Ndege ya Shirika la Precision Air iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma yalazimika kutua kwa dharura

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Shirika la Ndege la Precision Air limethibitisha kuwa ndege zake mbili zimeshindwa kufanya safari zake kama kawaida baada ya ndege moja kupata hitilafu na nyingine kulazimika kutua kwa dharura. Precision Air imethibitisha hilo kupitia Taarifa yake leo Februari 03, 2023 ikibainisha kuwa, moja ya ndege zake ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa safari.

Shirika hilo limesema kuwa, ndege nyingine ya Precision Air ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugonga kiumbe aina ya ndege kama kunguru au njiwa wakati ikiruka kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu pamoja na umma kwa jumla kwamba moja ya ndege zetu imepata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa baadhi ya safari zetu.” imesema Taarifa hiyo ya Precision Air

"Katika tukio lingine, ndege yetu yenye usajili namba 5H-PWD ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugongana na ndege. (kama njiwa au kunguru) wakati ikiruka kuelekea Dodoma ikitokea Dar es Salaam.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza, tunafanya jitihada za dhati kurejesha safari zetu katika hali ya kawaida."
Imeongeza.

Matukio hayo yanajitokeza ikiwa ni miezi kadhaa tangu ilipotokea ajali mbaya ya ndege ya Presicion Air mwezi Novemba mwaka jana ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19.
A71F0894-CD21-4CDF-B051-BFFA4B492314.jpeg
 
Magufuli alisababisha haya yote kwa kuwafukuza fast jet ili madege yake yatawale anga la Tanganyika
 
Shirika la Ndege la Precision Air limethibitisha kuwa ndege zake mbili zimeshindwa kufanya safari zake kama kawaida baada ya ndege moja kupata hitilafu na nyingine kulazimika kutua kwa dharura. Precision Air imethibitisha hilo kupitia Taarifa yake leo Februari 03, 2023 ikibainisha kuwa, moja ya ndege zake ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa safari.

Shirika hilo limesema kuwa, ndege nyingine ya Precision Air ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugonga kiumbe aina ya ndege kama kunguru au njiwa wakati ikiruka kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu pamoja na umma kwa jumla kwamba moja ya ndege zetu imepata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa baadhi ya safari zetu.” imesema Taarifa hiyo ya Precision Air

"Katika tukio lingine, ndege yetu yenye usajili namba 5H-PWD ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugongana na ndege. (kama njiwa au kunguru) wakati ikiruka kuelekea Dodoma ikitokea Dar es Salaam.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza, tunafanya jitihada za dhati kurejesha safari zetu katika hali ya kawaida."
Imeongeza.

Matukio hayo yanajitokeza ikiwa ni miezi kadhaa tangu ilipotokea ajali mbaya ya ndege ya Presicion Air mwezi Novemba mwaka jana ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19.
Naiomba serikali isaidie hili shirika kuchunguza kama wapo wanaolihujumu
 
hadenge ya openpangaboy ni shida😂😂😂 yani kunguru tu kasababishia ndege dharura
 
Mpaka wazimalize ndo watatosheka, afrika mama africa.
 
Shirika la Ndege la Precision Air limethibitisha kuwa ndege zake mbili zimeshindwa kufanya safari zake kama kawaida baada ya ndege moja kupata hitilafu na nyingine kulazimika kutua kwa dharura. Precision Air imethibitisha hilo kupitia Taarifa yake leo Februari 03, 2023 ikibainisha kuwa, moja ya ndege zake ilipata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa safari.

Shirika hilo limesema kuwa, ndege nyingine ya Precision Air ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugonga kiumbe aina ya ndege kama kunguru au njiwa wakati ikiruka kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

Tunapenda kuwataarifu wateja wetu pamoja na umma kwa jumla kwamba moja ya ndege zetu imepata hitilafu ya kiufundi hivyo kusababisha kuchelewa na kuahirishwa kwa baadhi ya safari zetu.” imesema Taarifa hiyo ya Precision Air

"Katika tukio lingine, ndege yetu yenye usajili namba 5H-PWD ililazimika kutua kwa dharura baada ya kugongana na ndege. (kama njiwa au kunguru) wakati ikiruka kuelekea Dodoma ikitokea Dar es Salaam.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza, tunafanya jitihada za dhati kurejesha safari zetu katika hali ya kawaida."
Imeongeza.

Matukio hayo yanajitokeza ikiwa ni miezi kadhaa tangu ilipotokea ajali mbaya ya ndege ya Presicion Air mwezi Novemba mwaka jana ilipokuwa ikitua katika Uwanja wa Bukoba mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 19.
Aisee!
 
Back
Top Bottom