Ndege ya ATCL yapelekwa Visiwa vya Malta kwa ajili ya matengenezo

Siku hizi uchakavu wa madude ya serikali unaletwa na Tagaz hapa JF kweli jamaa kaenda
 
Kanchi kenye wakazi 500,000 kametuzidi akili wenye wakazi milioni 60? Mpaka gereji zao ndo tunapeleka ndege kumwaga oil?
Lazima tuzidiwe wewe mwenyewe umekaa kulalamika tu humu huna kitu chochote ulichoifanyia nchi hii unasubiri watu wengine wakufanyie.
 
Mbona utaratibu wa kawaida huu, labda uwe na akili kama za ACT au CDM ndio utashangaa
 
Taarifa rasmi iliyotolewa leo Mei 17, 2021 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa Ndege 1 ya Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) imepelekwa nchini Malta kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo

Taarifa zaidi kutolewa

MCL
Wakati inaondoka ilikaguliwa?
 
Ni swali hata Mimi nimejiuliza... Au upigaji umeanza? Tena Malta ka nchi kadogo...
Na nyie watu hadi mnaboa kwani lini hii nchi upigaji ulikwisha, akiwepo mwenda zake tu licha ya kujisifu walikuwa wanapiga tu!!mfano huko ATCL, walipiga bilioni mbili za matengenezo ya ndege, wakati ndege ilishakufa toka 2015!!kulingana na ripoti ya CAG!!kwani gari linapolekwa service huwa linaenda vipi?!!kuhusu kisiwa cha malta kuwa ni kudogo haina mashiko, kwani hayo makampuni yanayotengeneza hizo ndege, yanaamua wapi waweke kituo chao cha kufanyia service.
 
Taarifa rasmi iliyotolewa leo Mei 17, 2021 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa Ndege 1 ya Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) imepelekwa nchini Malta kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo

Taarifa zaidi kutolewa

MCL
Mbona enzi za Mwendazake ndege tulikua tukizipiga rangi wenyewe, leo hii matengenezo tu zinapelekwa Malta kwenye kainchi kadogo hata wakazi wake hawafiki million moja!
 
Ina maana sisi hatuwezi kutengeneza
Swali zuri mkuu KWA Sasa ndege zinaendelea ongezeka au zimeongezeka , lazima kuwa na mawazo mapana Sasa
Serikali lazima kuwekeza kwenye karakana ya matengenezo ya ndege kwamba KWA kuanzia tunaweza ajujiri wataalam TOKA nje wenye ujuzi zaidi ambao watakaa na watanzania wenzetu wenye uwezo katika fan husika ili kupata uzoefu zaidi,itasaidia jenga shirika imara na kupunguza gharama
 
Taarifa rasmi iliyotolewa leo Mei 17, 2021 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa Ndege 1 ya Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) imepelekwa nchini Malta kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo

Taarifa zaidi kutolewa

MCL
Tutapigwa sana mpaka ATCL ife kifo cha pili tutakuwa tuna adabu njema.
 
Back
Top Bottom