Ndoa yangu changa inataka kuniua

Dah! ila huyo mke wako bwana

Inawezekana kuna kitu anakifanya huko kwao au sehemu nyingine ambacho kinahitaji hela, heba ongea naye afunguke.
 
Mkuu, umeoa mke au umeoa mwizi?

Huyo ni mdokozi kwa asili lakini pia tabia yako ya Ubahili wa kutompa hela inakuponza.

Atauza vyote. Vitu vya ndani vitaisha, itafuata gari kisha nyumba . Baada ya hapo nguo zako alafu utabakia wewe na mtoto. Nani atangulie kuuzwa?

Bila kufumba macho ni wewe. Utauzwa abaki yeye na mtoto.

Kimbia Mkuu. Mtu asiye na soni hata ya kupunguza hela ya sadaka ni mtoto wa Lucifer tu.

Kimbia. Viatu vikikatika wewe kimbia, bora miiba kuliko kuuzwa. Kimbia Mkuu.

Chaguo lako ni kukimbia ama kuamua kumpa hela zote unazopata. Chagua kwa busara.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo isue ndogo sana mkuu! Weka hela peupe tu usifiche pia tumia Teknolojia sana hasa cctv za siri. Weka hela makusudi uwe unamshika kabisa na kuonekana ni yeye amefanya. Ukimsha mshika unamwita unamuonesha unakaa kimya unaendelea na mishe zako kama hujamkamata vile. Silence is more powerful than proving a point. Pia jitahidi usitoe siri za mke wako kwa watu akija jua unafanya hivyo uwa wanamaamuzi ya kijinga mtunzie siri zake ataacha tu.
 
Umeshauri kwa akili sana
 
Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
NDOA DOA OA AAAAA
 
Kama ningekuwa mwanaume nisingeweza kuishi na mwanamke mchafu, mimim ni msafi hatari, umesema mwizi? achana nae tafuta mchepuko. Wanawake wako wengi kwa nini ujitese kha!
 
Sasa anajiibia hadi yeye mapazia ya kupendezesha nyumba yake,na kwann anakuwa hivyo au humpi hela ya mahitaj yake binafsi kwann haridhik
 
Wahesimiwa wa mmu, ndoa yangu ya mwaka mmoja inakaribia kuniua, ushauri wenu muhimu sana.

Huyu mwanamke nimejuana naye miaka miwili kabla sijaamua kumuoa, ingawa pia maamuzi ya kumuoa yaliharakishwa na kumpatia ujauzito akiwa mwaka wa pili chuo.

Matatizo sasa yanaanzia hapa:
1. Baada ya kumuoa katikati ya mwaka jana akiwa anakaribia kurudi chuo, aliamua kujifukuzisha chuo kimya kimya kwa kutoingia darasani. Ni mpaka mwaka huu mwanzoni ndo nilipojua ukweli, nikamsaheme nikifikiri ni mimba iliyomfanyia hivyo na nikamsaidia kuchaguliwa kwenye chaguzi za juzi hapa

2. Alianza tabia ya kuiba hela nazo rudi nazo nyumbani, hapa nikafikiri ni mdada wa kazi baada ya kumtimua lakini tabia ikaendelea. Hapa ilinilazimu niwe naficha hela kwenye gari.

Si akaja kugundua akaanza kuzifuata huko huko kwenye gari, sasa hapa nikawa nazificha sehemu ambazo asiye fundi hawezi zifikia. Hapa kunaujinga mwingi sana umefanyika mpaka ikafika yeye kukata hela ya chakula.
(Anabana hela ya chakula, chakula kina kata katikati ya wiki).

3. Wizi wa hela ya sadaka, hapa niliandaa hela ya sadaka ya shukrani, nikaiweka kwenye bahasha na tukaiombea, nikafunga bahasha na gundi. Kesho yake asubuhi tunaenda kanisani nikagundua bahasha ilifunguliwa na nusu ya hela imepigwa.

4. Kuna vitu vimeanza kutoweka nyumbani, begi kubwa la nguo, set za mapazia niliyonunua kwa bei kubwa, simu yangu ya ofisini (Naitumia mara chache, kwa shughuli za ofisi) na godoro dogo la chumba cha wageni. Nilivyoongea naye jana kuna kila ishara kuwa ameviuza.

Dah naombeni ushauri maana najiona kabisa kwenda kuua mtoto wa watu, maana sioni kitu anachokifanya na hizo hela zaidi ya nyumba kujaa makopo ya juice na soda.

Na hata hivyo ameanza uvivu, usafi kwake ni changamoto saa nyingine naogopa kwenda jikoni.
Daaaahhh mkuu pole sanaaa aiseee hii dunia ina watu🥺🥺
 
Kunavitu havihitaji ushauri mwingi maana maamuzi yanatokea baada ya matendo, hata hivyo unajitahidi maana sio kwa matendo hayo halafu unakuja kuomba ushauri,,,, kunavitu vya kuomba ushauri vingine unatakiwa Halmashauri ya kichwa ikae na kutoa maamuzi.

Hafai huyo mwanamke japo unampenda lakini yeye hakupendi.
 
Back
Top Bottom