Mjeeeeeee,
Sehemu 2
Shangazi kanifukuza bila hata kuniulumia, hakujali kuwa nimebakwa na mumewe. Nilitoka pale huku nachechemea, sijasikia pakwenda, giza lilikuwa limeingia, nikatoka hadi stendi ya basi. Tulikuwa tunaishi Bunju, nikapanda gari hadi Ubungo ili nilale stendi asubuhi nipande gari za kwetu. Nilifika Ubungo vizuri huku nalia, nikiwa natembea kuelekea geti la kuingilia nikamsukuma mama mmoja, nilikuwa sijamuona, nilimsukuma kwa bahati mbaya. Yule mama alinirudishia alinisukuma kwa nguvu hadi nikadondoka chini. Nikamwambia, "Mama, mbona umenisukuma kiasi hiki?" Akaniambia tena, "Ukome unavyotembea, uwe unaangalia mbele, sio macho chini kama mwizi." Nikajiinua ili niondoke zangu. Wakati nanyanyuka, nilipoteza hela niliyopewa na shangazi kama nauli ya kwetu. Sikujua kama sina hela. Nilianza kupekua kila sehemu, lakini wapi. Nikaanza kulia pale tena kwa nguvu. Watu waliniuliza, "Nalia nini?" Niliwabia, "Nimepoteza nauli," ila hakuna aliyenijali.
Nilitoka pale stendi hadi maeneo yale. Niliondoka nikaanza kutafuta hela, lakini wapi. Nikatoka nikaanza kutembea, hata sijui naenda wapi. Nilifika mahali nikakaa chini huku nalia. Hapo sijakula chochote tangu asubuhi. Nikatamani nimpigie shangazi wa Arusha, lakini sikuwa na namba zao. Nilikaa pale hadi usiku mwingi ukaanza kuingia. Niliogopa nikasema hapa nitabakwa tena. Mamujee mm alipita dada mmoja amevaa vizuri tu. Nikamfata nikamsalimia vizuri, nikaanza kumuomba msaada. Nikamfata, "Naomba unisaidie japo pa kulala tu kwa siku hiyo." Yule dada aliniangalia juu mpaka chini, akaniambia, "Nitafute mtu mwingine, mimi sina msaada."
Yule dada alivyokuwa anatoa akaja kaka akaniuliza, "Binti vp? Mbona unaangaika usiku wote huu?" Nikamwambia, "Sina pa kwenda, nimetoka mkoani, nimekuja kufanya kazi za ndani. Sasa mtu niliyeambiwa atakuja kunipokea simuoni." Ilibidi nidanganye, kwani aliniangalia vizuri. Akaniambia, "Twende, nikakutafutie pa kulala, kesho nimtafute bosi wangu." Nikamfuata yule kaka, tulipanda basi hadi kwake. Tumefika kwake vizuri tukaingia ndani, alikuwa kapanga chumba na sebule. Akaniambia, "Nenda kaoge, mimi naenda kukutafutia chakula." Akanionyesha choo kilipo, nikavua nguo nikaenda kuoga. Nikavaa nguo zangu vizuri huku nina wasiwasi, sijui hatima yangu.
Kaka akarudi akabeba chips mbili na soda. Akanipa nikala, na yeye akaenda kuoga. Akaniuliza jina langu, nikamwambia naitwa Mamujee. Basi akaniambia, "Sasa ingia chumbani ulale." Niliogopa, nikasema hapana, nitalala hapa panatosha. Akaniambia, "Jee, noo, ingia chumbani ulale na mimi, nitalala hapa sebuleni." Nikanyanyuka japo kwa uoga, nikaingia chumbani. Wakati nashusha neti nilale, kaka akagonga mlango. Nikainuka kufungua huku natetemeka, akaniomba achukue shuka. Alivyotoka, nikafunga mlango kwa ndani, nikalala.
Asubuhi palivyokucha, nikaamka zangu. Nikatoka sebuleni, ila sikumkuta kaka. Nikaanza kufanya usafi ndani, kuanzia chumbani hadi sebule. Nikapanga kila kitu vizuri, nikaoga, nikachukua begi langu, nikakaa kwenye sofa nimsubiri kaka aje nimuage niondoke zangu. Kaka alikuja akaniita, "Jee vp, umeamka salama?" Nikajibu, "Ndiyo, shikamoo kaka." Aliitika vizuri, alibeba soda mbili na chapati. Akaniambia, "Jee, njoo tunywe chai." Mimi ni msera sina hata jiko. Tunaanza kula huku ananiuliza maswali, "Kwetu ni Musoma, sehemu gani?" Nikawa namjibu, "Vp kuhusu wazazi wako?" Nikamwambia, "Mimi ni yatima."
Kaka aliumia sana akaniambia, "Jee, kaa hapa na mimi, nitakutafutia nauli urudi nyumbani. Maana hata ukirudi pale Ubungo, nina uhakika uwezi kumpata huyo bosi wako. Zaidi tu utafanyiwa vitu vibaya, maana hii Dar es Salaam sio kabisa." Aliniuliza, "Nauli ya kwenu sh ngapi?" Nikamwambia. Akasema, "Nisubiri apate mshahara." Tulikaa pale huku tukiangalia TV. Ilikuwa sio siku ya kazi, kaka hakwenda kazini. Mchana ilipofika alitoka, alivyorudi, akarudi akabeba jiko la gesi, sefuria tatu na hotpot mbili, ila havikuwa vipya. Akaniambia, "Amechukua kwa rafiki yake, tutumie kwa muda hadi nikiondoka, hatamrudishia maana sio vizuri kula mgahawani." Nikainuka, nikaviosha vizuri. Akanielekeza magenge, akanipa hela, nikaenda kununua vitu vya kupika.
Nilinunua vitu vyangu nikarudi, nikaanza kupika. Nakumbuka nilipika pilau, nikaweka kwa hotpot ili tule hadi usiku. Kaka alifurahi akaniambia, "Jee, kumbe unajua kupika vizuri?" Basi, siku ikaisha. Kesho yake kaka alikuwa anaenda kazini, akamwita mpangaji mwenziwe, ni mdada. Akamwambia, "Huyu ni ndugu yangu anaitwa Mamujee, naomba ushinde nae vizuri." Kaka akaondoka zake, nikabaki na huyo jirani. Ilivyofika jioni, nikaanza kupika chakula ili kaka akija tule.