafikiria kweli madhara yanayoweza kupatikana kwasababu tu ya tamaa/kutokuridhika kwao?
Magonjwa. .
. .Kuna dada alibeba mimba yake, akajifungua katoto kake wote wakiwa salama kabisa. Ila alivyoenda kupima miezi nane baadae akakutwa ameathirika na mwanae pia. Hiyo ni zawadi ya baba kwa mama na mtoto.
. .Idadi ya wanaoathirika pasi wao kujua kwasababu ya wenzi wao sio ndogo. Ndio maana kuna watu wakisikia swala la kupima tu presha inapanda hata kama hajatoka nje ya mahusiano yake.
. .Baadhi ya watu hupata magonjwa ya moyo kutokana na usaliti huu huu.
Kifo. .
Tunasikia kila wakati mume kaua mke/mpenzi wake, mke kaua mume/mpenziwake kwasababu hakuwa muaminifu. Mara mwanaume kaua anaetoka na mke wake n.k
Kwenye kesi nyingine hata kimada anaweza akafikia hatua ya kuua mwanaume anaetoka nae ama mwanamke wa huyo mwanaume.
Kujeruhiwa. .
Kutokana na fumanizi wako wanaobaki na viungo pungufu tofauti na alivyokuwa navyo awali. Wapo wanaume waliokatwa vitendea kazi vyao, wapo wanaopoteza mguu, mkono au hata jicho na majeraha mengine mengi tu.
Hadhi na uhuru. .
Unajishushia wewe hadhi pamoja na mke/mume hata familia yako. Wapo watu wanakosa hata raha ya kuishi/kwenda mahali fulani kwasababu ya kusalitiwa. Mke au mume anaona ugumu hata wa kutembea mtaani kwasababu ya mwenzi wake. Mtoto anakosa hata raha shuleni na mtaani sababu ya makosa ya mzazi wake.
Kujiamini. .
Ndio sio sahihi mtu kukosa kujiamini kwasababu ya kosa la mtu mwingine ila watu wengi hushindwa kujizuia na kuchukulia tabia za wenzi wao kuwa ni udhaifu wao. Hili hupelekea baadhi ya watu kupata msongo wa mawazo ama kuishi maisha ya unyonge wakati wote. Unyonge husababisha kukata tamaa ya maisha.
Madhara mengineyo. .
(. .hapa tusiulizane imani jamani. . )
Mitaani wanawake wanaloga wanaotoka na watu wao, wanaume wanakodisha wahuni wa kuwafunza adabu wanaotoka na wake zao.
Nyumba ndogo inaloga mwanaume ikibidi mke au hata watoto wa mwanaume and so on.
Watoto. .
Kweli watoto ni baraka ila mara nyingi watoto wanaopatikana kwenye usaliti huwa hawachukuliwi kama baraka. Mama yake mwenyewe anaweza akakutupia wewe, mkeo/mumeo akamkataa na akaishia kunyanyasika.
Yani maumivu yanaweza kusababishwa na yeyote yule KWA yeyote yule.
Maoni yangu. .
Fanya "risk analysis" kabla ya kutoka nje ya mahusiano yako ama kutoka na mtu mwenye mahusiano yake (mke/mume/mpenzi wa mtu). Wewe kama mume/mke/mpenzi wa fulani unadhani hiyo tamaa yako ina thamani sawa na afya/maisha ya mwenzi wako ama watoto wako? Je ina thamani sawa na maisha yako wewe? Au labda ina thamani sawa na mguu/mkono/jicho lako?Huyo mwanamke/mwanaume ni worth kisu tumboni mwake au mwako? We mwanaume uko tayari kugeuzwa mwanamke? Je mdada kubakwa na kundi la vijana kwaajili ya mume/mpenzi wa mtu mwingine?
Ukweli ni kwamba hamna anaejua kiwango cha wehu/kuchaganyikiwa anachoweza kufikia mtu mwingine mpaka pale inapobonyezwa ile swichi inayoendesha hisia zake kwa hali ya juu kabisa. Sio huyo unaetembea nae nje wala uliye nae ndani. Wa nje anaweza akamdhuru wa ndani, wa ndani akamdhuru wa nje na wote wanaweza wakakudhuru wewe.
Watu tupunguze ubinafsi, tujifunze kuridhika na tujifunze kujali watu wengine. Inawezekana kweli "cha wizi ni kitamu" ila utamu huo wa muda mfupi unaweza kusababisha matatizo ya kudumu. Ila ukiona mke/mume wa mtu, nyumba ndogo/kidumu chako is worth the risk basi tena sina la zaidi. Have your fun mpaka pale itakapositishwa kwa lazima.