Ndo muda huo umetoka kazini

Aiseee. Hii inasisimua cute b.
Halafu mkwe kakataa kutoa mtoto hata mmoja akakae na bibi yake, au hata kumsalimia.

Huyo bibi akapigane kwenye folen za maji peke yake , sokoni peke yake. Huku Mtoto wake aliyemlelea kwa tabu, ananyumba nzuri na magari na house maids wawili.

Nilipata nafasi ya kuongea na huyo bibi nilisikitika sana, basi nimemgeuza kama mama yangu, na nimemzoea sana. Kila siku moja katika kula wiki napitia kumsalimia wakati mwingine napika tunakula nikirudi kwangu ni kulala tuu. Basi anafurahia sana.

Wanaume wana tabu hawa, ukizaa mtoto wa kiume mweke kwenye maombi sana. Maana anaweza asiweze kukutetea popote.
 
Hahahaha unakuta cute b mwenyew kimodo kidogo dogo mkwe ni bonge la mtu halafu unamkunja eti...haahaha mama kwa heshima alionae kwa mwanae anatulia tu
Hahaah ila huyu mama mkwe kiboko, inaonyesha hadi sasa hivi ukifanya kosa bado anakudunda.

Mimi ni kimodo kweli japo kupiga mtu pia siwezi, nilikuwaga namsulubisha mdogo wangu wa kiume. Siku zinavyozidi kwenda na yeye anakuwa mkubwa...alinipiga hiyo siku. Nilikoma!!!

Hata mama mkwe simpigi , acha yeye anipige hadi atosheke hata kama ananionea.
 
Halafu mkwe kakataa kutoa mtoto hata mmoja akakae na bibi yake, au hata kumsalimia.

Huyo bibi akapigane kwenye folen za maji peke yake , sokoni peke yake. Huku Mtoto wake aliyemlelea kwa tabu, ananyumba nzuri na magari na house maids wawili.

Nilipata nafasi ya kuongea na huyo bibi nilisikitika sana, basi nimemgeuza kama mama yangu, na nimemzoea sana. Kila siku moja katika kula wiki napitia kumsalimia wakati mwingine napika tunakula nikirudi kwangu ni kulala tuu. Basi anafurahia sana.

Wanaume wana tabu hawa, ukizaa mtoto wa kiume mweke kwenye maombi sana. Maana anaweza asiweze kukutetea popote.
Daah! Huyo bibi ni sawa na hajazaa tu hapo.

Na kweli mwaya kama usemavyo kikubwa kuwaeka kwenye kuwaombea tu.
 
Hahaah ila huyu mama mkwe kiboko, inaonyesha hadi sasa hivi ukifanya kosa bado anakudunda.

Mimi ni kimodo kweli japo kupiga mtu pia siwezi, nilikuwaga namsulubisha mdogo wangu wa kiume. Siku zinavyozidi kwenda na yeye anakuwa mkubwa...alinipiga hiyo siku. Nilikoma!!!

Hata mama mkwe simpigi , acha yeye anipige hadi atosheke hata kama ananionea.
Hahaha wewe ndio mzuri sasa....

Siku zako za kuwekwa ndani zinahesabika
 
Hahaah ila huyu mama mkwe kiboko, inaonyesha hadi sasa hivi ukifanya kosa bado anakudunda.

Mimi ni kimodo kweli japo kupiga mtu pia siwezi, nilikuwaga namsulubisha mdogo wangu wa kiume. Siku zinavyozidi kwenda na yeye anakuwa mkubwa...alinipiga hiyo siku. Nilikoma!!!

Hata mama mkwe simpigi , acha yeye anipige hadi atosheke hata kama ananionea.
Huyo mwanaume karogwa
 
Kabisaaa.

Japo ile 50/50 nayo inatuvuruga wanawake saa nyingine na kutufanya wengi tushindwe kujishusha ndani ya nyumba sasa ukikutana na mwanaume kaikubali ile basi tunakuwa juu zaidi ya juu yenyewe na mwisho wa siku haya ndio yanatokea.

Wanaodai 50/50 ni wale ambao hawana nidhamu wanataka wamkalie Mume asiseme chochote. Mwanaume akirudi saa 6 Usk na yeye aruhusiwe kurudi SAA 6, mwanaume akichepuka na yeye achepuke. Huwa ndiyo kitu tunachotazamiaga tukiongelea 50/50.

50/50 kikawaida hii ni misemo tuu Shadeeya .
Haitumiki kiuhalisia, kwa sababu mwanamke anadai 50/50 wakati huo hawezi kuua hata panya, panya akiingia ndani anasubiriwa Mume hadi arudi kazini aje aue.

Mke na mume wana kazi , lakini matumizi ya watoto , ada matibabu yanamwelemea mwanaume na mwanamke akitoa jua amemkopesha Mume na atamdai au achangie kiasi kidogo sana.

Kodi za meza hivyo hivyo, ujue hii 50 tunayoidaigi tunaitakaga ili tushindane na wanaume ila kiuhalisia tukisema tubadilishane majukumu ndani ya ndoa , sisi tuchukue ya mwanaume na wanaume yetu tutajuta.

Na mwanaume akiruhusu 50/50 lazima ageuzwe ndondocha. Atadundwa hadi mbele za marafiki zake.
 
Hahaaa. Huo ndio ukweli kikawaida mengi wafanyayo wanaume sisi hatuyawezi hata kidogo na huu ndio ukweli halisi.

Hivyo tuwaheshimugi tu.
 
Na uombe Mungu usiwe hivyo.
Haujawahi kuona mtu hadi mke wake anakuja na mwanaume nyumbani na analala naye hapo hapo? Unadhani huo ujasiri huwa unatoka wapi?

Naijua familia ambayo Mama ndiyo ana sauti. Ni tabu kwenye ile nyumba.
Kwanza mwanamke alipata ujauzito, akasema hataki kukaa na mama mkwe ni mchawi, badala ya mwanaume achukue hatua stahiki, alienda kumpangishia nyumba mama yake mtaani na ni bibi Mzee.

Guess what?? Huyo mwanaume akiwa mtaani ni kidume na ubabe sana. Akirudi nyumbani anapooza kama uji wa mgonjwa.
Daah..Kesho naenda church kwa nia na dhumuni la kuwaombea hao wanaume..

Mke anakuletea mwanaume ndani ya nyumba na wewe upo hapo??????...
Hii nimewahi kuiona bongo movie..Sema mwanaume alikuwa kipofu..
 
Kuumbe! Japo nawaza Mkuu, mwanamke wa hivyo hata Mume wake hashindwi mzaba kibao siku akimuudhi.

Kwa mimi rafiki kwanza naamini haliwezi kutokea kwenye maisha yangu. Cha kwanza siruhusu familia yangu kuja kukaa mda mrefu kwangu wala familia ya mke kuja kukaa kwangu mrefu.. Maana ibilisi ana maarifa katika kuleta fitina, unaweza kuta shetani kampitia mmoja wapo wakaanza maneno maneno, na tabia ya maneno ni kama moto huwaka na mwisho wa siku kukuta nyumba imewaka moto.. Nimeonge kiutu uzima na mafumbo
 
Wanaume wa hivyo wanapaswa kubadilika kwa kweli. Hatusemi kwamba wao ndio watupige sie hapana ila angalau waonyeshe uanaume wao hata kwenye kauli kidogo jamaani.

Na kama ikitokea, cha kwanza namchukua mke wangu na kwenda nae chumbani ( wife first ) tena kwa mahaba, naenda kummbebisha kwanza hadi akae sawa ( najua nikimuweka sawa, atafunguka kila kitu ) , ndio narudi kwa mama kumuomba msamaha wangu na kumuombea mke wangu ( haijalishi nani alikosea), sito thubutu kumuweka kikao mke wangu na mama yangu hadi nakufa, maana mama ni mzazi na sie ni watoto.. huwezi shindana hoja na mzazi wako
 
TUSIKURUPUKE.
Kwa picha ilivyo wewe umejenga mazingira ya mama kupigwa na mkeo. Mama hapo ni kama mtumishi (anavazi la jikoni) wa ndani. Lazima mke atakua na kiburi dhidi yake.
 
wadau wote mmezingua majibu yenu, mimi kama mwanaume chakwanza kabisa nauliza swali.. kwanini unampiga mama angu? wife akitoa maji vyongo hapo ndo tunabadilishana majengo ya serikali monchwari na jela
Sawa utauliza kwanza.
Sitegemei kama kutakua na jibu muafaka na sababu za kushibisha mke kumpiga mamake mzaa chema
 
Kwa mimi rafiki kwanza naamini haliwezi kutokea kwenye maisha yangu. Cha kwanza siruhusu familia yangu kuja kukaa mda mrefu kwangu wala familia ya mke kuja kukaa kwangu mrefu.. Maana ibilisi ana maarifa katika kuleta fitina, unaweza kuta shetani kampitia mmoja wapo wakaanza maneno maneno, na tabia ya maneno ni kama moto huwaka na mwisho wa siku kukuta nyumba imewaka moto.. Nimeonge kiutu uzima na mafumbo
Nimekuelewa sana rafiki. Na hii ndio dawa rafiki sababu siku zote watu wanapokaa sehemu moja kwa muda mrefu ni ngumu kuepusha mikwaruzano.
 
Na kama ikitokea, cha kwanza namchukua mke wangu na kwenda nae chumbani ( wife first ) tena kwa mahaba, naenda kummbebisha kwanza hadi akae sawa ( najua nikimuweka sawa, atafunguka kila kitu ) , ndio narudi kwa mama kumuomba msamaha wangu na kumuombea mke wangu ( haijalishi nani alikosea), sito thubutu kumuweka kikao mke wangu na mama yangu hadi nakufa, maana mama ni mzazi na sie ni watoto.. huwezi shindana hoja na mzazi wako
Ila rafiki umefunguka. Ama kweli utu uzima dawa.
 
Back
Top Bottom