Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Safi sana sistaaa hua naomba mungu sana nimpate mwanamke kama wewe vipi mae umeolewa??

Hapana sijaolewa ila pia nimeshavuka umri wa kuolewa kwa maana mie sasa ni mama wa makamo au mtu mzima. Wapo wadada bado ambao wanasifa kama uzihitajizo, nikutakie heri endelea kutafuta maana atafutaye hachoki akichoka keshapata.
 
Nani ana muda wa kudeal na mtu dunia hii ya leo?

Mtu anadili na kumbadilisha mtu...mtu kama anaamini kuna watu wanataka kumbadilisha atakua naive tu kudhani kuna watu wanataka mbadilisha for sure...no one has time for anyone
 
Hongera.

Kama uko hivyo haufati mkumbo kama vidada vya siku hizi unafaa.

Siku hizi wadada wanatisha sana siyo siri;

Ngozi bandia

Nywele bandia,

Kucha bandia,


Yani maisha ya siku hizi ni zaidi ya movie.


nyusi bandia. Matiti bandia. Kope bandia.

Na mbaya zaidi... 'chura' bandia.

Huwa nawaona kama midoli.

-Kaveli-
 
Hahahahahahaa stay tuned on 25th September 2016 please be our guest - church

Didn't know that that you were waiting for the invitation. As I was waiting for lens glasses inspection naked thing..... hehehehe

Missed you... alot!!

September 25, huh? It's a date then. And maybe right after, we'll get to that lens glasses thingy and what not.

The missment is mutual, mi'lady.
 
Hapana sijaolewa ila pia nimeshavuka umri wa kuolewa kwa maana mie sasa ni mama wa makamo au mtu mzima. Wapo wadada bado ambao wanasifa kama uzihitajizo, nikutakie heri endelea kutafuta maana atafutaye hachoki akichoka keshapata.


madam kasie, shikamoo. Mie nakupendaga sana mom.

Nina gift yako nitakuletea.

-Kaveli-
 
THE BIG DADA JF NZIMA SIJAONA ZAIDI YA KASINDE UMEONESHA KUJIAMINI UJUMBE UMEFIKA MAMA YANGU KALALE SASA KESHO UAMKE MAPEMA ILI UWAHI KAZINI

Weeh shika adabu vizuri mkononi......

Kasie halewi sifa kisha apelekeshwe....

Pole umekosea namba.
 
kwann usisemage tu we ni KASINDE kuliko kujikoshakosha kwa kizungu ati we ni KASIE...are u selling??
 
September 25, huh? It's a date then. And maybe right after, we'll get to that lens glasses thingy and what not.

The missment is mutual, mi'lady.
Yeah it's 25th Sept. get ready I hope no excuses, its a date.
So its may be.... and or may be not..... hahah if you cut me off on lens thing I will cry for sure and I don't know if you'll manage to stop me crying .

Thanks Sergio have my teddy bear hug...
Muah!!
 
hahahahahahah! yamekua hayo kasie

Ndio, unaleta janja ya Nyani kula mahindi mabichi heheheheh au panya kutafuna na kupuliza weeh waacha hiyooo nimekwisa jua hahahah.
 
Habari za jumapili,

Mmh iko hivi...

Kasie ana mazoea yake na kawaida zake sasa usifikiri hata siku moja utatoka huko ulikotoka ukambadilisha Kasie muonekano wake au haiba yake.

Duniani hatulingani hata kidogo kama ambavyo tumeumbwa kwa namna tofauti tofauti ndivyo ambavyo haiba na mionekano yetu haiwezi kufanana.

Yaweza kutokea mtindo wa kisasa wa nywele au nguo au mavazi au nakshi ambazo wewe ukaona ni swaga kwa mschana au mdada yeyote basi usilazimishe nami niwe kama hao. Mfano sasa hivi kuna mtindo wa nywele bandia za kutoka Brazil ambazo mdada au mschana akivaa hizo nywele huonekana kama zake na zina bei hadi laki 9 na watu wananunua. Aiseeh kama hizo swaga hazipandi akilini mwangu hatoniona nimetinga. Vivyo hivyo kwenye vitu vya urembo kama rangi za mwili rangi za kucha au rangi za mdomo na nyusi.
Wako walioniita mshamba bin wakuja bin wazamani wengine wakasema mie ni shkamoo jazz band.... sawa ila nafanya navaa na kupaka kitu kwenye mwili wangu ambacho nimeridhika nacho na kwa asilimia kubwa kama si 97 huwa naambiwa nimependeza kutoka majirani, kanisani, sokoni hadi kazini.

Imenilazimu kuandika haya baada ya kukutana na mdada leo kanisani yuko eeh Kasie mbona unajizeesha kuvaa haya magauni ya kutarizi ya kizee? Halafu nywele mbona hiyo ni mitindo ya zamani? Nikamsalimu nikaingia kwenue gari na kurudi nyumbani maana ibada ilikuwa imeisha na sikutaka kupoteza upako wangu wa jumapili maana nilihisi ninhefunua mdomo kumjibu ningemtukana halafu ingekuwa mbaya zaidi.

Mchana baada ya kupata mlo wa mchana nyumbani nikaenda zangu mahali kuna mambo flani nilikuwa nafatilia nikakutana na mkaka tulisomaga nae chuo yuko ooh Kasie za siku mingi na makumbato mengi na busu za gafla za mashavu za kurudia rudia.... baada ya muhtahsari wa salamu akaniambia you still look good... hahaha tukaagana kila mtu anaendelea na yake.

Yawezekana huyo mkaka alinisifia ile ya mwanaume kawaida kimsifia mwanamke hata kama hajapendeza walau kuonekana ameongea na huyo mdada.

Sina shida na hilo ila nimejikuta Kasinde nafanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu au watu wanione.

Nikifanya mazoezi ni kwa ajili ya afya yangu na mie niwe fit kwa jinsi ninavyojipenda na si kwasababu flani anione. Ukiniambia tutoke out usitarajie ntaenda kununua nguo na kwenda saluni kwa ajili unione niko vizuri, ntakuja mtanashati kama sikuzote nnavokuwaga mtanashati.

Nikienda saluni kutengeneza nywele au kucha ni kuwa muda wangu wa kwenda kusuka au kutengeneza kucha umefika. Nikinunua nguo ni kwasababu nimeipenda na ntaivaa kwenye tukio lolote litalotekea au hata siku ya kawaida.

Hivo wee bidada (yupo humu) wiki ijayo ukiniona kanisani uwe ushapata jibu la maswali yako.

Poleni kwa maelezo marefu, ndivyo nilivyo hehehe.

Kasie.
Hongera kwa moyo wa uvumilivu
Msichana mwingine akiambiwa hajapendeza hadharani anaweza kuleta timbwili la asha ngedere
 
hahahahaahaa..... uuuuwiiiiiii nikalale mie nikue mtoto wawatu
 
Back
Top Bottom