Mwache aende mkuu japo ni ngumu kuhandle hali hiyo.
Chukua watoto uishi nao,hapo kwako itakuwa rahisi sana wewe kumsahau yy.halafu pambana kuzisaka kwa namna yoyote ile ili wanao wawe katika furaha tu.
Mwanamke akikutamkia hakutaki hilo ni jambo la kushukuru mungu sana tena sana.
Naamini kama watoto ulikuwa unaishi nao vizuri na walikuwa wanakukubali basi jua hawawezi kukusumbua kuhusu mama yao.
Mfano mimi mwenyewe
Ndoa yangu ya miaka 8 niliivunja mwaka huu mwezi wa pili.baada ya maugomvi yasiyoisha ndani kila siku.nikabaki na wanangu wawili mkubwa miaka 7 na mdogo miaka 4.
Nini nilifanya?
Baada ya kuachana nae nilifuta mawasiliano yake kabisa na kumblock kila sehem.
Nilitafuta kisimu kidogo na laini yake vipo nyumbani nikampatia namba kama atataka kuwasiliana na watoto apige kule ataongea nao.
Na iko hivyo hadi ninapoandika ujumbe huu.amekuwa akinitafuta kwa namba tofauti na kutuma tena wazee kila mara lakini hii safari haiwezi jirudia tena na tena.na kila namba anayonitafuta nayo yaani ile nikijua ni yy hakuna kinachofuata zaidi ya block tu.
Kwangu nimefanikiwa hili jambo kwa asilimia kubwa sana.kwa sababu....!!!!!
Nilijenga msingi imara kwa wanangu tangu yy akiwepo na nilikuwa naplay part kubwa sana ya baadhi ya majukum pale nyumbani ndio maana hata yy alivyoondoka wanangu hawajawahi kunisumbua mama yao yuko wapi na kwa nini kaondoka?imagine mtoto wa miaka 4 tena wakiume unadhani huo usumbufu ungekuwaje kuhusu mama yake?lakini huyu wangu hajawahi kuniuliza.unajua kwanini?
Yeye akiwa nyumbani anafanya majukumu yake,na mimi ilikuwa nikirudi kusaka mkate nilikuwa nafanya pale alipoishia yy.kuna nguo chafu nafua,chakula bado basi nafanya maandalizi yote na kupika kuna sehemu hapajakaa sawa ndani narekebisha then naendelea na mambo yangu mengine.uzazi wote wa watoto wawili sijawahi saidiwa na mtu hadi kumkanda ni mimi mwenyewe imagine hapo.
Kila siku watoto nilikuwa naamka nao,nawaogesha,niwape kifungua kinywa naondoka nao nawapeleka shule ndio nami naenda kibaruani kwangu.
Haya mimi nimeyaweza sababu malezi yangu sikulelewa kumtegemea mtu bali asilimia kubwa nijitegemee na kazi nyingi za nyumbani kwetu ilikuwa hazichagui wakike wala wakiume mpaka tunakuwa wakubwa.
Bro mambo ni mengi ila mteme huyo vinginevyo utaishi kwa tabu sana duniani hapa.hii vita manabii wenyewe waliopewa hekima na uwezo na muumba waliishindwa sembuse sisi.
Pambana upate hao wanao ukishindwa kukaa nao kutokana na changamoto za kimajukumu basi peleka kwenu hapo upambanie mkate wao tu huyo chap sana unamsahau.
Si lazima tuoe tena hali ya kuwa watoto tayari tunao kama hivi.mbususu mtaani kibao ni sisi tu kuchagua ipi inafaa kwa siku hiyo


..
MUNGU AKUSIMAMIE KWA KWELI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU UNACHOPITA..
Ila hapo mapenzi hakuna tena zaidi ya mateso kwako