Ben kwa nini mtu akikosoa na kusema ukweli mnasema ni siasa chafu,je wew ni mwananchi wa moshi na je umezungumza nao ukagundua kuwa ni uongo nimeandika hapa?
Mimi niliyeandika hapa ni mkazi wa moshi na nina uchungu na kura yangu niliyompa Ndesmaburo mwaka 2010 lakini sijaona maendeleo ambayo ameniletea,hata kwenye kikao cha baraza tangu achaguliwe ndo amehudhuria mwaka 2014,sembuse vikao vya bunge ambavyo sijaona akizungumzia hoja za wana moshi.
Sina ugomvi na yeye kuzunguka kwenye kata na kuzungumza na wananchi wake,lakini tangu achaguliwe alikuwa hawajawahi hata kufanya mkutano kwenye kata hata moja na kuwashukuru wananchi wake,licha ya wananchi kuwachagua kwa wingi madiwani wa chadema sasa wew nashangaa kushikilia hoja ya kwamba ni haki yake kufanya mikutano hakuna ambaye amsema kuwa asifanye mikutano.
Hata mimi pia nazungumza kama mmoja wa wananchi wa moshi,lakini kama kweli anauwezo wa kuendelea kuwakilisha wananchi wa moshi afanye hivyo akitambua kuwa anauwezo wa kuweza kuwatumikia wanan moshi siyo kwa kuwa anauwezo wa kushawishi wapiga kura kwa fedha alizonazo mwisho jimbo linabaki kama lina Mbunge wa CCM.