Ndesamburo na tamaa ya Madaraka....

Ndesamburo na tamaa ya Madaraka....

Utajadili umeme na gesi wakati wabunge tuliowachagua hawana muda wa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kisingizio cha afya zao.,lakini wakati wanakuja kuomba kura kwa wananchi wanasema wananguvu,tatizo linalotokea ni kwamba mimi ni mkazi wa Moshi na nimekuwa mkazi tangu Ndesmaburo amekuwa Mbunge hapa ila maendeleo nyie mnayazungumzia kwenye mitandao ya kijamii njooni kiuhalisia Moshi ndo usema amefanya nini au kama yeye yupo humu ajitokeze asema amefanya nini.
Haya wanamoshi,changamoto hiyo.Kama kuna maendeleo yaliyopatikana wekeni vielelezo.
 
Mwenyekiti ndiyo kawafundisha mnategemea nini kwa wadogo.

chamamzigo + mizigo yake ni ving'ang'anizi wa kuiongoza hii nchi pamoja na kuwa nchi ilishawashinda kitambo tu yamebaki kuvimbiana tu kwa jasho la kodi yetu.
 
Maendeleo yapi wamepata moshi?

moshi ni mji wa 2 kwa usafi africa, barabara zmejengwa na znaendelea kujengwa,,shule zmejazwa walimu co sawa na zile za singida na simiyu, dawa mahosptalin zpo za kumwaga,, mji unakua kwa kias kikubwa sana,, na mengine meng.,,
 
Mimi ni mwanachama hai wa chadema kutoka moshi na kama hujui chama kilishapanga kabla hata ya uchaguz wa 2010 kua 2015 atagombea Mh. Japhary, sasa huu umbea wako dada mangi tafuta pengine pakuuongelea,,,
 
Mkuu hapa nipingane nawe,

Kugombea sio tamaa ya madaraka bali kung'ang'ania madaraka ndio tamaa.

Ndesamburo ni tofauti sana na viongozi wengine wa Chadema na kwa kifupi wananchi wanamuhitaji yeye kuliko hata yeye anavyohitaji huo ubunge.

Katika viongozi wote wa upinzani, huyu kwangu ni role model and it is my wish to be like him.

Duh! Ama kweli si wakati wote milembe nipa vichaa! wakati mwingine huwa wenye akili timamu huenda kutoa ushauri! hahahaa
 
Sasa wewe kinakuuma nini? Huo ni wivu wa kike mbona mama yako kamng'ang'ani yule hawara yake hadi uzeeni?
 
moshi ni mji wa 2 kwa usafi africa, barabara zmejengwa na znaendelea kujengwa,,shule zmejazwa walimu co sawa na zile za singida na simiyu, dawa mahosptalin zpo za kumwaga,, mji unakua kwa kias kikubwa sana,, na mengine meng.,,
Nashukuru ndugu yangu kwa majibu yako swali kidogo mji wa kwanza ni upi hizi data umezipata wapi.
 
You can only dream about being like him kwa sababu katika umri wako wa miaka 40 plus, mzee Ndesa alikushakuwa mfanyabiashara mashuhuri Tanzania na hata nje ya Tanzania anayemiliki mali na rasilimali nyingi tu lakini wewe mpaka sasa unabeba mabox Uingereza na unaishi ghetto huku mkichangia rent. Poor you.....
Kwa hiyo unanikataza nisiote ndoto?
 
Duh! Ama kweli si wakati wote milembe nipa vichaa! wakati mwingine huwa wenye akili timamu huenda kutoa ushauri! hahahaa
Mtoi ukae ukijua kuwa nakuheshimu sana na sikutegemea wewe na busara zako ukaita watu vichaa.

Anyway, kwenye ukweli uongo hujitenga, huyu mzee is another level. Mimi mwenyewe namkubali sana
 
Mkuu tofauti na Slaa,

Mzee Nadesa hana njaa wakati babu ni mchumia tumbo

lakini hana tabia kama ya kwako kula rambirambi za wajane,na ushauri bure bw lukos kaondoe mkono sweta huo pale kwenu iringa hospitar ya mkoa ukiling'oa hilo zawadi buku kumi mkuu.
 
Sasa wewe kinakuuma nini? Huo ni wivu wa kike mbona mama yako kamng'ang'ani yule hawara yake hadi uzeeni?

huyo ndo mzeeNDESSA PESSA mwenye uroho wa madaraka kupitiliza.hawezi kuachia ngazi kwa sababu chadema SACCOS AMEWEKEZA HISA ZAKE HUKO
 
Mara ya mwisho nnilihudhuria mkutano wake Kiborilon alihutubia kidog than hali yake ikaanza kuwa mbaya akastack ikabidi ashushwe jukwaani,kiukwel mzee amechoa apumzike.
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1390227027.656484.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1390227027.656484.jpg
    13.3 KB · Views: 70
Habari za Mchana wana Jf.

Taarifa za ndani zilizonifikia ni kwamba Mbunge wa Jimbo la Moshi Philemoni Ndesamburo (Chadema )ambaye amekuwa Mbunge kwa zaidi ya vipindi vitatu,kwa sasa anamchakato wa kurudi tena kwenye Jimbo hilo katika uchaguzI mkuu ujao.

Ndesamburo ambaye amekuwa akitumia muda mwingi kwa ajili ya kutibu afya yake nje ya nchi na kushindwa kuwatumikia wananchi na hata kuhudhuria vikao muhimu vya Bunge leo inasikitisha kuwa bado mzee huyo anataka kufia kwenye ubunge.

Ndesamburo anamiaka zaidi ya 80 kwa sasa na awali katika uchaguzi ulioisha mwaka 2010 alifanya kampeni zake kwa shida kutokana na afya yake,lakini alifanikiwa kupata viti vingi vya udiwani kwenye kata za manispaa ya moshi zaidi ya 17.

Tangu alivyoshinda uchaguzi mwaka 2010 alikuwa hajawahi kuonekana wala kufanya mikutano ya kisiasa,hadi mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwaka huu ambapo ameanza kutembelea kata zote kwa ajili ya kujiimarisha ili agombania tena jimbo hilo,ambapo hata kwenye mikutano amekuwa ak,ihutubia kwa shida,huku wakati mwingine akitaka kuanguka.

Hatua hiyo ya Ndesamburo kutaka kugombe imekuja baada ya mpango wa kutaka kumuweka mwanae Lucy Owenye kugombea Jimbo la Moshi kuona hatauzika na kumchafua kisiasa hivyo kuamua kugombea kwenye nafasi hiyo.
Kwa sasa kuna wanahabari ambao anawatumia kwa ajili ya kupita kwenye Kata ili kumfanyia utafiti kujua kama anakubalika kiasi gani ili aweze kugombea,na kuwapa kiasi kikubwa cha fedha.

Hali hiyo imefanya Chadema Mkoa na Manispaa ya Moshi kuendelea kukosa nguvu ya umoja,licha ya madiwani wengi kulazimika kukaa kimya kwa kuwa wanamtegemea mzee ndesamburo kama mfadhili wao mkubwa.

Tangu achaguliwe mzee ndesamburo amekwishahudhuria kikao kimoja tu cha baraza la madiwani ambacho amehudhuria januari mwaka huu huku vikao vingine muhimu ikiwemo ya bajeti akishindwa kuhudhuria kwa kuwa alikua Uingereza zaidi ya Mwaka kutibu maradhi yanayomsumbua.

Siandiki waraka huu kwa chuki ila nahitaji kujadili kwa hoja,sina chuki na Mzee ndesamburo,ila na ni rafiki yangu,muda wake wa kupumzika umefika awaachie vijana,kwani Meya wa Manispaa ya Moshi japhary Michael amekuwa kama ndio Mbunge wa Moshi kwa kulazimika kuchukua majukumu yake na maswali yanayotoka kwa wananchi kwani Ndesamburo amekuwa hatambua tena nafasi yake na kugeuka kama mfadhili.
Meya wa Moshi Japhary Naye alikuwa ameshatangaza kugombea nafasi hiyo ya Ubonge wa Moshi lakini kutokana na Mzee Ndesamburo bado anatamaa ya kubaki madarakani imebidi atangaze rasmi kujiondoa kwenye siasa ifikapo mwaka 2015.
Sipo upande wa Meya,kwa atakayesoma hapa ila nazungumzia uhalisia uliopo kwa Jimbo la Moshi ambapo kwa sasa Waandishi hao ndio wanamdanganya mzee ndesa kuwa utafiti waliofanya unaonesha kuwa unakubalika hivyo arudi kugombea.
Moshi ingekuwa na Mbunge ambaye ni mfuatiliaji ambaye angeweza kushirikiana na Meya wa Chadema,moshi ingekuwa na maendeleo makubwa tofauti na ilivyo sasa.

Katika kikao cha bajeti kila Mbunge alisimama na kuzungumza changamoto zilizopo kwenye Jimbo lao lakini kwa kudhihirisha kweli moshi haina Mbunge,sikuona hoja ya Mbunge wetu kuzungumzia hospitali ya Mkoa ya Mawenzi ambapo ni zaidi ya miaka mitatu kwa sasa haina chumba cha upasuaji na ipo JImbo la Moshi.

Kiukweli siyo kwamba wazee hawawezi ila inapofika wakati embu tuwapishe vijana wafanye kazi kwa kuwa muda ambao ndesa anatumia kwa ajili ya matibabu na kucheki afya nje ya nchi unazidi hata ule ambao angetakiwa kuwatumia wana wa Moshi,je ni vema tukaendelea na Mbunge wa namna hiyo kwa kuwa anafedha au akawepo kiongozi mchapakazi na mwenye uwezo wa kuwajibika kwa wananchi?
Haachii ng'o!! siye tumerithika na mwakilishi wetu!! nyie ni nani!!??
 
Ndesa Pesa,hapo nusura aanguke jukwaani,kwel amechoka apumzike tu.
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1390229587.273675.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1390229587.273675.jpg
    96.1 KB · Views: 50
Mi naona kama ni tamaa ya madaraka kwani hata Nyerere alipoacha kugombea uongozi bado wananchi wanamuhitaji na alikuwa na uwezo wa kuwatumikia wananchi tofauti na Ndesamburo ambaye anataka afie kwenye Ubunge.

Hebu weka na data hapa kabisa tangia uchaguzi uliopita wabunge wa ngapi wa CCM wamekufa wakiwa wabunge;

Twende

1. Dr. Mgimwa
2.
3.

Sasa unamshangaa nini Mzee Ndesa? Kama hamna cha kusema bora mkae kimya.

Tiba
 
Hizi ni siasa chafu na hila. Inaonekana ID hii imefunguliwa kwa lengo hili

Wananchi wa Moshi ndio wenye ridhaa ya kuamua ni nani awe mbunge wao na sio vinginevyo

Ndesamburo Kufanya siasa na kupita kila kata ni kazi yake kama Mbunge.Sijui kwanini ulalamike sasa hivi kwa mbunge kutekeleza wajibu wake

Kama alikua anaumwa kuna makosa gani akipita kwenye kata kusimamia wapiga kura wake?

Ben kwa nini mtu akikosoa na kusema ukweli mnasema ni siasa chafu,je wew ni mwananchi wa moshi na je umezungumza nao ukagundua kuwa ni uongo nimeandika hapa?

Mimi niliyeandika hapa ni mkazi wa moshi na nina uchungu na kura yangu niliyompa Ndesmaburo mwaka 2010 lakini sijaona maendeleo ambayo ameniletea,hata kwenye kikao cha baraza tangu achaguliwe ndo amehudhuria mwaka 2014,sembuse vikao vya bunge ambavyo sijaona akizungumzia hoja za wana moshi.

Sina ugomvi na yeye kuzunguka kwenye kata na kuzungumza na wananchi wake,lakini tangu achaguliwe alikuwa hawajawahi hata kufanya mkutano kwenye kata hata moja na kuwashukuru wananchi wake,licha ya wananchi kuwachagua kwa wingi madiwani wa chadema sasa wew nashangaa kushikilia hoja ya kwamba ni haki yake kufanya mikutano hakuna ambaye amsema kuwa asifanye mikutano.

Hata mimi pia nazungumza kama mmoja wa wananchi wa moshi,lakini kama kweli anauwezo wa kuendelea kuwakilisha wananchi wa moshi afanye hivyo akitambua kuwa anauwezo wa kuweza kuwatumikia wanan moshi siyo kwa kuwa anauwezo wa kushawishi wapiga kura kwa fedha alizonazo mwisho jimbo linabaki kama lina Mbunge wa CCM.
 
Back
Top Bottom