Ndoa inaelekea kunishinda

Ndoa inaelekea kunishinda

Ushauri wenu jamani,

Mimi nimeolewa nipo kwenye ndoa hatujamaliza hata mwaka Ila kinachoniumiza mme Wangu ananisaliti, nimemkuta anamiliki simu ya Siri pamoja na line alikuwa kaficha kabatini baada ya kugombana naye akakubali kuwa ana mchepuko akampigia akaweka loud nikawa nawasikia akamuomba samahani kwa kumchezea akamwambia Mimi nimeoa, nina mke nmeona siyo vizuri kumsaliti mke wangu dada akalalamika we badae akakubali kumblock kidogo nikapata amani.

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.

Msamaha kaniomba Ila nashindwa kumsamehe, naumia sana Bora ningemkamata hata na mmoja nisingeumia sana Ila wa 3 ukitegemea ndoa haina hata mwaka nawaza sijui kalogwa, natamani nimshirikishe hata mchungaji wetu Ila napata wakati mgumu naona ni vitu vya aibu hata kushirikisha watu wetu wa karibu.

Natamani niondoke Ila kinachonipa wakati mgumu tayari Mimi ni mjamzito yaani nawaza ingekuwa siyo hii mimba ningeachana nae ananifanya Hadi nakata tamaa na mimba niliyonayo kitu ambacho ni dhambi.

Naombeni mnishauri nifanyaje nahisi kuchanganyikiwa nakosa maamuzi presha imeshuka naona Kama dunia imeniangukia kweli ndoa ni ngumu sana duh! Mungu anitie tu nguvu.
Kwani wewe kabla hajakuoa hukuwa na michepuko? Mwanaume ukimchunguza sana ndoa itakushinda amekuoa maana yake amekuona unamfaa akaacha wote akaamua kukuweka ndani Ili mpate familia usikate tamaa focus kwenye ndoa achana na mambo ya kumfuatilia
 
Hahaha nilikuwa nimenuna Ila umenifanya nimecheka ushauri wako nitaufanyia kazi
Huu ushauri ndo umeuona wa kukufurahisha?
Na umeahidi kuufanyia kazi basi sawa. Utanitambua vizuri, kwanza nshaongeza mwingine wa nne na nimenunua simu nyingine naicha ktk chaji kibandani siji nayo nyumbani.
 
Ushauri wangu kwako!

Kwasasa muweke pembeni kimawazo na kihisia usije ukakosa vyote, hudumia mimba yako ujifungue salama .. Kumbuka huyo ndio atakuwa faraja yako
Wanawake wengi kwenye ndoa, watoto ndio hua faraja zao na si mme tena, sijui hua kunatokeaga nini
 
hapo chacha kwamba unamuacha mtu kisa kucheat??? aaah utani huo....labda hiyo cheating iambatane na mambo mengine kama vipigo, na matabia mengine mabaya ila cheating plain??? ooohhh tutazikana siachi mtoto wa mtu
 
Usikate tamaa,vumilia tu,Usiondoke pambana na ndoa yako,hao michepuko wanapita tu

Hiyo ndiyo hulka ya mumeo kwahiyo ipotezee usimfuatilie ukimfuatilia utazidi kuumia kila kukicha,kikubwa asikuletee malazi tu.

Hakuna haja ya kushtaki kwa mchungaji

Wanasema ndoa kuvumilia,kwahiyo vumilia.


Wanaume na michepuko kama chura na maji.
shauri kama hizi zimepitwa na wakati, yaani aendelee kukaa kisa mimba kwani baba wa mtoto akifa Leo hiyo mimba hawezi kulea peke yake? afya yako ni muhimu Sana kuliko kitu kingine mama afu muache uoga wa maisha wanawake pambaneni
 
shauri kama hizi zimepitwa na wakati, yaani aendelee kukaa kisa mimba kwani baba wa mtoto akifa Leo hiyo mimba hawezi kulea peke yake? afya yako ni muhimu Sana kuliko kitu kingine mama afu muache uoga wa maisha wanawake pambaneni
Unaanzaje kumshauri mtu avunje ndoa yake??
 
Fuatilia vizuri ndugu yangu. Pengine huyo mchepuko aliepigiwa simu anacheza game tu ili amuharibie mwana kwako. Pengine kawapa hao wengine namba ya mwana ili wamtumie hizo msg kichaa wewe uzishike kiwake.

Mwana upo nae 5 years kabla hajaoa na alikuwa na uhuru wa kuchepuka lakini hakuwa hivyo, Leo miezi sita eti umshike na michepuko mitatu ghafla ghafla?? Mwana sio boya kiasi hicho.

Jengine, enyi wanawake, wavumilieni tu wanaume. Hali ni tete sana!

Kubalini ukewenza acheni kushupaza shingo.

Ukewenza ndio asili ya mwanadam.

Tutaelewana tu kidogo kidogo.


Ukewenza ndio asili ya mwanadamu kivipi?

Mbona ndio ya kwanza Mungu aliumba mume mmoja na mke mmoja tu ? Yaani Adam na Hawa tu?

Ingekuwa ni serious kiasi hicho si Adam angeumbiwa mke zaidi ya mmoja kuonesha msisitizo?
 
Wanawake wengi kwenye ndoa, watoto ndio hua faraja zao na si mme tena, sijui hua kunatokeaga nini
Na Mme siku akichokwa na michepuko na kurudi nyumbani anakuta mama/mke tayari anahimaya yake na watoto wake, anabaki kulia lia mke wangu amewalisha sumu watoto, kumbe sumu aliiacha mwenyewe mlangoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni movie ndio kwanza ipo kwenye ....
”Starring”....“Executive Producers”...”Title”... usijaribu kuvunja ambacho mungu amekiunganisha mkuu!

Nachokiona wewe umeolewa ila ni mgeni kwenye michezo ya mapenzi. Nikutoe hofu tu kuwa wanaume 80% huwa wana cheat ila kwa adabu sana! 20% ndio ambao hawana adabu kwenye cheating wao hawana aibu kuonesha kuwa wana cheat na hawa ndio wabaya sana.

Ukivunja ndoa sababu mume ameku cheat jua uendako pia utachitiwa tu na utakuwa dissapoonted mara mbili! Jifunze kuishi na hio hali kuwa mumeo sio muaminifu na maumivu yakizidi na wewe tafta mtu akugongege kwa siri ili akufariji.

Hio ndio namna ya kupunguza machungu ila usiache kumuheshimu mumeo hata ukishaanza kuliwa maana ukiteleza hapo tu utapewa talaka kwa aibu na fedhea. Liwa nje ila usianze dharau na kejeli utakamatwa.
Vipi huu ushauri wako umezaa matunda? Au bado hajaleta feedback?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom