Ndoa ni jukumu linalohitaji upendo wa kweli na kujitoa

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Ndoa ni chama cha majukumu makubwa sana, majukumu ya kujenga familia na kujenga jamii bora na baadae taifa bora. Tulio kwenye ndoa tupongezane na wanaotegemea kuingia chamani mjue tuu hili ni jukumu zito lenye raha na starehe ndani yake na linalohitaji watu wawili wenye upendo wa kweli, upendo ulio mkuu.

Starehe na raha ya ndoa haishushwi kama mana ilivyoshushwa kwa wana wa Israel kule jangwani bali inapatikana kwa kila mmoja kuwajibika katika nafasi yake na kujitoa kwelikweli.



Cc Kuhani Noah Ushimen mrangi Extrovert Equation x

Happy school fees week kwa wazazi wote
 
Ukiwa mwana ndoa wekeza kwenye ndoa yako, wekeza akili, muda, pesa, Upendo nk.
In the long run hutakaa ujute.
Uko sahihi kabisa 100% nakubali kabisa
Hasa hapo kwenye kuwekeza akili
Kuna muda inabidi utumie akili ya ziada kuweka mambo sawa ili kupata msawaziko
All mimi nawashauri vijana waoane katika wanaowapenda mkapendana na mnajuana vizuri
Ndoa ni taasisi ndoa ni heshima
Vijana wengi hushindwa katika ndo kwa kushindwa kujiheshimu yeye kama ni mwanandoa na kupelekea mpk ndoa yake kutoieshimu mpk watu wa nje wakajua hii ndo haina heshima
Ndoa ikikosa heshima kueshimiana na kujieshimu wewe mwenyewe
Matatizo mengi huanzia hapo
 
Ndoa ni Sakramenti Takatifu...

Kwa Wachache waliopendelewa kuipata.
Unajua relationships na ndoa ni kitu huwezi kufake hata, if you consider kwamba it is as though you're constantly monitoring and evaluating each other's behavioral change and development. Ukifake lazima uumie na kuumbuka tu. By nature, love relationship has to be intrinsically transparent in order to be genuine.
 
Wanandoa ni kama viungo day mwili na wanatakiwa kuishi kama viungo vya mwili vinavyoishi kila kiungo kikifanya majukumu yake kwa asilimia miamoja na kwa kutegemeana bila kumlaumu mwenzake.
Macho hutazama, akili hufanya maamuzi na miguu, hutembea kufika eneo linalotakiwa na mikono hufanya kazi.......... n.k.
Na haijawahi kutokea macho yakasema yamechoka kumfanyia kazi mikono na miguu au mikono imechoka kumpikia na kulisha tumbo.....
Na ndio hivyohivyo siku mwanandoa mmoja akigoma kufanya jukumu lake ndoa inakufa
 
Back
Top Bottom