Ndoa: Mwanamke mpumbavu

Ndoa: Mwanamke mpumbavu

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,463
Mithali 14:1 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe


​
1. Hudharau hekima na ushauri.

Mithali 1:7 Kumcha BWANA ndiyo chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

2. Huchukia maarifa ya kiMungu.

Mithali 1:22 "Enyi wajinga, mtang'ang'ania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha na wapumbavu kuchukia maarifa?

3. Humhuzunisha mama yake.

Mithali 10:1 Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.

4. Mkamilifu machoni pale mwenyewe.

Mithali 12:15 Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza shauri.

5. Hukasirika upesi.

Mithali 12:16 Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara, bali mtu wa busara hupuuza matukano.

6. Hapendi kuachana na uovu.

Mithali 13:19 Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.

7. Mdanganyifu.

Mithali 14:8 Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.

8.Mkorofi na asiyejali.

Mithali 14:16 Mtu mwenye hekima humcha BWANA na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.

9. Huwakasirisha wengine kwa maneno yake.

Mithali 18:7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake.

10. Mgomvi.

Mithali 20:3 Ni kwa heshima ya mtu kuepa ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.

11. Hutapanya mali.

Mithali 21:20 Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo.

12. Hawezi kutatua migogoro yake.

Mithali 29:9 Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.

13. Huichochea hasira yake.

Mithali 29:11 Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.


Je ni wewe? Jihoji.

Mwanamke Mpumbavu | Women Of Christ
 
Mmmmmmh! Ningekuchallange kupitia hio hio bible lakini ngoja niache tu! Maana ubishani wa dini mwishowe blasphemy!
 
Back
Top Bottom