Ndio kwanza nafika DAR-ES-SALAAM jana

Ndio kwanza nafika DAR-ES-SALAAM jana

uwesuporoto

Senior Member
Joined
Jun 2, 2017
Posts
116
Reaction score
58
Habari zenu viongozi.
Jamani mi nimefika jana dar je, nianzie wapi kutafuta ajira. Nina elimu ya darasa la saba na sina hata hiko cheti cha kumaliza shule. Msaada wenu tafadhali. Kwa anayeweza kuniambia pa kuanzia anielekeze niende pa kupiga kazi, kwangu kazi ni kazi. Akhsanteni
 
Nenda dampo pugu utakuta kazi tele huko
 
Ipo hapa kazi ya kuokota makopo,kg 1 nanunua kwa elf2,nitafute tuyajenge
 
Kuna kazi gani huko pugu na je malipo yake yanakuwaje? Mm nipo mbagala magari ya pugu unapandia wapi
Achana na habari za dampo.....Unaweza kulima? kuna mtu anahitaji mfanyakazi wa shamba,malipo ni Tsh.40,000 kwa hekari
 
Ipo hapa kazi ya kuokota makopo,kg 1 nanunua kwa elf2,nitafute tuyajenge
Tatizo la kuokota makopo ni kwamba mm dar ni mgeni naweza nikapotea kutokana na mitaa ya dar kuwa mingi ukilinganisha na kule kwetu
 
Bila shaka unatania.... 1kg ya chupa ni 250,kwa ofa hako unaweza nunua makopo yote TZ ndani ya siku moja tu.
 
Sitanii mkuu,nina biashara kama hiyo Morogoro,huko nanunua kwa shs.elf2.5/kg
 
Tatizo la kuokota makopo ni kwamba mm dar ni mgeni naweza nikapotea kutokana na mitaa ya dar kuwa mingi ukilinganisha na kule kwetu

Dar popote ulipo makopo yanapatikana,kama upo serious changamkia ofa hyo,mjini pagumu bila kazi
 
Nenda kariakoo kawachukulie wanaume wa DAR chaja, memory card, FLASH na Mp3 fake watanunua tu hasa katika foleni, mfano kule UBUNGO.
 
Back
Top Bottom