Ndege Njiwa amejenga pembeni ya nyumba yangu!

Kipindi cha Nuhu, njiwa alitumika kama ishara ya kuonyesha dunia imefikia hali yake, Roho Mtakatifu alikuja kama Huwa kwa wale Thenashara....ni ishara njema na ya Bahati kuwa na njiwa pori katika Nyumba yako. Biliv
 
Unamahaba ya njiwa wewe.....lakini nasikia wengine hufuga njiwa kwaanili ya kuwatuma kupeleka uchawi mahali
 
Katumwa huyo akufuatilie na kukupeleleza.

Njia peleka habari...
 
Naombeni kujua hii ina maana au inaashiria nini.

Ni kwamba wakati najenga kibanda changu nilipomaliza kupaua siku kadhaa baadae nilikuja gundua kuna njiwa wa porini wamejenga kiota ktk mbao za paa kwa ndani.

Baada ya kuziba kwa kuzunguka nje na baadae kuhamia wale njiwa waliondoka, ila nimegundua kuna ndege wengine wamenjenga pembeni ya nyumba, na baadae km miezi mitano mbele wale njiwa wamerud na wamejenga kiota chao pembeni kwa nje karibu na kenopi.

Sijapata tatizo lolote wala usumbufu wowote kwani pia napenda hawa viumbe.

Ninachotaka kujua kama kuna mahusian yoyote na mambo ya kiroho.
Mkuu nakuonea wivu... laiti ningekuwa mimi. Ndege siku zote huchagua kuweka viota vyao sehemu ambazo wanaona ni salama kwa wao na mayai/makinda yao. Japo siamini imani potofu lkini kwangu mimi naona mnyama au ndege wa porini anapoamini yupo salama anapokuwa kwenye mazingira ya nyumbani kwako basi ni baraka tena! Ushauri: Ikiwezekena boresha maeneo waliyowekea viota ili waongezeke. Niliwahi kwenda kutembelea mzungu mmoja ambaye nyumba yake ilikuwa na maua mengi mpaka yakawa kama kichaka hivi. Basi kulikuwa na bata maji waliotoka ziwani wakatagia kwenye maua. Jamaa alikuwa na furaha ya ajabu na ukitaka kukosana nae basi uwabughudhi wale mabata!
 
Kuna kitu nimepata kwako, thank, nitawaboreshea mazingira.
 
Naombeni kujua hii ina maana au inaashiria nini.

Sijapata tatizo lolote wala usumbufu wowote kwani pia napenda hawa viumbe.

Ninachotaka kujua kama kuna mahusian yoyote na mambo ya kiroho.
hiyo ni bahati, ningekuwa ni mimi hapo mboga imekuja yenyewe ningekumbusha zangu za vijijini enzi zileee, tena njiwa wa pori anakuwa mkubwa na ana nyama kuliko wa kufugwa. ningemwotea tu amelala namkamata kumnyonyoa, naandaa pilipili ya unga na chumvi, ndimu/limao, bizari na moto wa mkaa. nachonga fimbo nyembamba afu namchomeka kuanzia chini hadi juu na kumpakaa hivyo vitu vyote abanikwe kwa polepole, hamna haraka. akiiiva nakumbushia maisha yangu ya utoto yooote. kwasababu utoto wangu nimewinda sana hao.
 
Mmmh hivi kweli umekua? Mbona km bado enzi zako za kuwinda hujaacha
 
Kwa zanzibar ndege ni ishara bora na wenye baraka watu uwapa vyakula kuwalisha kama sadaka maana nao ni viumbe, hupasw kuwakamata na kuwala wapaswa wakae salama.

wanunulie mtama uwe unawamwagia watakula na kufurah na ww utabarikiwa na nyumba inakuwa na baraka.

Sadaka sio lazima umpe binadamu hata kulisha ndege ja viumbe vingne ni sadaka pia.

Njiwa au ndege wapende na watunze.
 
Porini hakuna ishu wanafuata ela za makinikia si wamesikia kuna noah za bure mjini[jokes],mkuu weka imani yako kwa Mungu pekee
 
Back
Top Bottom