Ndege Njiwa amejenga pembeni ya nyumba yangu!

Mmmh hivi kweli umekua? Mbona km bado enzi zako za kuwinda hujaacha
ni kwasababu tu nakaa mjini huku, nikirudi village nafasi ikipatikana nawinda kama kawaida mkuu. mtu hawezi kuacha asili yake.
 
Hawa ndege wamekuwa kero mno nyumbani kwangu,wamehamia kwenye dari kila nikiziba wanatafuta upenyo wanaingia,nikiziba wanalala kwenye bati mpaka wapate pa kuingilia,nimeshapiga sana manati hawaondoki,wanafanya uharibifu mkubwa hadi wanakera,ninawahamishaje hawa??ni wa kufugwa ila ndio wamehama makwao kuja kuweka makazi kwangu.,naombeni ushauri tafadhali
 
Naombeni kujua hii ina maana au inaashiria nini.

Ni kwamba wakati najenga kibanda changu nilipomaliza kupaua siku kadhaa baadae nilikuja gundua kuna njiwa wa porini wamejenga kiota ktk mbao za paa kwa ndani.

Baada ya kuziba kwa kuzunguka nje na baadae kuhamia wale njiwa waliondoka, ila nimegundua kuna ndege wengine wamenjenga pembeni ya nyumba, na baadae km miezi mitano mbele wale njiwa wamerud na wamejenga kiota chao pembeni kwa nje karibu na kenopi.

Sijapata tatizo lolote wala usumbufu wowote kwani pia napenda hawa viumbe.

Ninachotaka kujua kama kuna mahusian yoyote na mambo ya kiroho.
Aiseee unabahati sana najaribu kila njia ndege wagamie kwangu imeshindikana
 
Ooooh real?
njiwa anapenda amani na upendo, ndio maana hawezi jenga sehem inayohatarisha maisha yake na ya watoto wake.

Mimi nyumba ya babu yangu tangu tunakuwa kuna njiwa tena wale wakubwa walikuwa wamejenga hadi leo wapo, so huwa anavuna tu akiamua kula njiwa

So, relax mkuu
 
Hawa ndege wamekuwa kero mno nyumbani kwangu,wamehamia kwenye dari kila nikiziba wanatafuta upenyo wanaingia,nikiziba wanalala kwenye bati mpaka wapate pa kuingilia,nimeshapiga sana manati hawaondoki,wanafanya uharibifu mkubwa hadi wanakera,ninawahamishaje hawa??ni wa kufugwa ila ndio wamehama makwao kuja kuweka makazi kwangu.,naombeni ushauri tafadhali
Tengeneza banda ulitundike sehemu ili kuzuia wasiingie kwenye dari wakae bandani. Basi, kwa kifupi fanya kama ni wa kwako unawafuga.
 
Kwa imani za Kiislamu njiwa ni ndege wa baraka, Warabu wengi wanafuga ndege aina ya Njiwa kwa kuamini kuwa, baraka kama za Utajiri, au kulindwa na mabaya..

Mkuu waenzi na uwalinde hao Ndege, wewe ni mtu mwema ndio sababu ya hao Ndege kujenga kwako, njiwa wanahisia nyingi, wameshaona wewe ni mtu wa aina gani
 
Nijuavuo mim ndege hao njiwaa huto ishara ya jambo likitokeaa mfno kifo au msiba hawezi kuruka ndipo utaona kuna jambo litatokeaa nao pia hukosa furah ya kurukaruka watatuliaa kwenye viota vyao hadi msiba ule uuishe
 
Wewe ndio uliwakuta ukakata miti na kuharibu nyumba zao.
Sasa wape nafasi nao tena wawekee na maji na kila asubuhi mtama jioni wali
Safi sana, na nyongeza ni kuwa hao ni viumbe kama viumbe wengine hapo kwako wamepapenda tu usianze kuingiza tafakuri nyingine utajikuta unafungua mlango mwengine ambao usije weza ufunga.
Wakirimu uwezavyo na taraji malipo yako toka kwa aliyekuumba wewe na hao ndege,usije ukataraji madhara au faida kutoka kwa hao ndege.
 
Mkuu nakuonea wivu... laiti ningekuwa mimi. Ndege siku zote huchagua kuweka viota vyao sehemu ambazo wanaona ni salama kwa wao na mayai/makinda yao. Japo siamini imani potofu lkini kwangu mimi naona mnyama au ndege wa porini anapoamini yupo salama anapokuwa kwenye mazingira ya nyumbani kwako basi ni baraka tena! Ushauri: Ikiwezekena boresha maeneo waliyowekea viota ili waongezeke. Niliwahi kwenda kutembelea mzungu mmoja ambaye nyumba yake ilikuwa na maua mengi mpaka yakawa kama kichaka hivi. Basi kulikuwa na bata maji waliotoka ziwani wakatagia kwenye maua. Jamaa alikuwa na furaha ya ajabu na ukitaka kukosana nae basi uwabughudhi wale mabata!
Siku mzee koboko akiweka makazi kwa mmoja wetu sijui itakuwa baraka au.....
 
Kawaida njiwa hawezi kukaa sehemu yenye kelele na ugomvi, hivyo basi nyumba yako ina amani kiasi cha ndege mwenye baraka za kiroho kujenga makazi kwako.
Endelea kuweka mazingira rafiki maana kuna mazuri mengi utapata.
 
Mimi bwana wale njiwa wa kufugwa wawatu sijui wanatoka wapi wanajaa juu ya paa langu na kushuka chini kula pumba za kuku wangu wanashinda siku nzima kwangu mpaka wenye nao wanakasilika
 
Mimi bwana wale njiwa wa kufugwa wawatu sijui wanatoka wapi wanajaa juu ya paa langu na kushuka chini kula pumba za kuku wangu wanashinda siku nzima kwangu mpaka wenye nao wanakasilika
Kwako wanafwata msosi hao na ukiwapatia mtama hawatoki tena hao
 
Back
Top Bottom