Ndoa yangu inateketea

Umeoa? Una ndoa? Una Watoto?? Huujui unachosema

Jamaa alichoongea namuunga mkono mm nimeoa lkn huwez niambia mwanamke anitushie kuondoka sijamkosea nimzuie kuondoka et kisa nimemuoa au kisa watoto hapana hata mm pia nahitaj sehem tulivu ya amani nyie ndio mnakufa kwa presha na msongi wa mawazo kisa tu unavumilia ujinga wa mwanamk sababu umezaa nae
 
Tatizo lilianzia hapo ulipooa ukiwa na miaka30 tu,,! huo umri bado sana kuwa na mke

Hapana hiyo haiwez kuwa sababu kwahy unaniambia ukitaka kuenjoy ndoa uoe ukiwa na miaka 40 hapo tatizo ni mwanamke huwez shirikisha umri wa jamaa kuoa na ndoa kikubwa swala la mke hapo ni km bahat kuomba Mola ajalie mke aliemwema na mvumilivu weng wao ni wapenda pesa tu ila ukifulia na yeye anakudump
 

Mwanamke ukishamzalisha watoto hasa wawili asikusumbue kwa kukosa kwake akili...


Asipokuelewa hapa basi tena.

Kuna wanawake wawili aina 2 wasikusumbue uliyemuoa halafu bado hamjapata mtoto na uliyezaa nae watoto wawili.

Usiwe loser mto mada
 
pole sana boss!!,,ila nakushauli jali afy yako kwanza ili upone huyo mamy alikupenda kat ukiwa na kaz halafu anajivunia hako kaelimu kake,,,kizur kabisa tayar umesha zaa nae,, ko tulia usimutafute wala kwenda pale kama utaenda nenda kusalimia wtt wako tu,,usiache kuwasalimia wtt hata kw sm enough!!ila in short hakuna mke hapo na ukilazimisha utakufa kwa pressure burs kat bado uko mdogo,, saiv huo ndo mda wa ww kujipanga kutafuta not vizur...
 
Kama tajiri wa dunia aliweza kuachwa na mkewe,kwako ni kipi kisichoweza kufanyika? Huyo mwanamke hakuwa pacha wako,zunguka dunia nzima tafuta pacha wako. Wengi tunalazimisha uhusiano kwa mtu ambaye sio pacha wako, matokeo yake ndio kuumizana kwenye mahusiano.
NB:
Pacha-ni mtu mnayeendana kitabia, kimawazo, kihisia n.k
 
Maelezo yako yanaonyesha ni jinsi gani ulivyo mshirikina,acha mrudie Mungu
 
Anasema kazini kwake hajapandishwa mshahara!?.Hapo tatizo pesa,amechoka kukulea na kutimiza majukumu yako.
 
Pole mkuu.. kufanya maamuzi ukiwa too emotional hayatakuwa ya busara na ukajutia baadae.Chamuhimu kwanza afya yako..Kipindi unarecover,tumia muda huo kujipa break naye(kwa makubaliano ya pande zote)Naamini haka kamuda kakutafakari katakujana maamuzi mazuri kwa faida ya pande zote

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Hawa wanawake wapo wa aina mbili
1. Anayekupenda wewe km ww. Hapa uwe na hela au hauna bado mtakuwa naye
2. Wanawake wanaopenda vitu. Ukiwa na pesa mtakuwa naye, ila siku ukiwa hauna unakuwa mzigo kwake.
Mwanamke uliyenaye ni huyo type ya pili. Km unampenda na unataka mrudiane. Tafuta pesa atarudi mwenyewe. Tofauti na hapo huwezi kumrudisha.
Nashukuru kwa kunifariji mkuu,yaan kumpoteza mtu uliyemthamin na kushea mambo mengi inaumasana
 
Well said! But jamaa has to move on, asisumbuke kutafuta pesa kwa ajili ya kumridhisha huyo chui aliekua kavaa ngozi ya kondoo..

Hapo MUNGU amsaidie apone kisha apate machungu ya kutafuta PeSA ajiimarishe zaidi kiuchumi asipoteze muda wa kumfikiria tena huyo mwanamke. Atakuja kupata mwingine tu wa kukubaliana na hali yake wakati wote.
 
Bro unatafuta nini kaka!! maisha haya yana muda na hua tunapata funzo, Mungu yupo kuwa karibu nae sana kipindi hiki, tafuta kazi taratibu walau ya kukupa riziki, sali sana, usikate tamaa, sali sana, kuna kitu kikubwa Mungu amekiweka mbele yako, usimlilie mwanamke kwa tamaduni zetu za kiafrika ni mbaya, si uanaume, najua kwa hizi stress za sasa huwez kua na hisia na mwanamke, tulia tafuta kazi!! hayo unayopitia ni ya Muda, Mungu akusaidie!!
 
Daah hapo kikwazo ni wewe kukosa pesa, pole sana mkuu, hapo mke huna piga goti chini muombe mungu atakufungulia njia
 
Ndugu yangu japo mimi mwenyewe sina experience kubwa sana na ndoa ila kwa kusoma hili andiko lako kuna mambo kadhaa nimefikiria na pengine yanaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Kwanza binafsi naona kama kuna shida au jambo ambalo L imefichika kwenye ndoa yenu na jambo hilo inabidi uanze kufikiria tangia kuanza kwa mahusiano yenu hadi maisha ya ndoa kwa kipindi chote ambacho mmekuwa pamoja. Kuna kitu ambacho kama ukiuunganisha vipande vidogo vidogo vya mahusiano ya ndoa utakuja kukipata.

Pili kushaurisha mtandaoni siyo mbaya ila binafsi ningeshauri ungeanza kwa wazee kwanza, ikiwezekana familia yako na yake zikae pamoja, mazungumzo yafanyike naamini palipo wazee hakuna kinachoshindikana na hapa ikishindikana basi huyo mwanamke atakuwa siyo sahihi kwako

Tatu kama mlifunga ndoa kanisani au Msikitini siyo mbaya pia kama ukiweza kupata ushauri kutoka kanisani au msikitini. Inawezekana huyo mwanamke amedanywa na kitu kidogo ila kama mazungumzo yakifanyika anaweza kujirudi na mkajenga ndoa yenu.

Mwisho nakushauri utumie hekima, busara na akili yako yote ktk kufanya maamuzi maana ndoa inapovunjika wahanga wakuu huwa ni watoto ambao hawana hatia.

Nakuombea na nakutakia kila baraka na Neema ya Mungu ktk hili ndugu yangu.
 
Ukweli ni kuwa asilimia75 ya wanawake wenye ajira, wakishapata watoto wawili au watatu Ila hasa wawili wanapenda kuishi na watoto wao tu ili wawe huru,
Ili mume uvumilike ukubali kuwa Mjinga mjinga kwa mkewe Kama ushauri alio utoa mwijaku kwa pett .
 
Sasa unamkomoa nani? Wenzio wanakuchuna, hata ukiwazalisha matumizi unatoa. Hapo hujawakomoa.
 
Hakuachwa, aliacha. Elewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…