Habari ya Mujini
JF-Expert Member
- Dec 22, 2013
- 2,518
- 1,046
nimekupenda ghafla...
Mi nateseka sana mpaka sasa nafikiria kamchepuko kakunipa raha napotoka kwenye shida ya mke wangu
Watu kama nie ndo mnazidi kuichafua taasisi ya kinafiki ya ndoa! Yaani watu kama wewe ndo wanafiki wenyewe.
Mi juzi nimeenda kwenye kichen party sie ndo tunaoa, so kama mawifi, na huyo msichana namjua na familia yake. Basi nikaona wamama wanajimiminina wenyeweeee. Ndoa sio rahisi, ndoa uvumilivu,, blah blah blah. Basi mda wakutoka akaniambia Lara nimefundishwa mambo makubwaa sijui kama nitaweza. Mbona ukweli wa ndoa zao hakukumininia japo kijiko tu ujiandae vizuri?
Nikamwambia yaani ukidhubutu kufata hayo mafunzo bwana umemkosaaaa! Nyie mmekutana wawili, mkaridhiana, mkakubaliana mambo yenu, kuamua kukuoa ghafla bin vuu unachukua kanuni za mchezo kwa hii migumegume. Wanamju huyo bwana ni mtu wa aina gani? Anapenda nini? Anahitaji nini? Kipi kina mfurahisha?
Yao yanawashinda wanakuchuuza wewe. Yule mke wa flani mumewe ana mchepuko kila kona ya jiji atakushauri nini, yule mwingine anamfuga mumewe, yule mwingine binti wote wamezalia home, afu ndo waliokushauri jinsi ya kuishina mume! Utalamba joka bibi mda si mrefu.
Ndoa ina yote raha, karaha, huzuni, furaha, utamu, uchungu, amani, usaliti na mengineyo usiexpect raha tu,jipange ndo maana hata refa anaingia uwanjani na red card.
Hili nalo neno... wanasema mvuvi haogopi mawimbi ndugu yangu, kuna siku bahari huwa shwari na kuna siku inachafukaNdoa ina yote raha, karaha, huzuni, furaha, utamu, uchungu, amani, usaliti na mengineyo usiexpect raha tu,jipange ndo maana hata refa anaingia uwanjani na red card.
Ndoa ina yote raha, karaha, huzuni, furaha, utamu, uchungu, amani, usaliti na mengineyo usiexpect raha tu,jipange ndo maana hata refa anaingia uwanjani na red card.