Ndoa ni tamu sana

Mtoa hoja Mungu wetu si wa michanganyo. Kama mtu amekuwa mwaminifu kwa Mungu hilo suala la mchepuko mstarabu halipo, huo ni uzinzi tu kama ilivyo kahaba/mzinzi yeyote hakuna cha ustarabu, atendaye dhambi ni wa ibilisi
Nashukuru kwa kupigilia msumari
 
Mwanaume ni mbaya sana katika ndoa hasa kila ikifika mwisho wa mwezi,atakamuliwa njee zikiisha ndo anarudi ndani anakuita baby, ovyooooooo,wanaume mungu anawaona,yaani mwanaume akishapata hela anawaza kuchepuka tu!!!!
Si kweli pengine huyo uliyenaye ndio yuko hivyo haimaanishi wote wako hivyo wapo wanaofurahia huo mwisho wa mwezi na familia zao, kaa na mwenzio chini tumia kila namna mpaka amekuweka ndani ujue una nafasi yako kwake itumie hiyo
 
Hahahahahahah hatari lakini salama
 
katika vitabu vyenye kufunza historia ya hekima kuna kisa kirefu cha mtu aliekwenda kwa kiongozi mkuu wa kiroho wa wakati huo kutaka mashauri, alipokaribia mlango wa nyumba ya kiongozi yule alisikia sauti ya mke wa kiongozi analalamika sana, analalamika kwa maneno makali mno, jamaa akashangaa na kuamua kurudi anakotoka, kabla hajafika mbali kiongozi akamuona na kumuuliza kulikoni mbona anarudi anakotoka bila ya kueleza chochote, jamaa akamjibu nimekuja unishauri kuhusu mke wangu yeye analalamika na maneno mengi kila wakati lakini nimefika hapa naona ni afadhali wa kwangu kuliko wa kwako, kiongozi akamjibu rudi kakae na mke wako, nikikuuliza fadhila wanazotufanyia hawa unaweza kuzihesanbu? ndivyo walivyo. Tuwavumilie na tukae nao kwa wema.
 
Safi sana, kwa maana nyingine tusiwe wepesi kusema matatizo yetu kwa watu kila mtu anayo ya kwake
 
Tatizo lipo kwenye malezi tunayoyapata cku hizi. Unakuta mwanamke hamuheshim hata mama yake mzazi, atakuheshim wew mliyekutana chuoni na kuoana?

Bongo saiv kama ulaya. Ndoa magumashi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…