Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Ndivyo nilivyo .... Niko hivo....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,240
Habari za jumapili,

Mmh iko hivi...

Kasie ana mazoea yake na kawaida zake sasa usifikiri hata siku moja utatoka huko ulikotoka ukambadilisha Kasie muonekano wake au haiba yake.

Duniani hatulingani hata kidogo kama ambavyo tumeumbwa kwa namna tofauti tofauti ndivyo ambavyo haiba na mionekano yetu haiwezi kufanana.

Yaweza kutokea mtindo wa kisasa wa nywele au nguo au mavazi au nakshi ambazo wewe ukaona ni swaga kwa mschana au mdada yeyote basi usilazimishe nami niwe kama hao. Mfano sasa hivi kuna mtindo wa nywele bandia za kutoka Brazil ambazo mdada au mschana akivaa hizo nywele huonekana kama zake na zina bei hadi laki 9 na watu wananunua. Aiseeh kama hizo swaga hazipandi akilini mwangu hatoniona nimetinga. Vivyo hivyo kwenye vitu vya urembo kama rangi za mwili rangi za kucha au rangi za mdomo na nyusi.
Wako walioniita mshamba bin wakuja bin wazamani wengine wakasema mie ni shkamoo jazz band.... sawa ila nafanya navaa na kupaka kitu kwenye mwili wangu ambacho nimeridhika nacho na kwa asilimia kubwa kama si 97 huwa naambiwa nimependeza kutoka majirani, kanisani, sokoni hadi kazini.

Imenilazimu kuandika haya baada ya kukutana na mdada leo kanisani yuko eeh Kasie mbona unajizeesha kuvaa haya magauni ya kutarizi ya kizee? Halafu nywele mbona hiyo ni mitindo ya zamani? Nikamsalimu nikaingia kwenue gari na kurudi nyumbani maana ibada ilikuwa imeisha na sikutaka kupoteza upako wangu wa jumapili maana nilihisi ninhefunua mdomo kumjibu ningemtukana halafu ingekuwa mbaya zaidi.

Mchana baada ya kupata mlo wa mchana nyumbani nikaenda zangu mahali kuna mambo flani nilikuwa nafatilia nikakutana na mkaka tulisomaga nae chuo yuko ooh Kasie za siku mingi na makumbato mengi na busu za gafla za mashavu za kurudia rudia.... baada ya muhtahsari wa salamu akaniambia you still look good... hahaha tukaagana kila mtu anaendelea na yake.

Yawezekana huyo mkaka alinisifia ile ya mwanaume kawaida kimsifia mwanamke hata kama hajapendeza walau kuonekana ameongea na huyo mdada.

Sina shida na hilo ila nimejikuta Kasinde nafanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu au watu wanione.

Nikifanya mazoezi ni kwa ajili ya afya yangu na mie niwe fit kwa jinsi ninavyojipenda na si kwasababu flani anione. Ukiniambia tutoke out usitarajie ntaenda kununua nguo na kwenda saluni kwa ajili unione niko vizuri, ntakuja mtanashati kama sikuzote nnavokuwaga mtanashati.

Nikienda saluni kutengeneza nywele au kucha ni kuwa muda wangu wa kwenda kusuka au kutengeneza kucha umefika. Nikinunua nguo ni kwasababu nimeipenda na ntaivaa kwenye tukio lolote litalotekea au hata siku ya kawaida.

Hivo wee bidada (yupo humu) wiki ijayo ukiniona kanisani uwe ushapata jibu la maswali yako.

Poleni kwa maelezo marefu, ndivyo nilivyo hehehe.

Kasie.
 
Kiukweli a real woman has to b like that. Mi naamini we ni mkamilifu without adding anything kwa mwilini wako k
 
Iko vizur sana nimekupenda japo skujiw,unafaaa kwa kila namna kuolewa nk, ktk maisha yng,ipo siku kama imepangwa.
 
Wanakera kweli watu wa ivyo!!! Unakuta mtu hakununulii ata pipi ya hamsini lakini kazi kukukosoa! Kila mtu na misimamo yake kimaisha... Ukifuata watu wanavyoishi hautasonga mbele. Achana nao Kassie...
YOU ARE THE BEST AT BEING YOU
 
ni vibaya kushauriwa maishani?
 
ni vibaya kushauriwa maishani?
Si vibaya! Ndo mana inaitwa ushauri... Unaweza ufuata au kutoufuata. Ukiwa na msimamo hutayumbishwa na maneno ya watu! Afu watu wengine wanakosa busara jinsi ya kushauri! Kama huyo dada kamkwaza mwenzake akati ametoka kanisani.
 
Habari za jumapili,

Mmh iko hivi...

Kasie ana mazoea yake na kawaida zake sasa usifikiri hata siku moja utatoka huko ulikotoka ukambadilisha Kasie muonekano wake au haiba yake.

Duniani hatulingani hata kidogo kama ambavyo tumeumbwa kwa namna tofauti tofauti ndivyo ambavyo haiba na mionekano yetu haiwezi kufanana.

Yaweza kutokea mtindo wa kisasa wa nywele au nguo au mavazi au nakshi ambazo wewe ukaona ni swaga kwa mschana au mdada yeyote basi usilazimishe nami niwe kama hao. Mfano sasa hivi kuna mtindo wa nywele bandia za kutoka Brazil ambazo mdada au mschana akivaa hizo nywele huonekana kama zake na zina bei hadi laki 9 na watu wananunua. Aiseeh kama hizo swaga hazipandi akilini mwangu hatoniona nimetinga. Vivyo hivyo kwenye vitu vya urembo kama rangi za mwili rangi za kucha au rangi za mdomo na nyusi.
Wako walioniita mshamba bin wakuja bin wazamani wengine wakasema mie ni shkamoo jazz band.... sawa ila nafanya navaa na kupaka kitu kwenye mwili wangu ambacho nimeridhika nacho na kwa asilimia kubwa kama si 97 huwa naambiwa nimependeza kutoka majirani, kanisani, sokoni hadi kazini.

Imenilazimu kuandika haya baada ya kukutana na mdada leo kanisani yuko eeh Kasie mbona unajizeesha kuvaa haya magauni ya kutarizi ya kizee? Halafu nywele mbona hiyo ni mitindo ya zamani? Nikamsalimu nikaingia kwenue gari na kurudi nyumbani maana ibada ilikuwa imeisha na sikutaka kupoteza upako wangu wa jumapili maana nilihisi ninhefunua mdomo kumjibu ningemtukana halafu ingekuwa mbaya zaidi.

Mchana baada ya kupata mlo wa mchana nyumbani nikaenda zangu mahali kuna mambo flani nilikuwa nafatilia nikakutana na mkaka tulisomaga nae chuo yuko ooh Kasie za siku mingi na makumbato mengi na busu za gafla za mashavu za kurudia rudia.... baada ya muhtahsari wa salamu akaniambia you still look good... hahaha tukaagana kila mtu anaendelea na yake.

Yawezekana huyo mkaka alinisifia ile ya mwanaume kawaida kimsifia mwanamke hata kama hajapendeza walau kuonekana ameongea na huyo mdada.

Sina shida na hilo ila nimejikuta Kasinde nafanya mambo kwa ajili yangu na si kwa ajili ya mtu au watu wanione.

Nikifanya mazoezi ni kwa ajili ya afya yangu na mie niwe fit kwa jinsi ninavyojipenda na si kwasababu flani anione. Ukiniambia tutoke out usitarajie ntaenda kununua nguo na kwenda saluni kwa ajili unione niko vizuri, ntakuja mtanashati kama sikuzote nnavokuwaga mtanashati.

Nikienda saluni kutengeneza nywele au kucha ni kuwa muda wangu wa kwenda kusuka au kutengeneza kucha umefika. Nikinunua nguo ni kwasababu nimeipenda na ntaivaa kwenye tukio lolote litalotekea au hata siku ya kawaida.

Hivo wee bidada (yupo humu) wiki ijayo ukiniona kanisani uwe ushapata jibu la maswali yako.

Poleni kwa maelezo marefu, ndivyo nilivyo hehehe.

Kasie.
Lazma ulishawah kuolewa ukaachika au hujaolewa at al, i trust my instings
 
Hilo neno baada ya au ndo sahihi. Sio siri sikuzote humu nimekuwa nikiweka wazi Kasie ni bibi ambaye anaishi mwenyewe kwa lugha ya kigeni wanaita single.

Was never am not and will not get married. Ni sababu zipi zimekupelekea uhisi hivyo unajua mwenyewe ila huo ndo ukweli.
 
Yeah, u said it right, be urself bana y ujiongezee makorokoro kibao mwilini while u have ur natural beauty from ur mom?

Naweza nisiwe mrembo ila huwa napenda vitu visivokolea sana hata chumvi na mafuta kwenye chakula viwe kidogoo.

Si kuwa sipaki kabisa rangi za mwili na mdomo na wanja hapana, ila kama nimepaka basi huwezi kujua au nikaishia kupaka mafuta tuu mwili wote (nnayotumia siku zote) nikaongeza wanja wa chini ya macho na lipshine nimemaliza bila kusahau manukato ya upole.
 
Hilo neno baada ya au ndo sahihi. Sio siri sikuzote humu nimekuwa nikiweka wazi Kasie ni bibi ambaye anaishi mwenyewe kwa lugha ya kigeni wanaita single.

Was never am not and will not get married. Ni sababu zipi zimekupelekea uhisi hivyo unajua mwenyewe ila huo ndo ukweli.
Thank you for being honest, you juc cementd trust kwa instings zangu...

Welcom a bottle of wine if u dont mind
 
Kiukweli a real woman has to b like that. Mi naamini we ni mkamilifu without adding anything kwa mwilini wako k

Asante japo yaweza kuwa nna mapungufu vile vile ni kuwa niko hivyo sana mahei hei kuta tangu kuleee ugeuke kutizama yule anayekuja ni nani.
 
Back
Top Bottom