SoC03 Ndio una haki ya kulalamika, lakini umetimiza wajibu wako kama binadamu?

Stories of Change - 2023 Competition

andree

New Member
Jul 14, 2023
1
1
Sote tunajua kuwa, kulalamika ni haki ya mtu yoyote pale ambapo anakuwa hajaridhika na jambo alilotendewa na upande wa pili. Hii husaidia kumjulisha mtendaji wa jambo hasi kujua kuaw, alilolifanya sio sahihi na lina athari kwa upande unaolalamika, na pia hutoa fursa kwa kosa lililofanyika kusahihishwa, ili lisiendelee kua mwiba kwa pande inayolalamika.

Lakini sote tunafahamu kua mioyo yetu hua inatu zomea pale unapokua unalalamikia jambo lisilo haki ulilotendewa, huku ukiwa na kumbukumbu kua nawe una hatia ya kutenda ubaya huo huo au baya linalolandana na hilo kwa mtu mwingine, tofauti tu ikiwa wewe hukupata nafasi ya kumsikia mlalamikaji moja kwa moja au kwa ukaidi au kwa kujiongopea kua hakuna muathirika wa uovu wako, au kwa nguvu na madaraka uliyonayo, ukajipa uhakika hakuna sauti ya malalamiko itakayotoka miongoni mwa waathirika.

Kwa kupima hayo yote, sote tunagundua kuwa, katika maisha yetu ya kila siku tuna feli mara nyingi kwa kutokujitazama sisi wenyewe pindi tunapokuwa tumekutana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kama, je, na sisi wenyewe si sehemu ya tatizo lilitukumba? Au je, hatuja changia katika utengenezwaji wa tatizo husika?

Katika kuyatazama yote hayo tutakuja kugundua kuwa, asilimia kubwa ya malalamiko tunayoyatoa, yanakuwa hayana tija ya moja kwa moja kwetu, kwa kuwa upande ambao tunao ulalamikia unajua fika kuwa, hata sisi wenyewe wenyewe walalamikaji tungefanya ubaya huo huo laiti tungekua katika nafasi ya juu yenye nguvu ya kutenda kosa husika. Na katika hali hii tumekua tukiendelea kujenga jamii isiyowajibika kwa tatizo lolote linapotokea zaidi ya kusukukumiana lawama bila kutafuta suluhisho na kinga ya tatizo husika.

Hoja yangu sio kwamba tukae kimya pindi tunapotendewa isivyo haki, bali sote tujitahidi kua sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii zetu, na kwa kufanya hivo , pindi linapojitokeza jambo lisi lofaa miongoni mwetu au katika jamii yetu, sote tutajisikia ku tuna uhalali wa kulipigia kelele bila kusita na haijalishi matokeo ya kelele zetu yatakua na tija kiasi gani, lengo letu la kumjulisha mkosaji wetu kua hatujafurahia tendo tulilotendewa litakua limetimia, na hivo tutakua tumetimiza wajibu wetu sote kama wanajamii. ASANTENI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom