SOUND SYSTEM
Member
- Aug 31, 2021
- 39
- 59
Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.
Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.
Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa
2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.
Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).
3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.
4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.
Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.
Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.