Ndege ya ATCL yapelekwa Visiwa vya Malta kwa ajili ya matengenezo

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,010
2,000
Taarifa rasmi iliyotolewa leo Mei 17, 2021 na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa Ndege 1 ya Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) imepelekwa nchini Malta kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.

Taarifa zaidi kutolewa.

====

Ndege ya ATCL yapelekwa Malta kutengenezwa​


Dodoma. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanzania, Dk Leonard Chamuriho amesema kndege ya Shirika la Ndege Nchini ( ATCL) aina ya Dash 8 Q300 iliyokuwa mbovu tangu mwaka 2016 imepelekwa nchini Malta kufanyiwa matengenezo makubwa.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2021/2022 leo Jumatatu Mei 17 2021, Dk Chamuriho amesema matengenezo hayo yanatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu na hivyo kuifanya ATCL kuwa na jumla ya ndege 12.

“Kukamilika kwa matengenezo ya ndege hii kutaongeza wigo wa utoaji huduma zenye tija hata katika viwanja vyenye abiria kati ya 30 hadi 50,”amesema.

Aidha, Dk Chamuriho amesema Serikali inatambua juu ya uwepo wa gharama kubwa za uendeshaji za ATCL na hivyo kusababisha hasara isiyo ya lazima.

Amesema Serikali imechukua hatua ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Amezitaja hatua hizo ni kuwa ni pamoja na kulitafutia ufumbuzi deni lililorithiwa na ATCL iliyofufuliwa, ili litoke katika vitabu vya hesabu.
Waziri Huyo amesema uwepo wa deni hilo umechangia katika kuongeza gharama za uendeshaji.

Amesema hatua nyingine ni kufanya mapitio ya Mkataba wa Ukodishaji Ndege kati ya ATCL na Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) ili kuiongezea ATCL nguvu ya ushindani.

Dk Chamuriho amesema maboresho hayo hayatagusa maeneo yanayohusu uwezo wa kufanyia matengenezo ndege zilizonunuliwa.
Aidha, amesema Serikali imeendelea kuisadia ATCL kuongeza mapato nje ya ubebaji wa abiria na mizigo kwa kuipa uendeshaji wa kumbi za kupumzikia wageni (lounges) katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA).

Pia amesema Serikali imeijenga uwezo ATCL wa kutoa huduma kwa ndege na abiria katika viwanja vya ndege.

Chanzo: Mwananchi
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,502
2,000
Ndiyo uwazi wa awamu ya sita, tofauti na awamu ile . Kazi iendelee ktk namna Mpya.


Mega Pit Stops - Episode 1: Airplane Heavy Maintenance - Airbus A330-300 At Lufthansa Technik Malta, 700 hidden figures keep aviation the safest way to travel. The highly trained team specializes in aircraft safety checks and overhauls. They inspect and repair fleets from airlines around the world
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom