Ndesamburo na tamaa ya Madaraka....

Ndesamburo na tamaa ya Madaraka....

Personal attacks hizo!! Ndesa pesa hamtakaa mumuweze milele hata mpige kambi wote pamoja na mwenyekiti wenu.
 
Nasikia harufu ya mwigulu akiwa na gurunet mkononi tawanyikini fasta
 
Kwa mawazo ya kijinga kama haya kwa hawa vijana njaa ambao hata hawaoni maslahi ya Nchi kwanza ila kutumika tumika hovyo kumetufanya sisi kukaa kimya mno tunasoma tu maana we no longer have Great Thinkers hapa .Yaani mnasema Mbune Ndesa kuumwa .Kuna watu walianguka hata majukwaani na kuna watu wako kwenye ubunge muda mrefu zaidi ya Ndesa .Ndesa haibi pesa ya mtu na wala hatoi hongo nk .Leo unamuona mbaya ? Jadili umeme kupanda , gas kupanda nk .
 
Mbona umsemi anne makinda mbunge tangu mwaka 1976
 
Yule wakili atagmbea kama mbowe hata mfukuza yule aliye mgarahhaza lisu
 
Habari za Mchana wana Jf.

Taarifa za ndani zilizonifikia ni kwamba Mbunge wa Jimbo la Moshi Philemoni Ndesamburo (Chadema )ambaye amekuwa Mbunge kwa zaidi ya vipindi vitatu,kwa sasa anamchakato wa kurudi tena kwenye Jimbo hilo katika uchaguzI mkuu ujao.

Ndesamburo ambaye amekuwa akitumia muda mwingi kwa ajili ya kutibu afya yake nje ya nchi na kushindwa kuwatumikia wananchi na hata kuhudhuria vikao muhimu vya Bunge leo inasikitisha kuwa bado mzee huyo anataka kufia kwenye ubunge.

Ndesamburo anamiaka zaidi ya 80 kwa sasa na awali katika uchaguzi ulioisha mwaka 2010 alifanya kampeni zake kwa shida kutokana na afya yake,lakini alifanikiwa kupata viti vingi vya udiwani kwenye kata za manispaa ya moshi zaidi ya 17.

Tangu alivyoshinda uchaguzi mwaka 2010 alikuwa hajawahi kuonekana wala kufanya mikutano ya kisiasa,hadi mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwaka huu ambapo ameanza kutembelea kata zote kwa ajili ya kujiimarisha ili agombania tena jimbo hilo,ambapo hata kwenye mikutano amekuwa ak,ihutubia kwa shida,huku wakati mwingine akitaka kuanguka.

Hatua hiyo ya Ndesamburo kutaka kugombe imekuja baada ya mpango wa kutaka kumuweka mwanae Lucy Owenye kugombea Jimbo la Moshi kuona hatauzika na kumchafua kisiasa hivyo kuamua kugombea kwenye nafasi hiyo.
Kwa sasa kuna wanahabari ambao anawatumia kwa ajili ya kupita kwenye Kata ili kumfanyia utafiti kujua kama anakubalika kiasi gani ili aweze kugombea,na kuwapa kiasi kikubwa cha fedha.

Hali hiyo imefanya Chadema Mkoa na Manispaa ya Moshi kuendelea kukosa nguvu ya umoja,licha ya madiwani wengi kulazimika kukaa kimya kwa kuwa wanamtegemea mzee ndesamburo kama mfadhili wao mkubwa.

Tangu achaguliwe mzee ndesamburo amekwishahudhuria kikao kimoja tu cha baraza la madiwani ambacho amehudhuria januari mwaka huu huku vikao vingine muhimu ikiwemo ya bajeti akishindwa kuhudhuria kwa kuwa alikua Uingereza zaidi ya Mwaka kutibu maradhi yanayomsumbua.

Siandiki waraka huu kwa chuki ila nahitaji kujadili kwa hoja,sina chuki na Mzee ndesamburo,ila na ni rafiki yangu,muda wake wa kupumzika umefika awaachie vijana,kwani Meya wa Manispaa ya Moshi japhary Michael amekuwa kama ndio Mbunge wa Moshi kwa kulazimika kuchukua majukumu yake na maswali yanayotoka kwa wananchi kwani Ndesamburo amekuwa hatambua tena nafasi yake na kugeuka kama mfadhili.
Meya wa Moshi Japhary Naye alikuwa ameshatangaza kugombea nafasi hiyo ya Ubonge wa Moshi lakini kutokana na Mzee Ndesamburo bado anatamaa ya kubaki madarakani imebidi atangaze rasmi kujiondoa kwenye siasa ifikapo mwaka 2015.
Sipo upande wa Meya,kwa atakayesoma hapa ila nazungumzia uhalisia uliopo kwa Jimbo la Moshi ambapo kwa sasa Waandishi hao ndio wanamdanganya mzee ndesa kuwa utafiti waliofanya unaonesha kuwa unakubalika hivyo arudi kugombea.
Moshi ingekuwa na Mbunge ambaye ni mfuatiliaji ambaye angeweza kushirikiana na Meya wa Chadema,moshi ingekuwa na maendeleo makubwa tofauti na ilivyo sasa.

Katika kikao cha bajeti kila Mbunge alisimama na kuzungumza changamoto zilizopo kwenye Jimbo lao lakini kwa kudhihirisha kweli moshi haina Mbunge,sikuona hoja ya Mbunge wetu kuzungumzia hospitali ya Mkoa ya Mawenzi ambapo ni zaidi ya miaka mitatu kwa sasa haina chumba cha upasuaji na ipo JImbo la Moshi.

Kiukweli siyo kwamba wazee hawawezi ila inapofika wakati embu tuwapishe vijana wafanye kazi kwa kuwa muda ambao ndesa anatumia kwa ajili ya matibabu na kucheki afya nje ya nchi unazidi hata ule ambao angetakiwa kuwatumia wana wa Moshi,je ni vema tukaendelea na Mbunge wa namna hiyo kwa kuwa anafedha au akawepo kiongozi mchapakazi na mwenye uwezo wa kuwajibika kwa wananchi?

Mangi mkubwa;
kweli weye ni Mangi Mkubwa lakini wa wale wajinga wa mwisho kabisa. Fumbo mfumbie mjinga lakini si kwa mwerevu! Hiyo andika yenyewe tu. Unaonesha ni M ccm uliyejichokea na kupigika kimaisha vilivyo. Unayevizia namna ya kukinyemelea hicho kiti cha ubunge ukashindwa kabisa.
Moshi mjini, unayetaka kupambana na mzee Ndesa unajidanganya. Tena nakuambia, hata akitaka kumpitisha huyo mtoto wake Lucy uliyesema, kama mzee Ndesa atamsimamia atakupita mbali mnooo. Wala usipime weye.
Ati anaumwa, anakaa nje ya nchi kujitibu afya yake, umesikia ni fedha ya bunge imempeleka huko? Tafuta mbinu nyingine ya kulivuruga hilo jimbo si ----- huu. Meya Jafari hajakuambia anakitamani kiti hicho, wala huyo Lucy hajakutuma kuwa anakitamani kiti hicho.
Unasema ati mzee Ndesa ni rafiki yako, tueleze adui mmoja tu wa mzee Ndesa! Hata mama Minde ni rafiki wa mzee Ndesa weye urafiki wako ni wa kivipi? Mpaka unamfuatilia nyendo zake ati anajipitisha kwenye kata za jimbo lake, sijui ulitaka akae Dar ili upate cha kusema!
Cheap politics are not welcome here in Moshi. Peleka uji.nga wako hukoooooo
 
Kumbe kuhutubia na kutaka kuanguka kunakuondolea sifa ya kugombea, sasa wale wanaoanguka kabisa tuwaweke kundi gani?

Ndesamburo hali hiyo inamtokea si kwa bahati mbaya ni kutokana na umri wake pamoja na maradhi Lyimo
 
Mkuu hapa nipingane nawe,

Kugombea sio tamaa ya madaraka bali kung'ang'ania madaraka ndio tamaa.

Ndesamburo ni tofauti sana na viongozi wengine wa Chadema na kwa kifupi wananchi wanamuhitaji yeye kuliko hata yeye anavyohitaji huo ubunge.

Katika viongozi wote wa upinzani, huyu kwangu ni role model and it is my wish to be like him.

You can only dream about being like him kwa sababu katika umri wako wa miaka 40 plus, mzee Ndesa alikushakuwa mfanyabiashara mashuhuri Tanzania na hata nje ya Tanzania anayemiliki mali na rasilimali nyingi tu lakini wewe mpaka sasa unabeba mabox Uingereza na unaishi ghetto huku mkichangia rent. Poor you.....
 
Hizi ni siasa chafu na hila. Inaonekana ID hii imefunguliwa kwa lengo hili

Wananchi wa Moshi ndio wenye ridhaa ya kuamua ni nani awe mbunge wao na sio vinginevyo

Ndesamburo Kufanya siasa na kupita kila kata ni kazi yake kama Mbunge.Sijui kwanini ulalamike sasa hivi kwa mbunge kutekeleza wajibu wake

Kama alikua anaumwa kuna makosa gani akipita kwenye kata kusimamia wapiga kura wake?
images



Siyo siri, mzee Ndesa-Pesa is old, frail and tired!!
 
Kwa mawazo ya kijinga kama haya kwa hawa vijana njaa ambao hata hawaoni maslahi ya Nchi kwanza ila kutumika tumika hovyo kumetufanya sisi kukaa kimya mno tunasoma tu maana we no longer have Great Thinkers hapa .Yaani mnasema Mbune Ndesa kuumwa .Kuna watu walianguka hata majukwaani na kuna watu wako kwenye ubunge muda mrefu zaidi ya Ndesa .Ndesa haibi pesa ya mtu na wala hatoi hongo nk .Leo unamuona mbaya ? Jadili umeme kupanda , gas kupanda nk .

Utajadili umeme na gesi wakati wabunge tuliowachagua hawana muda wa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kisingizio cha afya zao.,lakini wakati wanakuja kuomba kura kwa wananchi wanasema wananguvu,tatizo linalotokea ni kwamba mimi ni mkazi wa Moshi na nimekuwa mkazi tangu Ndesmaburo amekuwa Mbunge hapa ila maendeleo nyie mnayazungumzia kwenye mitandao ya kijamii njooni kiuhalisia Moshi ndo usema amefanya nini au kama yeye yupo humu ajitokeze asema amefanya nini.
 
Sasa hapa ndio huwa nashindwa kuwaelewa, Chadema ni chama cha wachaga na Moshi ndio uchagani sasa ni kwa nini mnawaingilia wachaga?
Eti bwana , na hivyo viti ni vya ukoo!
Watu hawaelei elewi sera za CHADEMA , ukanda na kupokezana vijiti ndani ya familia!!!
4-IMG_2889.jpg


Tazma mwenyewe walivyofanana!!!!

Halafu mnataka kiti kiende Kigoma, mnawazimu nyie watu
 
Back
Top Bottom