Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Hongera kwa moyo wa uvumilivu
Msichana mwingine akiambiwa hajapendeza hadharani anaweza kuleta timbwili la asha ngedere

Uzuri wake umri wa kufanya timbwili hadharani ushapita kwa Kasie.
 
Habari za jumapili,

Mmh iko hivi...

Kasie ana mazoea yake na kawaida zake sasa usifikiri hata siku moja utatoka huko ulikotoka ukambadilisha Kasie muonekano wake au haiba yake.

Duniani hatulingani hata kidogo kama ambavyo tumeumbwa kwa namna tofauti tofauti ndivyo ambavyo haiba na mionekano yetu haiwezi kufanana.

Yaweza kutokea mtindo wa kisasa wa nywele au nguo au mavazi au nakshi ambazo wewe ukaona ni swaga kwa mschana au mdada yeyote basi usilazimishe nami niwe kama hao. Mfano sasa hivi kuna mtindo wa nywele bandia za kutoka Brazil ambazo mdada au mschana akivaa hizo nywele huonekana kama zake na zina bei hadi laki 9 na watu wananunua. Aiseeh kama hizo swaga hazipandi akilini mwangu hatoniona nimetinga. Vivyo hivyo kwenye vitu vya urembo kama rangi za mwili rangi za kucha au rangi za mdomo na nyusi.
Wako walioniita mshamba bin wakuja bin wazamani wengine wakasema mie ni shkamoo jazz band.... sawa ila nafanya navaa na kupaka kitu kwenye mwili wangu ambacho nimeridhika nacho na kwa asilimia kubwa kama si 97 huwa naambiwa nimependeza kutoka majirani, kanisani, sokoni hadi kazini.

Imenilazimu kuandika haya baada ya kukutana na mdada leo kanisani yuko eeh Kasie mbona unajizeesha kuvaa haya magauni ya kutarizi ya kizee? Halafu nywele mbona hiyo ni mitindo ya zamani? Nikamsalimu nikaingia kwenue gari na kurudi nyumbani maana ibada ilikuwa imeisha na sikutaka kupoteza upako wangu wa jumapili maana nilihisi ninhefunua mdomo kumjibu ningemtukana halafu ingekuwa mbaya zaidi.

Mchana baada ya kupata mlo wa mchana nyumbani nikaenda zangu mahali kuna mambo flani nilikuwa nafatilia nikakutana na mkaka tulisomaga nae chuo yuko ooh Kasie za siku mingi na makumbato mengi na busu za gafla za mashavu za kurudia rudia.... baada ya muhtahsari wa salamu akaniambia you still look good... hahaha tukaagana kila mtu anaendelea na yake.

Yawezekana huyo mkaka alinisifia ile ya mwanaume kawaida kimsifia mwanamke hata kama hajapendeza walau kuonekana ameongea na huyo mdada.

Sina shida na hilo ila nimejikuta Kasinde nafanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu au watu wanione.

Nikifanya mazoezi ni kwa ajili ya afya yangu na mie niwe fit kwa jinsi ninavyojipenda na si kwasababu flani anione. Ukiniambia tutoke out usitarajie ntaenda kununua nguo na kwenda saluni kwa ajili unione niko vizuri, ntakuja mtanashati kama sikuzote nnavokuwaga mtanashati.

Nikienda saluni kutengeneza nywele au kucha ni kuwa muda wangu wa kwenda kusuka au kutengeneza kucha umefika. Nikinunua nguo ni kwasababu nimeipenda na ntaivaa kwenye tukio lolote litalotekea au hata siku ya kawaida.

Hivo wee bidada (yupo humu) wiki ijayo ukiniona kanisani uwe ushapata jibu la maswali yako.

Poleni kwa maelezo marefu, ndivyo nilivyo hehehe.

Kasie.
Sawa nakubaliana" Be yourself..! Lakini kapicha kuthibitisha haya kama kweli umependeza basii KASIE [emoji8] [emoji8]
 
cwez kuzimikia jina wakati hata sura sijaiona..na kwa mbwembwe zako, ww utakua boga tu c bure

Umejuaje... boga lilivyo zuri hivyo hehehehe kwa kizungu si ndo wanaita pumpkin or butter squash....? Heheheh maskini hata hujui kufananisha vizuri na vibaya looh hahahaha.
 
Hehehehe wenyewe wanasema shkamoo jazz band na mie naitikia woyooo basi ivyo ivyo tunasonga hahahah
Pole sana, ndio maisha. Utakuta wala hawana kitu cha maana ktk maisha watakachokuzidi, Wanaotoa maneno kama hayo pia wengi wao ni MAGORIKIPA huko makwao/wanasubiria kudaka tu
 
Yeah it's 25th Sept. get ready I hope no excuses, its a date.
So its may be.... and could be may be not..... hahah if you cut me off on lens thing I will cry for sure and I don't know if you'll manage to stop me crying .

Thanks Sergio have my teddy bear hug...
Muah!!

Excuses aren't my thing, left those to Mourinho.

And the only time I make a lady cry, it's outta joy. If you know whata mean.

Right back atcha with that love.
 
Sawa nakubaliana" Be yourself..! Lakini kapicha kuthibitisha haya kama kweli umependeza basii KASIE [emoji8] [emoji8]

Kama huamini nisemacho hata nikikwambia huyu ndo Kasie hutoamini, ukweli ndo huo.
Halafu naomba nikurekebishe.... kuwa asilia au kutokwenda na mitindo ya wakati haimaanishi kuwa ni mrembo au ni mzuri kupitiliza. Bali ni kuwa niko hivyo haka kama sura ikiwa kama marehemu Remmy Ongala. (May his soul rest in peace) nimetumia jina lake kwasababu wengi walimtumia kama mfano wa sura mbaya hata yeye mwenyewe.

Hivyo tofautisha uzuri na kuwa asili.
 
Pole sana, ndio maisha. Utakuta wala hawana kitu cha maana ktk maisha watakachokuzidi, Wanaotoa maneno kama hayo pia wengi wao ni MAGORIKIPA huko makwao/wanasubiria kudaka tu

Aaah mie nawapotezeaga tuu.....
 
Hapana sijaolewa ila pia nimeshavuka umri wa kuolewa kwa maana mie sasa ni mama wa makamo au mtu mzima. Wapo wadada bado ambao wanasifa kama uzihitajizo, nikutakie heri endelea kutafuta maana atafutaye hachoki akichoka keshapata.
Sidhani kama nitachoka kutafuta!!vipi mbona wewe umekata tamaa hivyo kwani mtu akifika bei huitaji??
 
Hongera.

Kama uko hivyo haufati mkumbo kama vidada vya siku hizi unafaa.

Siku hizi wadada wanatisha sana siyo siri;

Ngozi bandia

Nywele bandia,

Kucha bandia,


Yani maisha ya siku hizi ni zaidi ya movie.
Umesahau na tako bandia
 
Kama huamini nisemacho hata nikikwambia huyu ndo Kasie hutoamini, ukweli ndo huo.
Halafu naomba nikurekebishe.... kuwa asilia au kutokwenda na mitindo ya wakati haimaanishi kuwa ni mrembo au ni mzuri kupitiliza. Bali ni kuwa niko hivyo haka kama sura ikiwa kama marehemu Remmy Ongala. (May his soul rest in peace) nimetumia jina lake kwasababu wengi walimtumia kama mfano wa sura mbaya hata yeye mwenyewe.

Hivyo tofautisha uzuri na kuwa asili.
Mbona kama vile umepanic KASIE nimesema uko sawa ila nikaomba ulete kapicha ili tuprove kama kweli uko kiasili au u hv some modernities, sasa umeenda mbali mara mzuri au mbaya labda tambua issue ya uzuri ni relative unaye muona mbaya mwingine anamwona kisu..!

Mie humu kuna wadada hawalali na hawali ingawa nami kuna mdada ananirukish.a kichurachura..!
 
nitashangaa kama utakasirishwa na comment za watoto wa sekondari.

Najua wanafanya uchokozi wa kukera nawapotezea japo saa ingine wanaudhi na huwa napeperusha mbawa tuu na kuwaachia manyoya
 
Sidhani kama nitachoka kutafuta!!vipi mbona wewe umekata tamaa hivyo kwani mtu akifika bei huitaji??

Ingekuwa ni kufika bei ningeshaolewa siku mingi basi tuu nimeamua hivyo kama jinsi nilivyo niko hivyo. Na hii naisemaga sana humu ndivyo ilivyo.
 
Mbona kama vile umepanic KASIE nimesema uko sawa ila nikaomba ulete kapicha ili tuprove kama kweli uko kiasili au u hv some modernities, sasa umeenda mbali mara mzuri au mbaya labda tambua issue ya uzuri ni relative unaye muona mbaya mwingine anamwona kisu.
Mie humu kuna wadada hawalali na hawali ingawa nami kuna mdada ananirukish.a kichurachura..!

Hahahahahaa shida ya Kasie kuongea sana na kuweka muhtahsari siwezi.

Picha angalia avatar ikuze kisha iangalie kwa umakini huyo ndo Kasie.
 
Hahahahahaa shida ya Kasie kuongea sana na kuweka muhtahsari siwezi.

Picha angalia avatar ikuze kisha iangalie kwa umakini huyo ndo Kasie.
Mbona umenyoa manyusi sasa[emoji23] [emoji23] afu kama ndiyo wewe fanya uzae aisei umri umekutupa mkono si muda utaanza kutuma watoto wa wenzio..! Saida kaloli..! Kaisikii iweee deba wazea, ....wange o'takutuma kasikiwe o'wawe o'kanaga (wewe binti umezeeka... mtoto wangu usitume wakwako mimba ulitupa). [emoji41] [emoji41] kasie ujue Mungu anakuona eti hutaki kuolewa.
 
Usijali Kasie. Visichana vya sasa wala! They should never bother you. Stick to the fashions that please and suit you. Kwani bibi zetu hawakupendwa na babu zetu japo walikuwa hawana make up? Tupo wanaume wengi tu we admire original beauty from God
 
Mbona umenyoa manyusi sasa[emoji23] [emoji23] afu kama ndiyo wewe fanya uzae aisei umri umekutupa mkono si muda utaanza kutuma watoto wa wenzio..! Saida kaloli..! Kaisikii iweee deba wazea, ....wange o'takutuma kasikiwe o'wawe o'kanaga (wewe binti umezeeka... mtoto wangu usitume wakwako mimba ulitupa). [emoji41] [emoji41] kasie ujue Mungu anakuona eti hutaki
Mambo mengine huwa napuuzia tuu sio kila kitu ni cha kujibu.
 
Back
Top Bottom