Ndoa yangu inateketea

Wee Jamaa kabila gan?? Nadhan wee ni mmoja ya wale wanaoamin. "Ukioa mchaga, atakuua".



Yaan mimi nimesoma na mwananke wangu, tumemaliza chuo, tumepata kazi, tumeoana,... Alafu ulitaka tulipomaliza tuachane kisa yeye ana elimu ? Na kazi pia??


Wee ni mkurya ??


Wewe ni aina ya Wanaume wakoloni, wanaopenda kunyenyekewa , hawapendi wanawake wasonge mbele, yaan wale ambao utasikia. "Usisomeshe mtoto wakike".
blaza unapotoka!
face the reality
 
Ndugu yangu amani ya bwana iwe nawe!,pole pia kwa kusumbuliwa na ugonjwa pamoja na changamoto za maisha
Kwa kipindi hiki naomba umuache mama kwanza atulie yamkini kuna mambo hayako sawa kati yenu ama amekengeuka kutokana na wewe kutokuwa na maisha yanayoeleweka,mpe nafasi ya kujitafakari na wewe pia jipe nafasi relax,unapoendelea kumzonga ndo utapozidi kuharibu mambo
Katika kipindi cha kila mmoja kujitafakari ikitokea mwenzio anakuhitaji basi atakutafta na ikitokea hakuhitaji tena basi hauna budi kuupokea ukweli mchungu
N.B
Ila kitendo cha kuomba uhamisho bila sababu ya msingi,kwenda kukaa kwao,kuacha kuja kwenye msiba wa baba yako ndugu yangu mapenzi yameshindikana,sie mengine ya nyuma ya pazia hatujui lakini ni bora uupokee ukweli huu na usimlazimishe muache kwanza
 
Its not that easy makaveli10 kumbuka wana watoto na ni mke wa ndoa, ni kweli kulazimisha penzi haiwezekani lakini inabidi ajitahidi kutafuta suluhu au kujua shida iko wapi
Kwa mujibu wa maelezo yake hizo ni jeuri za kike baada ya kipato, unachozungumza ni kweli, sitaki kupinga, watoto isiwe kitanzi cha mtu kujifia kwa kihoro, mpaka sasa naona mshikaj hana moyo wa kiume, kashindwa kuhandle hii kesi, kwa haraka haraka huyu mwamba anaweza kuja kufa kwa msongo wa mawazo, hili suala linampa tabu
 
Hapa ishu ni kwamba kwao ni karibu sana na sehemu yake ya kazi ndugu yangu,kuepusha usumbufu niliona ni vyema akae kwao kwa mda.mimi kwetu ni mkuranga.sasa kutoka mkuranga mpa UDSM ni mtihan
Anaingia kazini saa ngapi?mimi naishi mkuranga na familia yangu,mwanangu anafanya kazi masaki kila siku ananenda kazini kutokea nyumbani mkuranga.Najua anachoka sana lakini kumruhusu mkeo basi siku mbili alale mjini kwao sidhani angesema anachoka.
Kuhamia mkeo Dar akaishi kwao ndio kaburi la ndoa yako.Ndugu,wakwe na bwanazake wa ujanani wakashona sanda.Wanawake wakiwa na kipato kumshinda mwanaume wanakuona kama mnyonyaji na huijali familia.Wazazi wa mke kama wako wanaoona wewe ni mzigo kwa mtoto wao,lakini ingekuwa mke anakutegemea wewe kama housewife wangeitisha vikao vya kukusema unaharibu ndoa ujirekebishe,lakini hapa inaonekana wao wanaona ni sahihi na baba yako hawezi kuitisha kikao cha usenge kama huo.
Hata tukushauri nini,u r the decision maker,na hapa u will have to make a very tough decision.Ningekuwa mimi ningekubali alichosema na kukaa pembeni,mapenzi hayalazimishwi hata kidogo.Kuna Muda huwa tunadhani kulipigania penzi ndio ukamilifu wa mahusiano,lakini ninasema kuna muda wa kuliachia penzi hata kama kuliachia kuna maumivu makubwa kiasi gani.Ukimuacha mtu unayempenda kwa dhati aende huwa unahisi a part of your heart is being torn out lakini kumbe ukiendelea kumng'ang'ania mtu huyu your whole heart will be ripped open sooner or later.
Ushauri wangu kwako, la kwanza kwa vile unaumwa angalia afya yako ili uiimarishe then ndani ya muda wa kujiimarisha kiafya digest the news za kuachana. mwisho umuulize hatma ya watoto wenu,Imagine mpenzi wako akuambie muachane alafu umpe jibu la straight kuwa nimekubali kuachana!Tafakari ndugu.
Mwisho,mlifunga ndoa au sogea tuishi?Kama mlifunga ndoa ni kwa dini gani?
Pole kwa kuumwa,pole kwa kupitia unayopitia lakini hakuna refu lisilokuwa na mwisho,Muda kupita ni tiba ya matatizo kama haya.
 
Kuanza upya si ujinga kubali kuwa mapenzi yameisha lkn maisha lazima yaendelee
 
Hapa ishu ni kwamba kwao ni karibu sana na sehemu yake ya kazi ndugu yangu,kuepusha usumbufu niliona ni vyema akae kwao kwa mda.mimi kwetu ni mkuranga.sasa kutoka mkuranga mpa UDSM ni mtihan
Hapa ndipo tatizo lilipoanzia. Hukujua maana ya mkeo kwenda kwao na wewe kurudi kwenu, ni kwamba ulishindwa maisha ya kuwa na mke na familia.

Ilitakiwa baada ya kupata uamisho usimamie utaratibu wa nyumba atakayoshukia, yaani kwako hata kama ni kukopa pesa au kumhimiza yeye akuazime pesa ila wewe ndo ukatafute nyumba na kumuandalia mazingira ya makazi yenu mapya.

Hili la kumuazima ni la mwisho kabisa, ilitakiwa ukope popote kwa ajili ya familia yako maana uhamisho haukuja ghafla.

Hata hivyo huu ni wakati wa wewe kuipigania afya yako kisha urudi kwenye kupigania kipato chako. Usitake akuonee huruma na usikae kinyonge wewe ni mwanaume kubali hali kisha pigana.

Kwa uzoefu wangu huyu mkeo atarudi mwenyewe kuipigania ndoa yake pale utakapotengamaa na kuwa na sifa za mume mwenye uwezo wa kumiliki familia.

Kwa sasa kama anataka kukuacha mwambie yeye ashughulikie divorse paper wewe bado haupo tayari kumpoteza ila kama ni lazima sana utazisaini. Halafu watoto wako wapo kwa nani? Hilo la watoto liangalie kwa makini sana. Usije ukaacha kuwa sehemu ya malezi.
 
Fimbo ya dunia nzuri zaidi amuache tu kiroho safi asikunje roho . Mke ameolewa na unarudi kwenu unapokelewa na una watoto na mume ... Hivi unaanzaje kumwambia dingi issue za hivyo ....kuna shida mahala ...
Achilia mbali hayo mengine ila hili la mke wa mtu kurudi kwao na wazazi wakalikalia kimya,hili ni tatizo kubwa sana.

Wazazi hasa upande wa wake zetu huwa wanachangia sana kuharibu ndoa za watoto wao.

Huku kwetu huu ujinga haupo. Kwanza ukija tunakurudisha tuna kuuliza umekuja hapa nyumbani kwa ruhusa ya nani na wewe ni mke wa mtu ? Hapo tuna wasiliana haraka na mumeo.
 
Hapa ishu ni kwamba kwao ni karibu sana na sehemu yake ya kazi ndugu yangu,kuepusha usumbufu niliona ni vyema akae kwao kwa mda.mimi kwetu ni mkuranga.sasa kutoka mkuranga mpa UDSM ni mtihan
Hili kosa lingine ulifanya mzee.
 
Mtu kaamua had kuama mkoa ..huyo alijiandaa shekhe..na chanzo ni ngawila

Yaan ishu ni huo upangu pakavu..

Ndio maana mim nawatindua vibaya mno na kuoa sioi ngoo...wacha wanichune tu..ila kuoa wasahau..ni mwendo wa kuwazalisha na kuwaacha tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi huna!

Hela huna!

Afya mgogoro!

Mke amesema hakutaki!

ILA BADO UNALAZIMISHA MAPENZI.

TAFUTA HELA NA KAZI KWANZA. PIA PIGANIA AFYA YAKO.

NO MONEY, NO HONEY!

MAPENZI ULAYA AFRIKA NI BIASHARA.
 
Back
Top Bottom