Mlachake
JF-Expert Member
- Oct 13, 2009
- 4,412
- 4,559
Kuna habari ambazo nina wasiwasi nazo ,habari zenyewe ni kuwa Chadema imetumika katika kuiletea ushundi CCM na ni pale Slaa alipopiga U-TURN na kujiingiza katika kinyang'anyiro cha Uraisi ,ikumbukwe kuwa wengi wa wagombea wa vyama vya upinzani walikuwa wameshaamua kutogombea nafasi hiyo ,na wote kuelekeza nguvu zao katika kugombea ubunge.
Hapa tayari Watanzania walikuwa wameshalenga shabaha ya kuiangusha CCM kwa kupeleka nguvu zao kwa Mgombea mmoja tu wa CUF ,Lipumba ,mgombea ambae angeweza kabisa kuilaza CCM kutokana na kura zitakazo miminika kutoka vyama pinzani.
Ingawa wengi hawafahamu kilichomsukuma Slaa kugombea nafasi hiyo ,wenyewe ndani ya Chadema wanadai au yeye mwenyewe Slaa anadai kuwa wamempendekeza, ingawa yeye mwenyewe alikuwa hataki kuingia katika ugombea huo,hizi ni mbinu za kuwateka waTanzania na kuwalaghai kuwa ni mapendekezo ya Chama. Hapa mkae mkielewa kuwa pamechezwa mchezo mkubwa sana na kuwafanya hata wale waliokuwa na msimamo mkali wabaki wakiamini kuwa Chama ndio kimependekeza ,nawaomba mjaribu kuchunguza kwa kina kabisa mtauona ukweli kuwa hapa CCM wametumia karata yao ya kuwa na chama risavu ambacho ni Chadema,huwezi kuamini kirahisi lakini siasa ndivyo zilivyo wanaofahamu ni wachache sana.
Wengi tulishangaa sana na kutaka kujua kilichomsukuma Slaa na sasa imeeleweka kuwa CCM wamemtumia na wameshafanikiwa katika kuwagawa WaTz kwa mara ingine,you must think hard to get the inner core of the Slaa turning factors.
:A S-danger:
Sihitaji kuwa na degree kujua wewe ni mkereketwa wa chama gani.
hapo kwenye nyekundu panajieleza.