Ndoa sio lelemama

Ndoa sio lelemama

muku

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2014
Posts
313
Reaction score
82
Tumekuwa tukiskia kuwa ndoa sio lelemama kweli nimeamini nina mifano mingi sana ambayo bila kumuona mtalaamu wa saikojia kuoa jibu ni no umri umeenda ila kila nikijiuliza jibu linazidi kuwa hapana.

Wenye ndoa zilizotawala ucheshi,utani na amani nipeni somo ni muhimu sana kwangu ila na mabachelor kama mimi mnaweza kutoa mawazo.
 
Ukitaka upate raha kwnye ndoa,jifunze kuappreciate ur patner ie ujali zaidi mazuri yake
 
Ndoa ni kama ndoano. kuna muda unaikuvulia samaki, Muda mwingine inakuvulia chura magamba. Inabiddi uwe na roho ya kijasiriamali
 
Wewe me, ndoa ipo mikononi mwako ukiamua iwe paradiso itakuwa, ukiamua iwe jehanamu itakuwa. wewe si ndio kichwa bhana. jipange na omba mungu akupe mtu sahihi, ndoa sio mbaya, wabaya wanandoa wasiojua maana ya ndoa. 1417934123209.jpg
 
Watu kama nie ndo mnazidi kuichafua taasisi ya kinafiki ya ndoa! Yaani watu kama wewe ndo wanafiki wenyewe.

Mi juzi nimeenda kwenye kichen party sie ndo tunaoa, so kama mawifi, na huyo msichana namjua na familia yake. Basi nikaona wamama wanajimiminina wenyeweeee. Ndoa sio rahisi, ndoa uvumilivu,, blah blah blah. Basi mda wakutoka akaniambia Lara nimefundishwa mambo makubwaa sijui kama nitaweza. Mbona ukweli wa ndoa zao hakukumininia japo kijiko tu ujiandae vizuri?

Nikamwambia yaani ukidhubutu kufata hayo mafunzo bwana umemkosaaaa! Nyie mmekutana wawili, mkaridhiana, mkakubaliana mambo yenu, kuamua kukuoa ghafla bin vuu unachukua kanuni za mchezo kwa hii migumegume. Wanamju huyo bwana ni mtu wa aina gani? Anapenda nini? Anahitaji nini? Kipi kina mfurahisha?

Yao yanawashinda wanakuchuuza wewe. Yule mke wa flani mumewe ana mchepuko kila kona ya jiji atakushauri nini, yule mwingine anamfuga mumewe, yule mwingine binti wote wamezalia home, afu ndo waliokushauri jinsi ya kuishina mume! Utalamba joka bibi mda si mrefu.
 
ukishajua kuwa katika maisha yoyote hakuna raha tu....bali kuna shida na raha basi katika swala la.ndoa halitakusumbua........

mara nyingi ndoa za siku hizi zinawashauri wengi.....mnategemea mtadumu.....usiri wa mambo yenu wana ndoa hakuna tena siku hizi.......

muhimu kusikilizana, kuvumiliana, kuheshimiana na kuelewana.....
 
lara
Ni kama yamebaki masaa machache uingie kwenye chumba cha mtihani afu mtu anakuletea madesa kibao.Ukiyafwata hayo madesa unaingia chaka mazima muhimu ajiamini tu yale anayoyajua ndiyo yafanyiwe kazi,hata hvyo umempa ushauri mzuri.
 
Last edited by a moderator:
ndoa ina yote raha, karaha, huzuni, furaha, utamu, uchungu, amani, usaliti na mengineyo...usiexpect raha tu!!!
jipange ndo maana hata refa anaingia uwanjani na red card....
Nikweli aisee maana ukifikiria makubwa usipoyapata frustration lazima zizidi
 
Ndoa ni kama ndoano. kuna muda unaikuvulia samaki, Muda mwingine inakuvulia chura magamba. Inabiddi uwe na roho ya kijasiriamali
sasa kuna wengine kila akitupa anapata chura magamba....nimeipenda sana hiyo
 
Hizo mbona kama unaongea theory na sio uhalisia.
 
lara
Umenikosha kwa maneno yako lara 1 naona wewe utanifaa ngoja nijiandae kuleta application zangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom