Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,177
- 34,444
- Thread starter
- #201
SEHEMU YA 31
"One, hakika nakupenda sana na nilikuamini kila ulichonambia katika maisha yako. Nilikusikiliza na wala sikuwahi kukuhisi vibaya. Hakika ulipendeza machoni mpaka moyoni mwangu kila nilipofumba mboni zangu niliiona taswira yako. Sikuwahi kutegemea wala kuwaza kama nitakuja kuingia katika mkosi wa mapenzi tena katika wakati muhimu zaidi. Wakati wa kuunganishwa kuwa mwili mmoja. Hakika umeniumiza na kunitia aibu kuu mimi na wazazi wangu. Sijajua kwanini uliamua kudanganya lakini sitaki kukuhukumu kwa hilo. Ua hili nililokuletea ni ishara ya upendo wangu wa dhati kwako lakini sina uhitaji wowote tena. Nakusihi uishi na mkeo. Kwanza ni mzuri sana mwenye kuvutia pia ni msomi. Wazazi wangu wamekusamehe na hata mimi sina kinyongo zaidi nimekuja kukuaga zimebaki siku chache nasafiri kuelekea London kwa mapumziko ya muda na sidhani kama tutaonana tena One. Sitamani wala siwezi kuvumilia maumivu haya hapa nyumbani. Naelekea kwa mjomba London One baki na mkeo na usije thubutu kufanya kinyume kama ulivyotaka kufanya kwangu. Kumbuka ni dhambi hata Mungu hapendi. Kwaheri One huna haja ya kunihadithia chochote nishayasikia yote ya nyuma kwenye maisha yako. Hakika mkeo Atuganile bado anakupenda sana nakusihi umpende na umuheshimu. Ahsante!"
Hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno kati ya mengi aliyoongea Rose siku hiyo na kunifanya midomo inicheze na kuzungumza kwa hisia na uchungu.
"Ro...Ro...Rose tafadhali aaah! Rose hujui kitu. Mimm...." Kabla hata sijamalizia kusudi langu la kusema mara niliwashuhudia wazazi wa Rose nao wakiingia wakiwa sambamba na baba mchungaji. Ilibidi nimung'unye tu maneno na kujikaza.
Rose alinitazama kwa na kuniaga kwa ishara ya macho huku akiwapisha wazazi wake ambao niliwaonea aibu na kujisikia viabaya moyoni. Ingawa wao walionesha utu na kunifariji lakini niliona ndio kwanza utu wanaonionesha unazidi kuniumiza na kunidhihirishia dhambi zangu kwao. Mchungaji alifanya maombi na kuniombea pale huku wakimshukuru Mungu kwa kuzidi ifanya afya yangu kutengemaa.
"Onesmo mwanangu. Hupaswi kuumia kichwa kufikiria yaliyopita. Najua na nina hakika lengo lako halikuwa baya nafsini mwako kutokana na ukomo wa fikra tu. Mimi nimekusamehe pia nakupa pole kwa gharama zote zilizoenda bure pasipo kutimia jambo kusudiwa. Tumefanya mawasiliano na mkeo zaidi ya mara tatu na tumejaribu kuzungumza na uongozi wa kanisa Iringa wamewaita na wamezungumza nao na nina hakika sasa atarudi kuwa mke mpya bora na mzuri katika maisha yote ya hapa suniani. Hakuna kitu cha kuwatenganisha zaidi ya kifo tu. Nitaporudi London baada ya kumpeleka Rose akatulize kichwa chake. Nitakutimizia nusu ya yale yote niliyoyakusudia kukupa pindi utapomuoa binti yangu ili maisha yenu yaendelee kuwa katika mstari mzuri. Najua kwa hali uliyo nayo hupaswi kuumiza sana kichwa kufikiria vipi maisha utakabiliana nayo. Tuliza tu kichwa One wewe bado utaendelea kuwa mwanangu. Bwana ameipa mamlaka sauti yako usiache kumuimbia na kumsifu. Ugua pole mwanangu uponywe kwa damu ya yesu katika jina la baba, la mwana na la roho mtakatifu. Ameen."
Aliongea baba Rose maneno yaliyonitoa machozi nikishindwa jua nimshukuru vipi. Nilishindwa kabisa nimuweke kwenye kundi la wema kiasi gani baba yule. Daaah! hakika nilijiona mwenye bahati niliyevikwa joho la mikosi. Baba Rose alisema nami pasipo kuonesha kinyongo wala maono mabaya dhidi yangu.
*******
Saa zilikatika na siku tatu mbele zikapita nikizidi kuwa mzima na hatimaye nikaruhusiwa hospitalini. Kila siku mtu mwengine ambaye hakukauka hospitali alikuwa ni Sulu. Alinifariji sana kwa kweli zaidi ya sana. Hata siku naruhusiwa yeye ndiye aliiendesha gari yangu ambayo nilipewa na baba Rose. Tukiwa sambamba na dada zangu tulifika nyumbani kule nilipokuwa naishi. Watu wengi walionijua na wale waliopata mkasa wangu hawakukauka kunipigia simu na kuja nijulia hali. Ingawa nilidhoofika kimwili kwa kupungua mpaka uzito wangu wa kawaida lakinikupona kwangu wengi hawakuamini kwa vile wapo ambao walishazusha kuwa nilifariki kule hospitali. Wengi walishazoea kuwa wakisikia mtu amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi basi imani zao huwapelekea kuwa huyo ni mtu wa kufa tu. Si hivyo! walisahau kuwa kuugua si kufa. Nilipona japo furaha ilienda likizo. Muda wote nilikuwa mkimya nikiwa sina hata hamu ya kwenda kuliona kaburi la mamaangu. Wala hakuna mtu aliyenigusia msiba wa mama kwa haraka hata niliporuhusiwa hospitali na kuwa nyumbani. Dada zangu walinifariji kwa maneno ya hekima na kutia nguvu huku Sulu akiendelea kunisisitizia kuchangamka kama ilivyokuwa kawaida yangu. Ucheshi wote uliniisha. Sikuwa mtu wa maneno ya utani wala mchangamfu tena. Muda wote nilikuwa mkimya kama kobe. Moyo wangu pekee ndio ulikuwa unanijua nini nafikiria na vipi najisikia.
"Lazima nilipe kisasi! hapana! Atuganile sikuachi wewe na mamaako mtaiipa roho ya mamaangu kwa roho nzenu." Nilisema na akili zangu huku mawazo yakinituma kufunga safari ya Kyela kwenda kulipa kisasi hata kwa kuwachomea moto ndani kina Atuganile. Hakuna cha zaidi nilichofikiria zaidi ya hiko.
Usiku wa siku niliyoruhusiwa hospitalini ndiyo siku ambayo baba Rose alikuwa anampeleka bintiye London kwa mjombaake. Walisindikizwa hadi uwanja wa ndege salama.
Sikuwa najua kama siku hiyo ndiyo walisafiri hadi pale majira ya saa kumi jioni niliposikia sauti ya dadaangu mmoja akija akilia huku ameshika mikono kichwani.
"Dada vipi?" Niliuliza kwa mshtuko wakati huo nilikuwa nimekaa sebuleni na Sulu tukitazama mkanda wa video.
Dadaangu yule ambaye alikuwa mwanakwaya pia aliendelea kulia pasipo kunyamaza hata alipokuwa anabembelezwa na wenzake.
"Dada Angel kwani vipi? mbona Sara analia sana?" Aliuliza Sulu ambae alikuwa anaijua familia yetu yote vizuri tu nao walikuwa wanamtambua vyema.
"Alikuwa ametoka kuelekea kanisani kwenye mazoezi ya kwaya muda si mingi. Sasa ndio amerudi saa hizi akilia hata sisi anatutisha kwanini hasemi kimlizacho."
Alijibu dadaaangu yule mwengine. Moyo wangu uliripuka muda huo na kuhisi naikosa amani. Nilichukua simu yangu iliyokuwa pembeni lakini kabla sijafanya chochote ziliingia meseji tatu kwa mpigo kutoka kwa watu tofauti.
Moja ilisema.
'ROSE MASIKINI..'
Nyengine ikaandikwa.
'HIVI NI KWELI KAKA HIKI TUKIONACHO BECKER TV DAAAH SIAMINI'
Nilistushwa zaidi na kujikuta naisoma nyengine ambayo nayo ilisomeka
'POLE SANA ONE KWA MITIHANI MIZITO. R.I.P ROSE'
hii sasa ndiyo ilinichanganya kila kitu wakati huo na kukurupuka kuwasha king'amuzi huku nikibadili chaneli haraka na kuiweka Becker TV pasipo kumwambia chochte Sulu aliyebaki akinishangaa.
Machozi tayari yalianza kunitoka huku nikiwa naikodolea macho tv kuona habari gani hiyo. Dada aliyekuwa analia wakati huo naye alijitahidi kutuliza mzka na kuanza wahadithia kwa kwikwi na shida wenzake kilichokuwa kimemfanya alie vile.
Laaaaa haulaa! ama kweli ng'ombe wa masikini hazai na wa moja havai mbili. Taarifa ya habari iliyokuwa inatangazwa Becker TV wakati ule ilimstua kila mtu hata Sulu alijikuta anashika mikono kichwa.
"....................ndege hiyo pekee kutoka shirika la ndege Tanzania iliyokuwa inafanya safari kuelekea London ilikuwa na abiria takribani 35, marubani 3 na wahudumu 6 na wote wanaripotiwa kufariki katika mlipuko huo unaosemekana umesababishwa na kikundi cha kigaidi waliodhani ni ndege ya kijeshi iliyokuwa inakatiza kwenye anga yao. Mungu azilaze roho za marehemu wote peponi. Becker TV tunatoa pole kwa wanafamilia wote na watanzania kwa ujumla."
Habari ilikuwa inaishia lakini tayari ilitosha kutuzibua macho na masikio kwa kilichotokea ambacho sikutaka kukiamini kabisaaa.
"Ndiooo! ndege waliyosafiri nayo ndiyo iliyolipuliwa jamani wifiii yangu Roseeee"
sauti ya dada mkubwa nayo niliisikia ikilia kwa uchungu na hapo ndipo simu yangu ilipozidi kuita na kuingia meseji za watu tofautitofauti na kunivuruga.
Ooooh! yaani Rose ndio awe ametutoka hivi hivi? Aaaaah! sikutaka kuamini hata nilipompigia simu baba mchungaji ambae naye alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo mbaya ambapo ndege iliripuliwa na kubaki majivu. Hakuna kilichotoka ndani yake. Magaidi waliua watu wasio na hatia. Rose na babaye walisafiri kwa ndege ile iliyogeuka kuwa kaburi lao.
"Roseee! hapana Roseee oooh Rose wanguuuuu?"
Nilianza kulia taratibu huku Sulu naye akinifariji kwa kunizuia pasipo kufanikiwa.
Niliyakumbuka maneno ya Rose na yale ya babaake siku chache nyuma hospitalini. Ina aana yale yalikuwa maneno yao ya mwisho na sitowaona tena? Niliumia zaidi kila nilivyotafakari chanzo cha yote hasa kinarudi palepale kuwa ni NDOA YANGU.
Ndoa iliyosababisha sasa vifo vya watu watatu sambamba na mamaangu. AaaH
'Asante One. Kwa sababu ya ndoa yako imelazimisha mwanangu asafiri kwenda mbali kutafuta pumziko na kuipata faraja. Na kweli sasa amepata pumziko la milele. Umenisababishi ukiwa sina mke sina mtoto. Asante One kwa kuisambaratisha familia yangu.'
"ROOOOOOOOZZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII"
Nililia kwa sauti kuu ya maumivu huku nikisujudu na kupigapiga mikono chini baada ya kupokea ujumbe wa kuthibitisha ajali ile kutoka kwa mama Rose mwenyewe ambae alionesha wazi amenichukia na kuniweka kuwa chanzo cha ma5tatizo yote. Aaaah! ingawa inaweza nisiwe kwenye chanzo lakini kwenye ndoa yangu kuna chanzo. Oooooopppphhhh!!!! Buriani Rose wangu. Nisamehe uko ulipo aaaah!