Ndoa ya CCM na CUF ilifanyika lini?

Ndoa ya CCM na CUF ilifanyika lini?

Wengi maana yake ni kwamba siyo wote. Mwaka 1995 na mwaka 2000, CHADEMA hawakusimamisha mgombea wa Urais, badala yake walimsapoti Lipumba, lakini NCCR Mageuzi, TLP na UDP walisimamisha wagombea wao. Kama CHADEMA wamegeuka U-Turn, ni chama gani kingine kinamsapoti Lipumba sasa?


Madai kuwa walikuwa wamekubaliana siyaamini kwa sababu wasingefanya hivyo kisiri sisiri kufikia makubaliano hayo bila kuyatangaza hadharani, vile vile vyama hivyo visingeweza kukaa kimya iwapo mwenzao CHADEMA angewakuwa amewasaliti. Lipumba mwenyewe hakulalamika, badala yake alisema Slaa anakubalika lakini hata yeye ataingia tu kwenye kinyang'anyiro hicho kwa madai kuwa hakujua kuwa CAHDEMA wangemsimamisha Slaa.
Hii ni dalili ya kuogopa tu. Kama kuna kujiamini kwa nini kumjali Dr Slaa
 
kama Chadema ingekuwa na uhakika wa kushinda ingepokea sh. milioni 100 kutoka kwa Sabodo wa CCM.

Hiki ni kipindio cha mavuno wajomba.... kuna michango mingi sana inatolewa ya siri na ya dhahiri.... huuu ndio wakati wa ku make infact wagombea na wapambe wao wanatamani iwe hivi kila baada ya miaka miwili....
 
Kuna habari ambazo nina wasiwasi nazo ,habari zenyewe ni kuwa Chadema imetumika katika kuiletea ushundi CCM na ni pale Slaa alipopiga U-TURN na kujiingiza katika kinyang'anyiro cha Uraisi ,ikumbukwe kuwa wengi wa wagombea wa vyama vya upinzani walikuwa wameshaamua kutogombea nafasi hiyo ,na wote kuelekeza nguvu zao katika kugombea ubunge.

Hapa tayari Watanzania walikuwa wameshalenga shabaha ya kuiangusha CCM kwa kupeleka nguvu zao kwa Mgombea mmoja tu wa CUF ,Lipumba ,mgombea ambae angeweza kabisa kuilaza CCM kutokana na kura zitakazo miminika kutoka vyama pinzani.

Ingawa wengi hawafahamu kilichomsukuma Slaa kugombea nafasi hiyo ,wenyewe ndani ya Chadema wanadai au yeye mwenyewe Slaa anadai kuwa wamempendekeza, ingawa yeye mwenyewe alikuwa hataki kuingia katika ugombea huo,hizi ni mbinu za kuwateka waTanzania na kuwalaghai kuwa ni mapendekezo ya Chama. Hapa mkae mkielewa kuwa pamechezwa mchezo mkubwa sana na kuwafanya hata wale waliokuwa na msimamo mkali wabaki wakiamini kuwa Chama ndio kimependekeza ,nawaomba mjaribu kuchunguza kwa kina kabisa mtauona ukweli kuwa hapa CCM wametumia karata yao ya kuwa na chama risavu ambacho ni Chadema,huwezi kuamini kirahisi lakini siasa ndivyo zilivyo wanaofahamu ni wachache sana.

Wengi tulishangaa sana na kutaka kujua kilichomsukuma Slaa na sasa imeeleweka kuwa CCM wamemtumia na wameshafanikiwa katika kuwagawa WaTz kwa mara ingine,you must think hard to get the inner core of the Slaa turning factors.

:A S-danger:
Nafikiri wewe ulistahili kuwemo kwenye maandishi mekundu. Hivi unadhani sisiemu watapata asilimia ngapi ya kura mpaka uwe na wasiwasi wa Lipmba au Slaa wasishinde. Jaalia sisiemu wakapata asilimia 20 na zilizobaki wakagawana CHADEMA na CUF. Hapo ndio utaona jinsi upeo wako ulivyoo.
Hebu kuanzia leo ufanye utafiti kujua fikra za watanzania kama bado zinategemea kura za kuungaunga. Vyama vya siasa havitaungana kwani sisiemu haijaungana na chama chochote, kila chama kina sera zake, sisiemu wanajua wamechoka na leo wameanza na mtindo wa siasa za kulipwa, "Fika mkutanoni, kaa mpaka mwisho then kula buku 5". Si ndo ivo bana. Sera zinaanza kutoa jibu
Pole kwa uchovu wa kutafakuri, au ni swaumu kaka?
 
Ukitaka kujua ni kweli angalia profile yako below; umejiunga humu jana kuchafua hali ya hewa huku ukijua mna hali mbaya.

ANTIBAYOTIKI
user-online.png
Member
Join Date Tue Aug 2010
Posts 42
Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power0
.

mimi nafikiri profile is nothing to do with facts and reality. Tuangalie hoja sio wasifu wa JF member hiyo haitusaidii kufikia hitimisho la mada iliyo mbele yetu
 
Mkuu Karibu,

Naona tangu March 2008 ulikuwa umepimzika maana post ni kama data inavyooshesha hapa chini. Huu ni wakati muafaka tuliendeleze libeneke. Mimi nimeshahamasisha ndugu zangu na marafiki hadi mitaani kwangu wampigie Dr. Slaa. Hata kama kura hazitatosha kugawana na JK lakini nataka apate kura ambazo ni mwamko, na iwe njia ya kuandaa kuingia Ikulu 2015 Kila kitu kina mwanzo wake. Nataka mpambano mkali, ikiwezekana watoke kwa penalty!!! Na hapo tuanze kuzungumzia serikali ya umoja!

Today 01:44 PM #80
Mwanajamii


user-online.png

Senior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Wed Mar 2008
Posts 60
Thanks : 2
Thanked 4 Times in 3 Posts
Rep Power 23


ndugu, mwanajamii kampigia debe mgombea wake KIKWETE wewe umempigia debe mgombea wako DR Slaa sasa mbona unasema mods amfungie mwenzi mwanajamii? Mods ni muungwana sana hafungii bila vielelezo vya kutosha.
 
Nilijisikia vizuri sana kuwa member hapa. Nikatoa michango yangu bila unafiki kwa kipindi kirefu tu. Na baadaye na mimi nikaanza kuanzisha thread, bado ni chache. Huwa napenda kuchangia zaidi. Ninapenda wageni ila sipendi wageni wasiokuwa na staha na wanafiki ambao wanakuwa wametumwa (vibaraka) wanaolenga kuchafua hali ya hewa. Hata mtoto akizaliwa anapita stages hadi anakuwa mkubwa, nami si mkubwa sana, kuna ambao wako hapa since 2006!!! Hata hivyo, huwezi kuafikiana na kila jambo hapo, ndiyo maana tunakuwa na majibizano, au uchangiaji wa huru. Tatizo langu tu ni pale ambapo unaona kabisa mwanzisha thread hana nia njema kabisa na kinachozungumziwa kwenye thread husika. All ni all tunahitaji wanachama wapya hapa kila siku, ndiyo kukua kwa forum na uhuru wa habari zisizo na uchochezi na matusi. i.e zenye tbs!


Ukitaka jukwaa hili kuwa huru ni pale tu kila mmoja wetu atakapokuwa tayari kuvumilia hasa linapokuja suala la kumnadi mgombea wa chama chochote cha siasa. Kuna washiriki wanataka kuligeuza jukwaa hili kuwanadi wagombea wao lakini hawakubari wengine kufanya hivyo kwa wagombea wao. Hii ni kuifinya demokrasia.
 
A lot will be talked. Tunataka kusikia vyama vitatufanyia nini. Slaa ametoa vipaumbel vyake. Soma MwanaHALISI la leo utaziona. They make a lot of sense!
.

Ni rahisi kutoa ahadi na zikavutia lakini atazitekezaje inahitaji maelezo ya ziada?
 
Halafu wewe ngoja tu,kikwete aende Hospital kwanza

Mgombea wako aliyekutuma hapa ndiyo alilazwa MOI baada ya kuvunjika mkono, Kikwete kakukosea nini kusema aende hospitali kwanza wakati hakwenda hospitali?
 
Mgombea wako aliyekutuma hapa ndiyo alilazwa MOI baada ya kuvunjika mkono, Kikwete kakukosea nini kusema aende hospitali kwanza wakati hakwenda hospitali?

Kifafa hicho cha kuanguka anguka! sasa hivi atembelea Ambulansi
 
atafanya nini maalim seif sharif hamad hata kama akiwa na vithibitisho kuwa alishinda zanzibar lakini kanyimwa ushindi? Je zawadi waliyopewa cuf kutoka ccm ni kusubiri lipumba kutangazwa mshindi wa pili? Na cuf kuitwa chama kikuu cha upinzani?

Wanatumia nguvu zote ili ionekane dr slaa hakubaliki, nina hasira na uchungu kwa yote yaliyotokea, uchakachuaji huu unashuhudiwa na dunia nzima, na wote wana hamu ya kuona what will tanzanians do.

Mungu ibariki tanzania, mungu waumbue hawa mafisadi.
 
Mwafrika, imeelezwa hilo neno ndoa ni tusi kwa wenzetu!. angalia hapa
Matusi hayo.

Mimi ni CCM lakini wewe Pasco hii lugha uliyotumia hapa ni ya kishenzi na si lugha ya kisiasa.

Punguani wahed.
Nisianze nini wewe? hakuna ndoa ya kisiasa duniani, sijawahi kuona, onesha moja kama u mkweli.

Hizi lugha za kishenzi pelekeni hukohuko, kama kwenu ni kawaida wengine zinatuudhi. kama huo si ushenzi na matusi ni nini?
Muafaka wa kisiasa wa Zanzibar ni faraja kubwa kwa Wazanzibari kushirikiana na kuijenga nchi yao, na huo muafaka si ndoa, kufikiri hivyo ni kuwatukana Wazanzibari na matusi si uungwana.

Hayo yalianzia huku bara baina ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa ikiitwa ndoa ikapigiwa kelele kuwa hilo si neno jema ni kutukanana, siku hizi halitumiki sasa

Natoa wito tusilitumie tena neno hili ndoa!.

Pasco
 
Ikiwa CCM na CUF ni wana Ndoa, Basi huu uhusiano wa sasa wa CUF na CHADEMA tutaupa jina la Mchepuko. Sasa sijui mchepuko huu ulianza lini na utakwisha lini. Bila shaka utakwisha pale yule muowaji wa kwanza atakapotaka/ amua. All the best Mchepuko.
 
Back
Top Bottom