Ndoa 300 huvunjika Dar kwa mwezi

Ndoa 300 huvunjika Dar kwa mwezi

Kumbe
 

Attachments

  • 187427409422963.jpg
    187427409422963.jpg
    104.5 KB · Views: 10
Solution ni kutunga sheria ukiachana na mmeo jera miaka 20 au kurudisha gharama za muhusika ulizokura piah ukifumwa na mke wa mtu jera miaka kumi au fine milioni 10 ukileta mdomo mdomo kwa mmeo jera miaka miwili
 
Serikali kuhamia Dodoma pia imesababisha ndoa nyingi za watumishi kuvunjika na zingine zikiwa katika umaututi wa kuvunjika
 
Dodoma.

Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeshtushwa na kasi ya kuvunjika kwa ndoa nchini chanzo kikubwa kikiwa ni kumomonyoka kwa maadili huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ndoa ni zaidi ya 300 zikivunjika kwa mwezi.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, leo Jumatatu Septemba 5, 2022 baada ya kukutana na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na makundi Maalum.

“Tumepata hesabu (ya ndoa kuvunjika) kwa mfano Dar es Salaam pekee yake zaidi ya ndoa 300 kwa mwezi zinavunjika. Hili tunaona ni tatizo kubwa ni janga. Sisi kama kamati tunaona haja kubwa ya kuishauri Serikali kuona jinsi gani kuchukua hatua kwa ajili ya kupambana na hali hii iliyopo,”amesema.

“Hili limeshamiri sana katika jamii yetu. Na kwakweli kuna haja ya Serikali kutafuta kwa kina chanzo nini na kuona ni hatua gani za kuchukua,” amesema.

Amesema watu wanaona ndoa kama ni jambo tu la kupita na kwamba watu wanaoana baada ya muda mfupi wanaachana.

Aidha, Nyongo amesema kuna ushauri ambao wameutoa kwa Serikali na utatolewa bungeni kuhusu mauaji yanayotokea baina ya wanandoa.

“Tumeona mmonyoko mkubwa wa maadili na ukatili mkubwa wa kijinsia hasa wa watoto ni mkubwa inahitaji Watanzania wajipange,”amesema.

Amesema ukatili umeongezeka unaoweza kusababishwa na vyanzo vingi ikiwemo ugumu wa maisha unaweza na kwamba Serikali ina jambo kubwa la kufanya kuondokana na hilo.

Amesema hilo ni tatizo kubwa na ni janga ambapo kamati imeona kuna haja ya kuishauri Serikali kuona jinsi ya kuchukua hatua maalum ya kupambana na hali iliyopo.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuliona hili na kuamua kuanzisha Wizara hii maalum, aliona kuna tatizo kubwa la ukatili, watu kuathirika kiakili na haya yote yapo kwenye jamii yetu,” amesema.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa wizara, Waziri wa wizara hiyo, Dk Dorothy Gwajima amesema katika kukabiliana na tatizo hilo vitendo vya ukatili katika jamii wizara yake imeendelea kuelimisha jamii ambapo baadhi ya wananchi wameelewa na kuhamasika kuhusu ukatili wa kijinsia na watoto.

Source:Mwananchi
 
Ninapozungumziaga mambo haya Kwa sababu ya akili yako ndogo hujui Taikon huwaga nazungumzia nini.

Wenzako tunaona katika angle ambayo wenye akili zenye matege hamuoni, tunaona miaka 10 ijayo wakati wewe hata kesho hujui nini kitatokea.

Hata hivyo sikulaumu
 
Do!.

Na bado hizo ni chache sana, kuna mada humu tume komenti, haya mambo ni lazima yatokee wababu yametabiliwa ilihali hata kizazi chenyewe hakisikii ya wakunga.

Kubadirika kwa mfumo wa maisha ni sehemu ya hizo vurugu ndani ya NDOA, mke anataka kuwa juu baba naye likewise.
 
Dunia imebadilika mno hivyo hayo hayaepukiki nyakati hizi, Sasa wanataka kuishauri serikali ichukue hatua gani?...maana ndoa ni makubaliano ya wawili tu.
 
Point ni zile zile tu
1. Maadili hayapo kabisa kwa sasa kwa asilimia kubwa tumeingia kweny uzungu na jamii za nje ambazo sio kawaida yetu

2.Elimu ya kukariri na kujua kingereza ilawaletea wanawake majivuno hata afike masters hamna kitu zaidi ya kukariri quotes za waandishi wa vitabu ...kuleta ujuaji mwingi kujifanya wapo kaangalie kule Instagram wapo wanawake wa kanda ile kujifanya wanajua sasa kutetea haki za wanawake behind hawana ndoa zimewashinda.

3.Stara hakuna kwa wanawake nimeenda mbeya juzi kati kule nimekuta wanwake wako tofauti kabisa wanajielewa wanavaa nguo za heshima sasa njoo hapa dar ujinga ni mwingi, na hata mwaka 2016 nilifika iringa wanawake wamevaa vizuri kabisa wanajielewa hapa dar ujinga mtupu..point yangu baadhi ya mavazi huleta ushawishi wa kutongozwa hata walioko maofisini wapo wanwake wanajiheshimu kwa imani zote hongera yao.

4.Baadhi ya wanaume tumekuwa ovyo usela wa kijinga mtu una familia lakini bado akili haipo sawa mambo ni mengi kila unayemuona unamtamani,fanya kazi zako kama kwenda bar nenda kwa kampani yako mambo ya marafiki unajikuta una kampani za ovyo mara ununulie watu bia huko bar..

5. Wanawake wamekuwa wapya kabisa bila ya hela hutoboi kabisa kwa vile anajifananisha na wengine matumizi ya ajabu mara nywele mara upumbavu gani cost ni nyingi kuhudumia, siku ukiyumba na ndoa hauna.

Hizo ni baadhi

Ushauri wangu kwa vijana wenzangu;
Hawa wanwake tunaokutana nao mkoa huu wenye mchanganyiko wa tabia tofauti na asili tofauti lazima tuwe makini katika kuchagua usibabaike ...kingine utoto tuache unaweza kuwa unavaa vizuri tu kulingana na kipato chako na kumuwezesha mpenzi wako nae apendeze ila ishu za kishamba ujiamini simama mwenyewe sio kampani za kijinga za marafiki.

Jambo la muhimu: Tukumbuke nasaba au asili zetu kuoa mtu unayetoka nae sehemu moja ni better kuliko kuokota huku town, nendeni vijijini na miji yenu mkaoe
 
Kuna mahali hizi takwimu zinapatikana mtandaoni?
 
Ndoa kama nyumba, ina msingi. Unapobomoa msingi tegemea majanga kwenye nyumba.
Bahati mbaya nyumba ikiangushwa huwa inaua kama kuna watu ndai au kujeruhi na mara chache sana walio ndani hutoka hai bila majeraha!
 
Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeshtushwa na kasi ya kuvunjika kwa ndoa nchini chanzo kikubwa kikiwa ni kumomonyoka kwa maadili huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ndoa ni zaidi ya 300 zikivunjika kwa mwezi.
  1. Kumomonyoka kwa maadili kunasingiziwa, chanzo cha kweli ni Mwigulu na wabunge wake
  2. Ndoa 300 ni wastani wa ndoa 10 kwa siku
 
Back
Top Bottom