Ndoa 300 huvunjika Dar kwa mwezi

kamba0719

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
804
1,904
Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, imeshtushwa na kasi ya kuvunjika kwa ndoa nchini chanzo kikubwa kikiwa ni kumomonyoka kwa maadili huku Mkoa wa Dar es Salaam pekee ndoa ni zaidi ya 300 zikivunjika kwa mwezi.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo, leo Jumatatu Septemba 5, 2022 baada ya kukutana na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na makundi Maalum.

“Tumepata hesabu (ya ndoa kuvunjika) kwa mfano Dar es Salaam pekee yake zaidi ya ndoa 300 kwa mwezi zinavunjika. Hili tunaona ni tatizo kubwa ni janga. Sisi kama kamati tunaona haja kubwa ya kuishauri Serikali kuona jinsi gani kuchukua hatua kwa ajili ya kupambana na hali hii iliyopo,”amesema.

“Hili limeshamiri sana katika jamii yetu. Na kwakweli kuna haja ya Serikali kutafuta kwa kina chanzo nini na kuona ni hatua gani za kuchukua,” amesema.

Amesema watu wanaona ndoa kama ni jambo tu la kupita na kwamba watu wanaoana baada ya muda mfupi wanaachana.

Aidha, Nyongo amesema kuna ushauri ambao wameutoa kwa Serikali na utatolewa bungeni kuhusu mauaji yanayotokea baina ya wanandoa.

“Tumeona mmonyoko mkubwa wa maadili na ukatili mkubwa wa kijinsia hasa wa watoto ni mkubwa inahitaji Watanzania wajipange,”amesema.

Amesema ukatili umeongezeka unaoweza kusababishwa na vyanzo vingi ikiwemo ugumu wa maisha unaweza na kwamba Serikali ina jambo kubwa la kufanya kuondokana na hilo.

Amesema hilo ni tatizo kubwa na ni janga ambapo kamati imeona kuna haja ya kuishauri Serikali kuona jinsi ya kuchukua hatua maalum ya kupambana na hali iliyopo.

Chanzo: Mwananchi.
 
Sababu ni zile zile....
1.Kula ujana kwenye ndoa,
2.uchawi mapenzini,
3.kukosa hofu ya Mungu,
4.past yenye maumivu ya kutendwa au kutenda,
5.kipato duni
6.ukosefu wa nguvu za kiume,
7.tamaa,
8.kiburi,
9.mdomo,
10.kutokuhudumia na kutokujitambua
Swadaktaaa
 
Jando na Unyago tumepiga teke. Shuleni tena mwendo wa kuwafundisha watoto wetu 50/50,haki sawa na usawa wa kijinsia.

Matokeo yake single parents wa kumwaga, watoto wanakuwa bila kupata malezi ya baba na mama, baadae inakuwa ngumu kumwambia mtoto umuhimu wa ndoa na familia.

Ndoa ndio msingi wa kila kitu,ndoa bora, hutengeneza jamii iliyo bora na taifa lenye ubora.
 
Jando na Unyago tumepiga teke. Shuleni tena mwendo wa kuwafundisha watoto wetu 50/50,haki sawa na usawa wa kijinsia.

Matokeo yake single parents wa kumwaga, watoto wanakuwa bila kupata malezi ya baba na mama, baadae inakuwa ngumu kumwambia mtoto umuhimu wa ndoa.

Ndoa ndio msingi wa kila kitu,ndoa bora, hutengeneza jamii iliyo bora na taifa lenye ubora.
Mkuu unatumia kinywaji gani
 
Wanaosema ndoa 300 zinavunjika wanasahau na zao zimo..halafu wanatafuta solution badala wao kwanza watafute solution kwa ndoa zao.
 
Back
Top Bottom