Ndege zisizo na rubani kusambaza dawa nchini

Ndege zisizo na rubani kusambaza dawa nchini

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,309
Dar es Salaam. Serikali, Bohari ya Dawa (MSD) kwa kushirikiana na kampuni ya Zipline kutoka nchini Marekani wamesaini mkataba wa makubaliano ya kusambaza dawa kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani 'drones'.

Tukio hilo lililofanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya waliohusika katika utafiti uliochukua miaka mitatu wakiwemo Ifakara Health Institute (IHI).

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Lauren Bwanakunu amesema makubaliano hayo yataanza rasmi mara moja kuangalia namna ya kuanza kutumia teknolojia hiyo.

"Wenzetu wa Ifakara watafanya utafiti kuangalia uwezekano wa drones kufanya kazi Dodoma na Mwanza wakipata matokeo chanya tutaanza kusambaza dawa kwa kutumia Ndege hizi," amesema Bwanakunu.


Chanzo: Mwananchi
 
Hii wadau imekaa vipi ? hakuta kuwa na muingiliano na watu wa tanzania civil aviation katika matumizi ya anga na je kwa ndugu zangu wafugaji watakuwa wanaelewa nini kinapita kwao je kuna elim yoyote kwao ?..
 
Kwanini watumie drone? Lisipofika sehemu husika itakuwaje ? Wakulima wakilipiga manati huko porini.
 
waache watumie tu hizo drone

huku mtaani watazipoa kwa mawe wauze screper maana hali tete
 
WAzo zuri nliona documentary CNN wakielezea namna Rwanda inavyotumia drone kusambaza damu.ITasaidia sana,kupopolewa mawe sio rahis labda uipopoe inapotaka kupaa,coz haitui kwenye destination yake ukifika eneo husika ikiwa bado angan inaachia package then inarudi kule ilikotoka.
 
WAzo zuri nliona documentary CNN wakielezea namna Rwanda inavyotumia drone kusambaza damu.ITasaidia sana,kupopolewa mawe sio rahis labda uipopoe inapotaka kupaa,coz haitui kwenye destination yake ukifika eneo husika ikiwa bado angan inaachia package then inarudi kule ilikotoka.
Duuh kwa Bongo hapa. Inaweza ikaachia juu ya paa la nyumba yangu.
Isiwe damu. Iwe dawa. Itakuwa burdani.
 
Au wakizifungua dawa na kuzinywa...
kwa mujibu WA documentary ya CNN ya zipline Rwanda drone zinapeleka dawa sehem husika Na wanatumia GPS,drone haiwezi kukosea labda aliyeingiza coordinates akosee,pia wapokeaji wanapewa muda ambao drone itaachia mzigo kutoka angan so wanakua standby kuupokea.Pia kwa umbali inaopita Ni ngumu Sana kupopolewa mawe labda wakati WA kutua Na kupaa Kama nlivosema mwanzo kuwa kule inakipoleka mzigo haitui Ina udondosha then inageuka kurud kwenye station yake.
 
Back
Top Bottom