Ndoa inaelekea kunishinda

Ndoa inaelekea kunishinda

Sasa huyo jamani ni uchepukaji au ujinga, kama umeshakaa miaka naye kadhaa utakomaa, embu umeolewa na miaka yako 22-25 miezi 6 michepuko 3 umekomaa kweli hapo, ila simshauri aondoke ila kwa mwanaume afanyacho sio kabisa
Akiondoka ataenda wapi ambapo mume hachepuki? Wanaume huwa wanatulia tu Ila at some point katika ndoa lazima atoke tu! Sio wote Ila wengi ..
 
Ushauri wenu jamani,

Mimi nimeolewa nipo kwenye ndoa hatujamaliza hata mwaka Ila kinachoniumiza mme Wangu ananisaliti, nimemkuta anamiliki simu ya Siri pamoja na line alikuwa kaficha kabatini baada ya kugombana naye akakubali kuwa ana mchepuko akampigia akaweka loud nikawa nawasikia akamuomba samahani kwa kumchezea akamwambia Mimi nimeoa, nina mke nmeona siyo vizuri kumsaliti mke wangu dada akalalamika we badae akakubali kumblock kidogo nikapata amani.

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.

Msamaha kaniomba Ila nashindwa kumsamehe, naumia sana Bora ningemkamata hata na mmoja nisingeumia sana Ila wa 3 ukitegemea ndoa haina hata mwaka nawaza sijui kalogwa, natamani nimshirikishe hata mchungaji wetu Ila napata wakati mgumu naona ni vitu vya aibu hata kushirikisha watu wetu wa karibu.

Natamani niondoke Ila kinachonipa wakati mgumu tayari Mimi ni mjamzito yaani nawaza ingekuwa siyo hii mimba ningeachana nae ananifanya Hadi nakata tamaa na mimba niliyonayo kitu ambacho ni dhambi.

Naombeni mnishauri nifanyaje nahisi kuchanganyikiwa nakosa maamuzi presha imeshuka naona Kama dunia imeniangukia kweli ndoa ni ngumu sana duh! Mungu anitie tu nguvu.
KWani baada ya kuchepuka kapungua nini?wewe tulia lea mimba yako..hakuna mtu hachepuki duniani!
 
Na Mimi nawaza kitu Kama hicho niwe tu bize na maisha yangu na mwanangu aliye tumboni nafikiria kwanzia Leo nisishike simu yake Wala nisimfatilie akiamua kuchepuka achepuke. Maana nshaona nikijua naumia alafu ameshanikatisha tamaa coz ndokwanza tuna miezi 6 kwenye ndoa alafu namfuma na wanawake 3

Bora hata angekuwa mmoja ningesema labda kwakuwa na mimba ameona anitafutie msaidizi nafikiria hata siku akitaka nishiriki nae niwe tu Mimi natumia nae condom maisha yote kujiepusha na maradhi maana nimewasiliana na wadada wawili kati ya hao wanasema walikuwa hawatumii condom.

Mmoja ndo anasubiri kazi ya upolisi hivyo alimforce wakapime ukimwi kuhofia asijepata maambukizi akakosa kazi, yani hata hajali afya yangu na mtoto wake mpaka Kuna wakati inanijia roho ya kishetani nawaza sijui nimchomee hata ndani.

Jamani naumia Basi tu mpaka naona tena Kama huu ujauzito nlobeba ni mzigo kwangu maana mimba tu nayo inanitesa naumwa badala ya yeye kuwa faraja kwangu ndio kawa moto ananichoma
Pole Sana dear....usifadhaike Sana. Pengine kutokana na hali yako ya ujauzito ndio maana akatafuta pa kupumzikia. Ni mambo ya mpito.


Anyway...ananikumbusha mbali kipindi cha ujauzito wa wifey.....ila sijawahi kukamatwa. Ndio tulivyo, mtuzoee.
 
Mkuu unampea vya kutosha.

Mtoto akishiba nyumbani atapunguza kudoea kwa jirani.
 
Mume wako ila unabaki kusubiri siku akipatwa na maradhi, amefulia au amefariki; ndiyo mke wa ndoa unakumbukwa sasa. Siku hizi wanaume wanahamia kwa michepuko mazima; unaachwa ndani na pete yako na vyeti vya ndoa.

Yaani
Maisha ya ndoa yamekuwa kitanzi miaka hii


Wanawake wengi wapo kimaslahi akijua mwanaume Ana vimali vya kumsogezea maisha, akimpata ndo basi tena. Mwanaume anasahau nyumba na kila kitu anahamia kwa mchepuko.. wakati wa shida anamwacha anatafuta mwingine wa kumteka.
 
Wewe Mama na kushauri, kutulia tu huo ni mwanzo, na hilo sio kosa kubwa katika ndoa za siku hizi, popote utakapo enda utayakuta hayo, usaliti umekua officialised na watznia wengi,......kama huduma zingine anatoa tulia tu.
Uko sahihi
 
Wanawake hapo ndo mnapofeli, et unataman umshirikshe mchungaji wenu??? Huna wazaz, ndugu na jamaa?? Kuwa makin na hao wachungaj watakuomba buree!! Nao binadamu
Huyu mara nyingi atakuepo ni makanixa ya kilokole ambao akili zao wanashikiwa na wachungaji
 
Mmoja ndo anasubiri kazi ya upolisi hivyo alimforce wakapime ukimwi kuhofia asijepata maambukizi akakosa kazi, yani hata hajali afya yangu na mtoto wake mpaka Kuna wakati inanijia roho ya kishetani nawaza sijui nimchomee hata ndani.

Wet shit! Gone stone

Mkuu achana na hayo mawazo,,,Narudia tena achana na hayo mawazo kama unaipenda familia yako na huyo mwanao ambae yupo tumboni..

Mapenzi ni ugonjwa wa akili,,, Jitahidi tu kufanya mambo mengine achana na kufuatilia simu ya mpenzi wako.. Kama hajakukuta Bikira basi tulia tu...

Ukiona umechoka zaidi unaweza kuachana nae ukaendelea na maisha yako,,, Life does not stop for anybody.
 
Mmh wewe ndio kivuruge. Mwisho wa siku wenzio wakianza kupata magonjwa nyemelezi kinga zipo chini wewe uko zako pembeni unawacheka. Kucheat ndan ya ndoa ya miezi 6 haimpi credibility mwanaume aliye serious na ndoa, NEVER.

Kwanini uoe na huwezi tulia na mwanamke mmoja. Kuna bahat mbaya sawa lakini ndoa bado changa una wanawake watatu nje tayari
Nadhani haya yalikua makoloni yake hata kabla ya ndoa. Labda tumwambie bibie ampe mda atawaacha.
 
Forgive me - means i need help
You forgave me - doesnt mean i already trust you
 
Changanya na za kwako, maisha ya kuleteana stress wengine hatutaki,, au kwenu uliua,nenda kwenu,, atakuletea magonjwa bure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom