mwenzangu nilikuwa nawahi job sikusikiliza hadi mwishoni
Nimewapenda sana hawa wana ndoa kumbe hawakuwahi kulala pamoja kabla ya kuoana! ingekuwa ndoa za siku hizi hata wasingeoana manake lazima wangekaa kaa kwanza wakizini ndo waoane na ndipo wangeshtukiana mapemaaaa!
....duh, aisee....
Ngoja niusubirie ushuhuda wa 'wanaokoroma'...
Hahahaa. Sijakusikia umesemaje manake Paw anakoroma hapa. Khabari za masiku sheikh? Ulimisika sana.
Unatoa siri za mumeo?
ahahaaa ila kuna haja ya kupigana interview kabla ya ndoa aisee maana dah watu wanapretend jamaniKukoroma ni siri?
Mbona hata mimi nakoroma kama treni? Na anaekoroma anarekodiwa asubuhi tunasikiliza kabla ya morning glory. Yaani mtu anadakwa huku anacheka.
Ukicomplicate maisha hautayafurahia mdogo wangu. Maturity is the ability to laugh at yourself!
kama ndege wa mtu je?
ahahaaa never nitamsaliti baby wangu aisee hata iweje
Iaka mai.Asante kwa hotuba nzuri na ushuhuda mzuri.leo asubuhi nimeona ushuhuda mmoja toka emmanuel tv
huyu mama yupo 48 kwa sasa
alipatwa na tatizo la kukojoa kitandani since yupo miaka 10. kaishi na hilo tatizo kwa mateso mengi
sasa akaolewa mume wake alikuwa hajui kama mkewe ana tatizo la kukojoa kitandani kila siku!
duh siku ya kwanza kulala wote ndo aligundua kwamba mwenzake ndo hivo tena. ila sasa kwa maajabu kumbe na mwanaume nae alikuwa na tatizo so walijikuta wanaelea mto nile kitu kimedouble .huyu kamwaga yule kamwaga!
kwa hiyo wakaamua kuchukuliana hivo hivo na tatizo lao till 10 dec 2012 walipopata uponyaji kwa maombi ya tb joshua
KWELI MUNGU ANAJUA NANI NA NANI WAISHI PAMOJA
NAONA HUU ULIKUWA NI MPANGO WA MUNGU KWA WATU HAWA WAOANE .
KWA WALE AMBAO HAWANA WENZA TUSUBIRI WENZA WETU KUTOKA KWA BWANA
NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA!