|
|
| Lugano Mwambuja(50) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya. akiwa amelala nyumbani kwake akiuguzwa majeraha ya moto |
^^
Haya wanawake shangilieni, mwenzenu kafanya mpendayo
^^
ni wanawake wachache sana wenye roho mbaya ya namna hii kati ya wanawake 100 watapatikana 3 tu, kwaiyo hatuna cha kushangilia
Sidhani kama kuna mwanamke 'kamili' atakae penda/kuwa na wazo la kufanya haya...
Sidhani kama kuna mwanamke 'kamili' atakae penda/kuwa na wazo la kufanya haya...
^^
Lakini ni furaha sana kutafuta haki zenu kwa mbinu hii?
^^
Huku sio kutafuta haki, huu ni uuaji kwakweli....
Haki tunayotaka wengine si ya kumiliki nyumba iliyojengwa na mwanaume, NEVER...
ni wanawake wachache sana wenye roho mbaya ya namna hii kati ya wanawake 100 watapatikana 3 tu, kwaiyo hatuna cha kushangilia
^^
Kipo cha kushangilia kwa sababu, humu jukwaani ikija mada ya mwanamke kupigwa hata kofi, thread nzima itajaa kwa kashifa na laana za kutosha kana kwamba wanawake wote ni innocent !! Mf. Kuna mada ya Ablessed amewahi kuleta hapa, ni mimi peke yangu niliyesimama kusema wazi matendo kama haya hata wanawake hufanya. Sasa leo mfano huu hapo juu, wanawake wapo kimya, wanasoma na kutoweka! Ndio maana nasema, shangilieni maana mmepata wa kuwakilisha mawazo yenu kwa vitendo
^^
^^
Lakini si mnasema hata mwanamke kumpikia mume tu ni mchango tosha wa kugawana mali? Na asipokubali kuitoa, roho yake halali yako?
I think its your time to celebrate, Women !!
^^
mwanamke kamili yukoje?
Kwanza mwanamke ni lazima hajieshimu na pia haeshimu jamii inayomzungua, pili ni lazima ajue responsibilities zake akiwa kama mama, mke, mtu anaetegemewa kuwa kioo kwa jamii nzima, mtu anaetegemewa kuwa mwalimu kwa generation inayokuja... tatu...
Hiyo yatosha kumfanya mwanamke aweze kufikiri kabla ya kutenda...
Je wewe ni mwanamke "kamili"?
Hakuna cha kushangilia hapo tunahuzunika tu maana hii kitu mbaya na na si ya kuishangilia, kama issue ni kuja juu sababu ya wanawake kupigwa acheni kutupiga, mwanamke hupigwa ka kanga sio makonde, mikanda, mateke aaah hapo lazima tutakemea kama tunavokea tendo la picha hapo juu
Swala la kugawana mali za mwanaume hata kama ni wanandoa, sio swala la kutazama juu juu tu kama wanawake wengi wanavyofikiria.
Unaweza ukaolewa na usipate chochote.
Wengine hatuhitaji mali ya mwanaume ama shilingi zake, we need respect. Nyie wanaume mnatuhumiliate sana kivitendo na kimaneno. Huyo mwanamke akikamatwa, si ajabu kutakua na mengi zaidi ya nyumba and at the end, she was provoked though simsupport kwa alichokifanya.