Ndoa Yangu

Ndoa Yangu

Yaani hafi episode niyo nimejikuta najiuliza mambo yaliyomtokea one,kuanzia kudondoka na kupoteza fahamu kwa kipindi kirefu,ile ya kuombewa na atu akiwa hospitalini hadi akakiri kuwa alihisi mabadiliko baada ya maombi,kumbe yote yalikuwa madawa ya kichawi tu.

Atu atapigwa na radi moja kali sana
bas nikawa najiuliza huyu one kwa mahaba haya ni ya akili za kawaida au
 
SEHEMU YA 30

Kundi la ndege wa ajabu lilitanda kunizingira kila nilipopiga hatua wakiwa tayari kunishambulia. Ajabu siku ile sikuweza kuwaona wala kuwahisi zaidi nilitembea na kuna muda nilisimama baada ya kuona hali ya hewa ikibadilika pale. Ndege walikuwa wengi ambao sijawahi kuwaona katika ulimwengu wa kawaida. Na kila waliposogea kunishambulia nilimuona akitokea tena yule binti mrembo Suyrashfatina na kuwatemea moto tokea mdomoni mwake. Niliogopa na kumuuliza yule mtu niliyekuwa nasema nae muda wote.
"Nani huyu binti mzuri hivi ni jini ama malaqika?" Pasipo kujibiwa ajabu yule bwana alicheka sana na hapo ndipo mbele yetu tulipowaona mama Atuganile akiwa na lile lijitu akilipa maelekezo huku uso wake ukiwa wenye kukasirika kabla hajaliruhusu liende kunivamia.
"Jaribio la kwanza ulitakiwa utolewe kiini macho kwa kunyanyuliwa na wale ndege wa kichawi, lakini Suyrashfatina amewaangamiza pasipo mama Atuganile kuona na hilo ndilo lilimchukiza hata kumtuma kiumbe huyu ambae ilipaswa akuangamize kimazingara." Sauti ilinipa maelekezo ambayo yalizidi kunipa maswali kwanini mama Atu al;itaka kunifanyia hivyo hali ya kuwa alionesha kunipenda sana machoni? Na hapo ndipo kwa macho yangu nilipomshuhudia yule binti wa ajabu akinivaa mwilini kama kivuli na kuanza kupambana na kile kiumbe hata kugalagazana chini. Vita ilikuwa kali sana ingawa nilishuhudia walipofika mafundi wenzangu na viongozi waliona tofauti na uhalisia uliokuwa. Nilipambana kupitia yule binti wa ajabu na mwishowe nililishinda lile jitu hata kulimaliza kabisa ingawa Suyrashfatina nae alionesha kutweta haswa. Nikiwa nimetaharuki mazingira mara yalihama tena na kutokea pale hospitali nilipokuwa. Nilishangaa kujikuta nimeketi na Atuganile huku fomeni akiwa pembeni akinitazama kwa masikitiko makuu. Yeye hakuwa anaona kama niliketi na mtu na tulikuwa tunazungumza. Nilichokuwa namsimulia Atuganile ndicho kile kilichotokea huku naye akinijibu na kunipongeza kwa kumuangamiza huku akifurahi kuolewa nami. Nilishangaa na kuchanganyikiwa zaidi kwani tukio lile nililiona ndani ya ulimwengu ule kabla ya kuzinduka na kujikuta hospitali ingawa kwenye maono yangu ya awali niliona tupo sehemu tofauti kabisa na Atu.
"Alikuja baada ya zoezi la mamaake kushindikana. Nyota yako One ni kali na Atuganile alikupenda kwa sababu kuu moja. Nyota yako ndiyo nyoita iliyokuwa inasakwa kwenye mzunguko wa nyota yake ili iweze kung'aa kwenye utawala. Ilipaswa wakutoe kafara na wanywe damu yako ambayo pia ingetumika kumtawaza Atuganile kuwa mkuu wa wachawi wilaya ya Kyela. Na njia ya pili iliposhindikana ile ya awali basi kufungua nyota yako kwa kumuoa Atuganile ili afanikishe kuipata damu yako kupitia mtoto wa damu yako. Na hilo liliwezekana siku zilezile za mwanzo wa ndoa yenu."
Maelekezo yaliendelea huku nikizidi kuyaona ya Firauni wakati nikistaajabu ya Musa. Kumbe wakati nikiamini Atu alikubali kuolewa nami eti kwa kuwa ananihitaji ilikuwa sivyo. Atu alikubali kuolewa nami baada ya kugundua nyota yangu ndiyo itayomvusha kwenye kukikwaa cheo cha ukuu wa uchawi Kyela kupitia damu yangu ambayo walishindwa kuichukua kimazingara.
"Sasa lakini mimi si ndie mwanaume wake wa kwanza huyu?"
Niliuliza na pao hapo mazingira yakabadilika tena. Nikamshuhudia baba mtu mzima ambae nilitambulishwa siku ile ya ndoa yangu kuwa ni mjombaake Atuganile.
"Huyu ndie mwanaume wa kwanza wa Atuganile. Na kila ulichokiona kwa Atuganile kuhusu utoto ilikuwa ni kiini macho. Alitolewa usichana akiwa na umri wa miaka tisa. Miaka mitatu baada ya kuingizwa kwenye chama cha wachawi na mamaake."
Nilistaajabu na mara mazingira yakahama tena mpaka Mbeya mjini ambapo nilimshuhudia Atuganile akiingia kwenye taxi sambamba na kijana mmoja tuliyeendana endana kimtazamo wa kimo na hata muonekano wa miaka.
"Huyu ndie kijana ambae kwa sasa ni daktari na amejitoa sana kumsomesha Atuganile tangia kidato cha kwanza. Alitarajia kumuoa Atuganile na aliahidiwa hilo lakini hakukuwa na mapenzi zaidi ya kuwa alikuwa miongoni mwa vijana wengi wajazao sheli."
"Sheli? unamaanisha nini unaposema sheli!"
"Kazi nyengine ya Atuganile ilikuwa kukusanya manii halisi kwa vijana tofauti kwa njia ya kutembea nao kimwili. Na huyu kijana alikuwa na manii zilizowafurahisha wachawi wengi kila alipokamuliwa na kuhifadhi kwenye tenki maalum la mkeo lililohifadhiwa ndani ya uke wake. Hii inaweza kukuchanganya wala hupaswi kuuliza mengi ni sheli ya nini lakini utambue kuwa nia ya mapenzi kwa kijana huyu ilikuwa kumkusanya manii tu ambayo ilitumika kujaza vyombo maalum vya usafiri wa kichawi."
"Mungu wangu! ina maana hizo manii ndio mafuta?"
"Naam, ndiyo maana yake. Atuganile alikuwa kama sheli ya kuhifadhia manii za vijana wanaochemka damu ipasavyo kwa niaba ya kukusanya mafuta ya vyombo vya kichawi virukavyo usiku. Dunia hii wapo mabinti wengi wanaofanya shughuli hiyo wengine kwa kujitambua kama Atuganile na wengine kwa kutojitambua. Wanapokua na vitu hivyo ukeni hawawezi kushika mimba kamwe pasipo kuvitoa. Na muda mwingi huwaletea hamu ya kufanya tendo kwa wale wasiojijua na kwa wanaojijua kama Atuganile hawakuagi na hamu yoyote ya tendo."
Maelezo yaliendelea kunifunua akili huku mazingira nayo yakizidi kubadilika na kuonesha matukio mengi tofauti yaliyozidi niacha kinywa wazi.
Baada ya kushuhudia hilo mara ndipo mazingira yalipotuhamisha mpaka Morogoro kule nilipomlipia Atuganile ada na kujiunga na shule kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Sikuamini mazingira yalivyokuwa yanabadilika na kile nilichokuwa nakiona. Atuganile aliwavuruga walimu mpaka wanafunzi kwa ngono tena zisizo salama ikiwa katika zoezi lake endelevu la kukusanya mafuta.
Sikuamini kila nilichokuwa nakiona kwenye ulimwengu ule ulionirudisha nyuma na kunifunulia uchafu wa mtu niliyemuamini na kumpenda mno.
"Kwa hiyo kipi hasa kilikuwa kinamfanya ashindwe kufaulu darasani? Na mbona aliipenda shule?" Niliuliza kwa mshangao.
"Shuleni kuna mabalobalo wengi ambao hukaa muda mlefu pasipo kuchuja manii zao. Hiyo ndio njia kubwa iliyomvuta Atuganile kupenda shule lakini si kupenda masomo. Hakuwa msomaji zaidi aliwachezea vijana wengi wakiwa usingizini ama kwa njia halali."
Baada ya kuyaona mengi yaliyopita ambayo sikuyajua mara nilishangaa kujikuta kwenye mazingira yajayo kwa mujibu wa mwenyeji wangu ambapo mbele yetu nilimshuhudia Atuganile akiwa amepambwa amependeza mno. tena sehemu yenyewe ilikuwa ngeni siifahamu lakini kwa alivyopambwa na alivyochorwa ilionesha wazi alikuwa anaolewa lakini kwa ndoa tofauti na imani zetu. Alikuwa anaolewa kama binti wa kiislamu na mzee mmoja mnene mwenye ndevu nyingi tena akionesha wazi ni tajiri kwa hali ile ya sherehe na mazingira ya ndoa yalipokuwa yanafanyika.
"Wapi hapa? na aliolewa lini tena?"
"Hapa ni Tunduma na huyo ni mkeo Atuganile miaka mitano ijayo ataolewa katika utabiri na tajiri huyu kutoka Sudan."
Nilishangaa na kustuka sana. Atuganile ataolewa na tajiri kutoka Sudan? tena ndoa ya kiislamu? Ina maana Atuganile atabadili dini? Na vipi kuhusu Uchawi?!!
Nikiwa nimejawa maswali kabla sijauliza mara akili ilizima tena na sikukumbuka chochote.
********
Mauzauza yaliendelea nikiwa kweny usingizi ule wa nusu mfu ndani ya wodi malum ya wagonjwa mahututi. Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya tatu ambapo kwa mara ya kwanza niliweza kujitingisha na kurejesha tumaini jipya kwa madaktari na ndugu waliopata taarifa kuwa fahamu zangu zilianza kurejea taratibu.
Sikumbuki hata mara ya mwisho kama tuliagana ama tuliachana vipi na yule mtu wa ulimwengu ule wa ajabu ambaye aliniacha katikati ya maswali mengi tafakuri nzito.
Hali yangu ikaanza kutengemaa katika ulimwengu wetu wa kidunia. Nilihamishwa mwishowe baada ya wiki moja na kurudishwa wodi za wagonjwa wa kawaida. Tokea nilipopata fahamu sikuweza kuzungumza kabisa hata nilipojaribu na kujitahidi sauti haikutoka. Midomo ilikuwa mizito kunyanyuka. Sijajua kwanini ingawa wataalamu waliwatoa hofu ndugu na jamaa juu ya hali ile na kuwasisitiza kuwa wasiniongeleshe wala kuniuliza maswali yoyote kwa lengo la kutousumbua ubongo wangu sana kwa kile walichobaini kimenikuta kisayansi. Muda wote nilikuwa natafakari hatima yangu nikiwa hospitali. Wengi niliwatambua kwa macho walipokuja kuniona huku wengine wakishindwa kuzuia machozi yao hususani dada zangu ambao sasa tulibaki yatima kamili tusio baba wala mama. Nilitamani niwasimulie mengi niliyoyaona lakini nilishindwa. Hakika Atuganile alinichanga na kufikia wakati kujuta hata ile safari ya kikazi Kyela. Niliyawazia maisha yale magumu kabla ya kwenda Kyela yalikuwa na amani na ndoto zilizoishi ingawa sikuwa na pesa. Lakini ndoto zote zimevurugwa na kuzikwa kwa ndoa yangu. Ndoa ni jambo la heri lakini kwanini imegeuka shari kwangu?
Maswali yasiyo majibu yaliendelea kutafuna kichwa changu na nilidumu pale hospitali kwa wiki mbili zaidi. Na katika wiki hizo sintosahau ile siku alivyokuja Rose akiwa pekee kwenye chumba nilicholazwa. Alikuja akiwa na ua mkononi tabasamu lilimshiba machoni aliponiona nimekaa kwa kuegemea mto kitandani. Ingawa nilistuka lakini hatamimi nilijisikia faraja kumuona. Nilitamani kujua mengi japo sikuweza kuuliza na kuishia kumtazama kwa macho ya aibu na kujiona nisiyestahili kwa ukatili niliomfanyia kutomwambia ukweli wa maisha yangu.
Alipiga hatua taratibu Rose na kuketi pembeni yangu. Siku hiyo ilikuwa siku nyengine ya mwiba wa maisha yangu. Hakika sikujua kama itakuwa mara ya kwanza na ya mwisho kumuona Rose baada ya tukio lile la mvunjiko wa ndoa yetu kanisani. Maneno aliyonena Rose siku hiyo hiyo ndiyo yaliyoiwezesha midomo yangu kucheza na sauti kunitoka kwa mara ya kwanza tangia nipate fahamu. Aaaaah! hakika yaliyonikuta ni mazito yasiyoweza kubebwa popote zaidi ya kwenye msalaba wa Ndoa yangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom